Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miamba iliyocheza mechi nyingi Kombe la Dunia

MIAMBA Pict

Muktasari:

FAINALI za Kombe la Dunia 2026 zimefshachezwa mechi tatu kwa kila timu hadi sasa. Lakini, nyuma ya fainali hizo kuna mastaa waliocheza mechi nyingi hadi sasa katika mashindano hayo na hawa ndio waliotoa shoo kwa muda mrefu.

WASHINGTON, MAREKANI: FAINALI za Kombe la Dunia 2026 zimefshachezwa mechi tatu kwa kila timu hadi sasa. Lakini, nyuma ya fainali hizo kuna mastaa waliocheza mechi nyingi hadi sasa katika mashindano hayo na hawa ndio waliotoa shoo kwa muda mrefu.

MIAM 01

LIONEL MESSI (ARGENTINA MECHI 28)

Huyu mwamba amechezea michuano ya Kombe la Dunia iliyopigwa 2006, 2010, 2014, 2018, 2022 na 2026.

Kuna nini kingine cha kusema kuhusu Lionel Messi? Mshindi huyo wa tuzo ya mchezaji bora (Ballon d’Or) mara nane aliweka historia ya soka kwa kuvunja rekodi ya muda wote ya mechi za Kombe la Dunia katika fainali za 2022, mashindano ambayo, hatimaye, yaliisha kwa ushindi wa nchi yake kubeba ubingwa.Katika fainali hizo za 2022 uchezaji wake ulifanana na ule wa hayati Diego Maradona 1986, ambaye pia alilipeleka kombe Argentina huko Mexico.

Kwa miaka mingi kulikuwa na swali lililorudiwa. Je, Messi angeweza kweli kuchukuliwa kama staa bora zaidi wa wakati wote kama asingeshinda taji kubwa zaidi?

Mwaka 2006, Messi aliachwa benchi kwa utata wakati Argentina ilipotolewa na Ujerumani katika robo fainali, huku kocha Jose Pekerman akikosolewa kwa kutompa nafasi nyota wake huyo alipokiwa na umri wa miaka 19.

Miaka minne baadaye, Ujerumani waliitoa Argentina, lakini safari hii kwa kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Afrika Kusini chini ya Diego Maradona, ikiwa ni kipigo kikubwa zaidi cha Argentina katika Kombe la Dunia tangu 1974.

Kisha likaja pigo 2014, ambapo Ujerumani tena walimnyima Messi taji. Mwaka 2018, Argentina iliondolewa katika mchezo wa kusisimua wa mabao 4-3 dhidi ya mabingwa watetezi Ufaransa katika hatua ya 16 bora.

Moja ya ukosoaji wa mara kwa mara kuhusu Messi katika Kombe la Dunia ulikuwa kushindwa kwake kufunga katika hatua za mtoano. Licha ya kucheza dakika 756 na kupiga mashuti 23 katika mechi za mtoano kabla ya 2022, hakuwahi kufunga katika hatua hizo.

Lakini, Qatar, Messi alibadilisha simulizi. Alikuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya Kombe la Dunia kufunga katika hatua ya makundi, 16 bora, robo fainali, nusu fainali na fainali katika fainali moja alipoiwezesha Argentina kushinda moja ya fainali bora zaidi kuwahi kutokea dhidi ya Ufaransa kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya 3-3. Na kwa mechi zake za 2026, Messi ameongeza rekodi yake kileleni, na pia akawa mchezaji wa kwanza kushiriki katika matoleo sita tofauti ya Kombe la Dunia.


MIAM 02

LOTHAR MATTHAUS (UJERUMANI, MECHI 25)

Matthaus alicheza michuano ya 1982, 1986, 1990, 1994 na 1998 na kwa mafanikio ya Ujerumani haishangazi kumuona mchezaji wao mwenye mechi nyingi zaidi, Lothar Matthäus, akiwa juu kwenye orodha hiyo. Safari yake ilianza 1982 akiwa na nafasi chache, na ikaisha 1998 alipoitwa kama mbadala. Lakini, kati ya nyakati hizo kulikuwa na mafanikio makubwa.

Matthaus aliiongoza Ujerumani Magharibi kutwaa Kombe la Dunia 1990. Aliicheza dakika zote za michuano hiyo na kuwa mfungaji bora wa timu yake akiwa na mabao manne. Baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Argentina fainali, alinyanyua kombe kama nahodha na ilikuwa tu baada ya ushindi huo alipotunukiwa tuzo ya Ballon d’Or.


MIAM 03

MIROSLAV KLOSE (UJERUMANI MECHI 24)

Klose alicheza michuano ya 2002, 2006, 2010 na 2014 na ndiye aliyekuwa mfungaji bora wa muda wote wa Kombe la Dunia, akiwa na mabao 16 katika mechi 24 sawa na Messi aliyeifikia rekodi hiyo mwaka huu.

Nyota huyo alianza kuwaka katika michuano ya 2002 akianza vizuri kwa hat-trick dhidi ya Saudi Arabia. Ni mmoja wa wachezaji 13 waliofunga hat-trick katika mechi za kwanza tu za Kombe la Dunia.

Mwaka 2014 ulikuwa wa mwisho kwake na wa kihistoria, alipovunja rekodi ya mabao 16 dhidi ya Brazil katika ushindi wa 7-1. Alimaliza baada ya kuingia kama ‘sub’ wa Mario Gotze aliyefunga bao la ushindi fainali.


MIAM 04

CRISTIANO RONALDO (URENO, MECHI 24)

Nyota yake imewaka katika michuano ya Kombe la Dunia 2006, 2010, 2014, 2018, 2022 na 2026, lakini tayari Ronaldo amefikisha mechi 24, na alicheza mechi iliyopita ya Kombe la Dunia 2026 akiwa na umri wa miaka 41 na siku 138. Mchezaji huyo ni mmoja wa wachezaji wawili pekee walishiriki mashindano sita ya Kombe la Dunia.


MIAM 05

PAOLO MALDINI (ITALIA, MECHI 23)

Paolo Maldini alicheza mechi za michuano ya 1990, 1994, 1998 na 2002 akiwa nguzo ya ulinzi wa Italia, lakini hakuwahi kushinda Kombe la Dunia. Alianza 1990 akicheza mechi zote saba na Italia ilifika nusu fainali, lakini ikaondolewa na Argentina kwa penalti. Mwaka 1994 walifika fainali lakini wakapoteza kwa penalti dhidi ya Brazil. Mwaka 1998 na 2002 pia walitolewa mapema na mwisho ikiwa ni dhidi ya Korea Kusini.