Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashujaa na mtazamo mpya Ligi Kuu

MASHUJAA Pict

Muktasari:

  • Mwanaspoti limezungumza na uongozi wa timu hiyo, wachezaji na kocha ili kujua wamejipangaje kuanza msimu mpya, kauli yao kuu ni wamejipanga kukabiliana na ushindani utakaokuwepo dhidi ya timu pinzani.

KITENDO cha Mashujaa kumaliza nafasi ya 11 na pointi 33, mabao ya kufunga 15 yalitikiswa mara 27 nyavuni msimu uliopita wa 2025/26, kilikuwa kama alamu ya kujipanga zaidi kuhakikisha Ligi Kuu inayoanza leo Agosti 14,2026 inafanya vizuri.

Mwanaspoti limezungumza na uongozi wa timu hiyo, wachezaji na kocha ili kujua wamejipangaje kuanza msimu mpya, kauli yao kuu ni wamejipanga kukabiliana na ushindani utakaokuwepo dhidi ya timu pinzani.

MASHUJ 01

MAANDALIZI

Meneja wa timu hiyo, Athuman Amir anayazungumzia maandalizi yaliyofanywa chini ya kocha Amani Josiah na mechi za kirafiki zilizochezwa, anaamini zimewasaidia kuwaandaa wachezaji na kuwaweka fiti.

Anasema jumla ya mechi ilizocheza Mashujaa 1-0 Tanzania Prisons(Dar es Salaam), Mashujaa 6-1 Temeke Combine (Dar),Mashujaa 1-0 Namungo(Babati),Mashujaa 1-1 Kagera Sugar(Arusha),Mashujaa 4-0 Mbuni (Arusha) na Mashujaa 1-0 TRA(Arusha.).

"Naamini timu tulizocheza nazo mechi za kirafiki zina ushindani mkali, makocha watakuwa wamefanikiwa kupata kile ambacho walitaka kukiona kwa wachezaji, kabla ya kuanza kucheza mechi za ligi," anasema meneja na kuongeza;

"Tumefanya maboresho ya wachezaji kuna waliotoka na walioingia, mabadiliko ya benchi la ufundi, hivyo tunaamini msimu utakuwa wa ushindani mkali na tupo tayari kwa mapambano, hatutaki yajirudie ya msimu uliopita ambapo tulikuwa tunacheza kwa presha ya kupambana kusalia Ligi Kuu."

Anasema benchi la ufundi lina kocha mkuu Josiah, msaidizi wake ni Charles Fred ,meneja Athuman Athuman, kocha wa fitinesi Aman Kyata, kocha wa magolikipa Abdulkarim Mtumwa, daktari Novat Kalabi na kiti meneja John Pangan.

MASHUJ 02

WACHEZAJI WALIYOTOKA

Wachezaji waliyoondoka kikosini anawataja ni Swig Karihe,

⁠Yusuph Dunia, ⁠Erick Johola, ⁠Suwed Juma, ⁠Frank Magingi, ⁠Dany Lyanga, ⁠Jafar Kibaya, ⁠Mudathir Said, ⁠David Ulomi na ⁠Hasan Haji.


WALIYOINGIA

Musa Malika, ⁠Michael Joseph, ⁠Tariq Simba, ⁠Omari Mponda, ⁠Said Naushad, ⁠Hassan Kabunda,⁠Mishamo Daud,⁠Venance Leonard, ⁠Chinkson Ruben, ⁠Fadhil Mahimbo, ⁠Hijah Shamte,⁠Abdul Mangalo, ⁠Abdullah Mfuko,⁠Machela Julius na ⁠Hasan Gumbo.

"Naamini wachezaji wapya wataongeza nguvu wakisaidiana na waliokuwepo na timu,kuipambania timu kumaliza msimu ikiwa nafasi ya juu, natamani tufanye vizuri kama ilivyokuwa msimu wa 2024/25 ambapo timu ilimaliza nafasi ya saba ikiwa na pointi 35 pia tulipata wachezaji wengi ambao walichukua tuzo za mchezaji bora wa mechi zaidi ya 15," anasema.

MASHUJ 03

KAULI YA KOCHA

Kocha Josiah ambaye msimu uliopita alikuwa na Dodoma Jiji na sasa ataiongoza Mashujaa anasema:"Nitaanza msimu na chalenji mpya, naamini nitafanya vizuri nikiwa na Mashujaa, maandalizi yamefanyika, wachezaji wamekuwa wepesi wa kuzishika mbinu ninazowalelekeza."

Kwa upande wa wachezaji, kiungo wa timu hiyo Salum Kihimbwa anasema:"Naamini utakuwa msimu mzuri, maana uliopita nilipitia changamoto ya majeraha ya hapa na pale na sasa nipo fiti."