Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa wanaoongoza kwa kila timu EPL 2025/26

MASTAA Pict

Muktasari:

  • Wanasoka wanaolipwa mishahara mikubwa kwenye Ligi Kuu England kwa msimu huu wa 2025–26, wengi wanafahamika, lakini wapya wapo pia, huku wachezaji wakilipwa viwango vinavyoshtua.

LONDON, ENGLAND: MASTAA wa Ligi Kuu England ni miongoni mwa wanamichezo wanaolipwa pesa nyingi zaidi duniani. Kuna baadhi wanalipwa pesa nyingi kuliko inayolipwa kwa kikosi kizima kwa baadhi ya timu.

Wanasoka wanaolipwa mishahara mikubwa kwenye Ligi Kuu England kwa msimu huu wa 2025–26, wengi wanafahamika, lakini wapya wapo pia, huku wachezaji wakilipwa viwango vinavyoshtua.

Ipswich, Southampton na Leicester zimeshuka. Burnley, Leeds na Sunderland zimepanda, lakini majina mengine yale maarufu bado yanatawala kwenye ligi.

Kwa mujibu wa Capology, hii hapa orodha ya vinara wa mishahara mikubwa kwenye kila timu inayoshiriki Ligi Kuu England msimu huu.

MASTA 01

Arsenal – Kai Havertz (Pauni 280,000 kwa wiki)

Havertz anaendelea kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi ya wengine wote Arsenal na kwa mwaka anapokea Pauni 14.5 milioni. Kwenye umri wa miaka 26 anaingia kwenye kilele cha soka lake.


Aston Villa – Youri Tielemans (Pauni 150,000 kwa wiki)

Huko Villa Park kuna mastaa watatu, Boubacar Kamara, Emiliano Martinez na Youri Tielemans wanalipwa kiwango sawa cha mshahara, Pauni 150,000 kwa wiki na ndiyo wanaolipwa mshahara mkubwa.


Bournemouth – Evanilson (Pauni 85,000 kwa wiki)

Bournemouth ilivunja rekodi yao ya uhamisho ilipomsajili straika wa Kibrazili, Evanilson kutoka Porto mwaka 2024 na kumpa mshahara mkubwa. Staa huyo aliyefunga mabao 10 katika mechi 31 za ligi, analipwa Pauni 85,000 kwa wiki.


Brentford – Aaron Hickey (Pauni 70,000 kwa wiki)

Baada ya kuwa nje kwa mwaka mzima kutokana na kuwa majeruhi, Hickey alirejea uwanjani Mei mwaka huu na amejiweka pazuri akiwa chaguo la kwanza la beki wa kati. Ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa huko Brentford.


Brighton – Ferdi Kadioglu (Pauni 87,500 kwa wiki)

Brighton ilimfanya Kadioglu kuwa usajili wao wa rekodi Agosti 2024, ilipolipa Pauni 29.2 milioni kupata huduma yake. Alifunga mabao kwenye Kombe la Ligi na Ligi Kuu England na analipwa Pauni 4.5 milioni kwa mwaka.

MASTA 02

Burnley – Lesley Ugochukwu (Pauni 50,000 kwa wiki)

Huko Burnley mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa ni usajili wao wa dirisha hili la Ugochukwu, ambaye alinaswa kutoka Chelsea kwa mkataba wa miaka mitano baada ya mkopo Southampton. Kiungo huyo Mfaransa ni bosi Burnley.


Chelsea – Reece James (Pauni 250,000 kwa wiki)

Nahodha wa Chelsea anabaki kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa kwenye Ligi Kuu England akipokea Pauni 13 milioni kwa mwaka. James alicheza mechi 19 tu za ligi msimu uliopita kutokana na kuwa majeruhi.


Crystal Palace – Daichi Kamada (Pauni 105,000 kwa wiki)

Kamada anakuwa mchezaji wa kwanza wa Kijapani kikosini Crystal Palace aliponaswa kutoka Lazio mwaka 2024 na kuonyesha kiwango bora na hivyo kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa, Pauni 5.4 milioni kwa mwaka.


