Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MIUJIZA! Ubingwa EPL unapopishana na Ngao ya Jamii

MUUJIZA Pict

Muktasari:

  • Ngao ya Jamii ya FA 2026 ilichezwa mwishoni mwa wiki hii iliyopita, Agosti 16, ambapo mabingwa wa EPL msimu wa 2025/26, Arsenal, walikutana na Manchester City, mabingwa wa Kombe la FA msimu huo, kwenye Uwanja wa Principality, Cardiff, ambapo Washika Mitutu waliondoka na ushindi wa mabao 3-0.

LONDON, ENGLAND: NGAO ya Jamii ni mchezo wa jadi wa kufungua msimu wa soka duniani kote katika miaka ya karibuni. Lakini, unaweza kuwa kiashiria kizuri cha timu itakayoshinda taji la Ligi Kuu England (EPL)?

Ngao ya Jamii ya FA 2026 ilichezwa mwishoni mwa wiki hii iliyopita, Agosti 16, ambapo mabingwa wa EPL msimu wa 2025/26, Arsenal, walikutana na Manchester City, mabingwa wa Kombe la FA msimu huo, kwenye Uwanja wa Principality, Cardiff, ambapo Washika Mitutu waliondoka na ushindi wa mabao 3-0.

Ikichukuliwa kama mchezo wa jadi wa kufungua msimu wa ligi kuu, Ngao ya Jamii, ambayo awali kwa England ilijulikana kama Charity Shield, ilichezwa kwa mara ya kwanza 1908 na mwaka huu ulikuwa ni mchezo wa 104 ya nchi hiyo.

Iwapo Ngao ya Jamii ni mchezo wa ushindani au la, inategemea mtazamo wa mtu binafsi. Mchezo huo huipa timu nafasi ya kuongeza kombe kwenye kabati la mataji, lakini kwa hakika hauhesabiwi kama mojawapo wa mataji makubwa. Kwa vyovyote vile, je, Ngao ya Jamii ni kiashiria kizuri cha mafanikio ambayo timu inaweza kupata katika Ligi Kuu England msimu husika?

MUUJI 01

ZIPI ZIMEBEBA NGAO, EPL MSIMU MMOJA?

Katika michezo 34 ya Ngao ya Jamii iliyochezwa tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu England msimu wa 1992/93, ni timu nane tu zilizoshinda Ngao ya Jamii ambazo baadaye ziliendelea na kutwaa ubingwa wa ligi msimu huohuo ikiwa ni sawa na chini ya robo moja, asilimia 24.

Hakuna hata moja kati ya mabingwa sita wa mwisho wa Ngao ya Jamii aliyekwenda kushinda taji la EPL katika msimu huohuo. Ni timu moja tu kati ya 15 zilizoshinda Ngao ya Jamii katika kipindi hicho iliyoweza pia kutwaa EPL ambayo ni Manchester City 2018/19.

MUUJI 02

MABINGWA NGAO NA MABINGWA EPL

Mfano mwingine unaoweza kuonyesha kwamba Ngao ya Jamii huenda isiwe kiashiria kizuri cha mafanikio ya msimu unaofuata unatokana na mchezo wa mwaka 2022 kati ya Liverpool na Manchester City.

Erling Haaland alicheza mchezo wa kukatisha tamaa. Ulikuwa mchezo wake wa kwanza kwenye ardhi ya England baada ya kujiunga na Manchester City akitokea Borussia Dortmund, na alicheza dakika zote 90 bila kufunga katika nafasi tatu alizopata. Moja kati ya hizo ilikuwa ya wazi, lakini alipiga mpira uliogonga mwamba wa juu wa lango.

Darwin Nunez ambaye aliingia akitokea benchi na kucheza mchezo wake wa kwanza wa Liverpool akiwa amebakiza zaidi ya dakika 30, alisababisha penalti na kufunga bao la tatu la Liverpool katika ushindi wa 3-1.

Hata hivyo, mchezo huo haukuwa ishara ya kile kilichokuja kutokea baadaye. Vilevile Haaland alivunja rekodi ya mabao mengi zaidi katika msimu mmoja wa EPL akifunga mabao 36, na alifunga jumla ya mabao 52 katika mashindano yote 2022/23 akiisaidia Manchester City kutwaa mataji matatu.

Kwa upande mwingine, Nunez alifunga mabao tisa pekee katika EPL, huku Liverpool ikimaliza msimu ikiwa nafasi ya tano na bila taji lolote zaidi ya Ngao ya Jamii. Ubingwa wa Manchester City katika ligi msimu huo ni miongoni mwa matukio 10 ambayo timu iliyopoteza Ngao ya Jamii iliendelea na kushinda EPL katika msimu huohuo.

Hiyo ni mara nyingi zaidi kuliko timu zilizoshinda Ngao ya Jamii ambazo zimefanikiwa kufanya hivyo zikiwa ni nane. Timu nne kati ya saba zilizopoteza Ngao ya Jamii katika misimu ya hivi karibuni zimeendelea na kushinda EPL katika msimu huohuo ambazo ni  Liverpool 2019/20 na Manchester City katika misimu ya 2021/22, 2022/23 na 2023/24.

Manchester City ilimaliza hatimaye mfululizo wa kushinda michezo mitatu ya Ngao ya Jamii baada ya kuwafunga wapinzani wao Manchester United kwa penalti msimu wa 2024/25, lakini ilishindwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.

Kwa kifupi; historia inaonyesha kuwa kushinda Ngao ya Jamii siyo uhakika wa kutwaa EPL. Katika enzi ya EPL ni timu nane tu kati ya 34 (24%) zilizoshinda Ngao ya Jamii na baadaye kutwaa ubingwa wa ligi katika msimu huohuo. Cha kushangaza zaidi, timu zilizopoteza Ngao ya Jamii zimefanikiwa kutwaa EPL mara 10.

MUUJI 03

HAWA HAPA WENYEWE

Msimu wa kwanza kabisa wa Ligi Kuu England 1992/93 Manchester United ilibeba ubingwa wa ligi, huku Leeds United ikitwaa Ngao ya Jamii;

1993/94 Man United ilibeba EPL na Ngao ya Jamii kwa pamoja; 1994/95 Blackburn Rovers (EPL) ilhali Ngao ya Jamii ikienda Man United na

1995/96 Man United ilibeba Ligi Kuu huku Ngao ya Jamii ikichukuliwa na Everton.

Katika msimu wa 1996/97 Manchester United ilichukua Ligi Kuu na Ngao ya Jamii, huku 1997/98 Arsenal ikibeba Ligi Kuu na Ngao ya Jamii ikachukuliwa na Manchester United; 1998/99 Manchester United ilichukua EPL na Arsenal ikabeba Ngao ya Jamii; 1999/00 Manchester United ilibeba EPL na Ngao ya Jamii ikachukuliwa na Arsenal; 2000/01 Manchester United ilibeba EPL, Ngao ya Jamii ikaenda Chelsea.

Msimu wa 2001/02 Arsenal ilibeba EPL, Ngao ya Jamii ikawa ya Liverpool; 2002/03 Manchester United (EPL) na Arsenal (Ngao ya Jamii); 2003/04 Arsenal (EPL), Manchester United (Ngao ya Jamii); 2004/05 Chelsea (EPL), Arsenal (Ngao ya Jamii); 2005/06 Chelsea (EPL), Chelsea (Ngao ya Jamii) na 2006/07 Manchester United (EPL), Liverpool (Ngao ya Jamii).

Kwenye msimu wa 2007/08 Manchester United (EPL na Ngao ya Jamii); 2008/09 Manchester United (EPL na Ngao ya Jamii); 2009/10 Chelsea (EPL na Ngao ya Jamii); 2010/11 Manchester United (EPL na Ngao ya Jamii); 2011/12 Manchester City (EPL), Manchester United (Ngao ya Jamii);

2012/13 Manchester United (EPL), Manchester City (Ngao ya Jamii).

Msimu wa 2013/14 Manchester City (EPL), Manchester United (Ngao ya Jamii); 2014/15 Chelsea (EPL), Arsenal (Ngao ya Jamii); 2015/16 Leicester City (EPL), Arsenal (Ngao ya Jamii); 2016/17 Chelsea (EPL), Manchester United (Ngao ya Jamii); 2017/18 Manchester City (EPL), Arsenal (Ngao ya Jamii); 2018/19 Manchester City (EPL), Manchester City (Ngao ya Jamii) na 2019/20 Liverpool (EPL), Manchester City (Ngao ya Jamii).

Katiika 2020/21 Manchester City (EPL), Arsenal (Ngao ya Jamii); 2021/22 Manchester City (EPL), Leicester City (Ngao ya Jamii); 2022/23   Manchester City (EPL), Liverpool (Ngao ya Jamii); 2023/24 Manchester City (EPL), Arsenal (Ngao ya Jamii); 2024/25 Liverpool (EPL), Manchester City (Ngao ya Jamii); 2025/26 Arsenal (EPL), Crystal Palace (Ngao ya Jamii) na 2026/27 Arsenal (Ngao ya Jamii); Ubingwa EP nani?