Everton – Jordan Pickford (Pauni 125,000 kwa wiki)

Kipa namba 1 wa England, Jordan Pickford ndiye anayeongoza kwa kulipwa mshahara mkubwa Everton na mkataba wake utafika mwisho 2027. Pickford ni mchezaji bora wa mwaka wa Everton, analipwa Pauni 6.5 milioni kwa mwaka.


Fulham – Bernd Leno (Pauni 130,000 kwa wiki)

Leno amekuwa na kiwango bora tangu alipojiunga na Fulham akitokea Arsenal mwaka 2022, akicheza mechi 112 za Ligi Kuu England kwa misimu mitatu. Mkataba wake utakwisha 2027 na analipwa Pauni 6.8 milioni kwa mwaka.


Leeds United – Jack Harrison (Pauni 90,000 kwa wiki)

Miaka mitano baada ya kuisaidia Leeds United kurudi kwenye Ligi Kuu England, mashabiki walivutiwa na kiwango cha Harrison. Hata baada ya usajili wa Dominic Calvert-Lewin, Harrison anaendelea kuwa kinara wa mshahara Leeds.

MASTA 03

Liverpool – Mohamed Salah (Pauni 400,000 kwa wiki)

Akitokea kuipa Liverpool taji la Ligi Kuu England na yeye kushinda Kiatu cha Dhahabu, Mo Salah ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa huko Anfield, akipokea zaidi ya Pauni 20 milioni kwa mwaka.


Man City – Erling Haaland (Pauni 525,000 kwa wiki)

Akiwa na mkataba mrefu zaidi kwenye historia ya Ligi Kuu England, ambapo utakwisha 2034, Haaland analipwa Pauni 27.3 milioni kwa mwaka. Straika huyo wa Norway alifunga mabao 22 msimu uliopita na bado ni tishio kubwa uwanjani.


Man United – Casemiro (Pauni 350,000 kwa wiki)

Mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa Man United ni kiungo Casemiro, ambaye anapokea Pauni 18.2 milioni kwa mwaka. Mbrazili huyo alikosolewa kutokana na ubora wake, lakini alituliza daruga zake kubaki Old Trafford kusaidia timu yake.


Newcastle United – Bruno Guimaraes (Pauni 160,000 kwa wiki)

Nahodha wa Newcastle United ndiye moyo wa safu ya kiungo ya timu hiyo, Bruno Guimaraes na ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa, akipokea Pauni 8.3 milioni kwa mwaka. Aliisaidia timu kubeba Kombe la Ligi.


Nottingham Forest – Morgan Gibbs-White (Pauni 150,000 kwa wiki)

Nahodha wa Nottingham Forest alisaini mkataba wa miaka mitatu Julai 2025 baada ya Tottenham kujaribu kumsajili na kushindwa. Kwenye dili jipya ndiko ambako lamba dili tamu, akilipwa Pauni 7.8 milioni kwa mwaka.


Sunderland – Granit Xhaka (Pauni 100,000 kwa wiki)

Akitokea kuwa nahodha Bayer Leverkusen na kubeba ubingwa wa Bundesliga bila ya kupoteza, Granit Xhaka amerejea kwenye Ligi Kuu England kujiunga na Sunderland. Amesaini miaka mitatu na analipwa Pauni 5.2 milioni kwa mwaka.

MASTA 04

Tottenham – James Maddison (Pauni 170,000 kwa wiki)

Nahodha wa Totenham Hotspur analipwa Pauni 8.8 miolioni kwa mwaka, lakini aliumia kwenye kipindi cha pre-season na huenda akakosa msimu wote wa 2025/26. Maddison ni bora anapokuwa fiti na ndiyo maana mshahara mkubwa.


West Ham – Jarrod Bowen (Pauni 150,000 kwa wiki)

Kwa sasa ndiye nahodha wa klabu, Jarrod Bowen anaendelea kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa, Pauni 7.8 milioni kwa mwaka. Winga huyo alivuka ma bao 100 kwenye Ligi Kuu England katika maisha ya soka lake.


Wolves – Fabio Silva (Pauni 80,000 kwa wiki)

Usajili wa rekodi wa Wolves ni Fabio Silvaakirejea kwenye Ligi Kuu England baada ya kucheza kwa mkopo Las Palmas, alipofunga mabao 10 kwenye La Liga ikiwamo moja dhidi Barcelona. Mshahara wake, Pauni 4.16 milioni kwa mwaka.