Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa Mangungu, nimewaelewa mashabiki wa Simba

ZENGWE Pict


NIMEKUWA Napata shida kuwaelewa mashabiki wanaomshambulia Mwenyekiti wa Simba Sports Club, Murtazar Mangungu kuhusu mwenendo mbaya wa timu hiyo kimataifa na mwendelezo wa klabu hiyo kuukosa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mwaka wa nne mfululizo, huku hali ikionekana kama inaweza kujirudia msimu huu.


Kila kunapotokea jambo baya, hasira za mashabiki huamka na mara moja jina la Mangungu hujaa midomoni mwao, wakimhusisha na tatizo hilo. Lakini mara zote, mashabiki hao hushindwa kueleza Mangungu amehusikaje katika jambo hilo baya.


Wanapolazimika kumwaga sifa, basi jina la mwekezaji wa klabu hiyo, Mohamed Dewji hufurika midomoni mwao, hasa wanapoambiwa klabu imesajili nyota ama kutoka Afrika Magharibi, Kusini au hata hapo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Lakini mchezaji huyo akija nchini na kutoonyesha makali yoyote, jina la Mangungu hurejea midomoni mwao na kusahau walihusisha mafanikio ya kumsajili nyota huyo na tajiri wao.

Jambo baya zaidi walilofanya ni hili la kumzonga Mangungu mara baada ya mechi ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyoisha kwa sare ya mabao 2-2, matokeo yanayoifanya Simba iokote pointi yake moja ya kwanza katika mechi nne, na huku zikiwa zimesalia mechi mbili, matumaini ya kufika robo fainali ni kama yamekwisha.

ZENG 01

Unashangaa sababu za mwenyekiti wa klabu hiyo kuwa mbuzi wa kafara katika matukio mabaya na kusahauliwa katika matukio mazuri.

Mangungu hakusifiwa wakati timu ilipojitutumua hadi kufika fainali ya Kombe la Shirikisho msimu uliopita. Mafanikio hayo hayahusishwi kabisa na uongozi au uenyekiti wake, bali uwekezaji.

Simba ni klabu ambayo imeamua kufanya mageuzi katika umiliki na mfumo wake wa uongozi. Lakini mchakato huo bado haujafikia mwisho kutokana na vikwazo vya kisheria kuhusu idadi ya wawekezaji wanaotakiwa kununua hisa ili wawe wamiliki na klabu kuonekana imeporwa mamlaka yake na kuhamishiwa Simba Sports Club Company, ambayo inatakiwa iundwe kwa wanachama kununua hisa ambazo ni asilimia 51 na hivyo kumiliki klabu hiyo kwa pamoja na wawekezaji.

Hata hivyo, katika hali halisi (de facto) ni kama Dewji ameushanunua asilimia 49 zote zinazotakiwa zimilikiww na wawekezaji zaidi ya wawili na katika moja ya mahojiano yako alishasema alishainunua klabu takriban miaka saba sasa (alisema miaka mitano).

ZENG 02

Kwa walivyojipangia, Dewji ndiye anatakiwa ateue mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, ambayo ndiyo inatakiwa iendeshe klabu. Pia anateua wajumbe wengine wa kuingia kwenye bodi hiyo, sambamba na wajumbe wengine kutoka upande wa klabu inayoongozwa na Mangungu.

Mangungu, ambaye ni mwenyekiti wa pili tangu Simba ianze kufuata utaratibu huo, anakuwa mjumbe wa kawaida kwenye bodi hiyo na hivyo masuala yote ya uendeshaji klabu yanakuwa chini ya bodi, ambayo kwa sasa inaongozwa na Crescentius Magori aliyeteuliwa na Dewji kushika nafasi hiyo baada ya Salim Try Again kuachia ngazi.

Katika hali ya kawaida, mwenyekiti wa klabu, ambayo inamiliki asilimia 51, ndiye angetakiwa kuwa na nguvu na mamlaka ya kuteua mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi. Na kwa mujibu wa taratibu za uendeshaji wa taasisi zenye muundo huo, mwenyekiti wa klabu na wawekezaji hawatakiwi kuwa sehemu ya bodi, bali kuteua wajumbe, huku wakiwekwa wakurugenzi wawili au watatu wasiotoka upande wowote kwa ajili ya kuhakikisha haki inalindwa kwa wote.

ZENG 03

Lakini ni kama Dewji na upande wake ndio walioshika klabu, na hasa timu ya mpira wa miguu. Hapo ndipo jambo linalosumbua linapokuja. Kama bodi ina mwenyekiti na ina mtendaji mkuu, inakuwaje mashabiki wamzonge Mangungu katika masuala yanayohusu shughuli za kila siku.

Kama mwenyekiti wa klabu anatakiwa ahudhurie kikao kupata taarifa za kinachoendelea na kuhoji pale anapoona pana tatizo au kuweka msimamo wa klabu kuhusu jambo hilo. Yaani anatakiwa asimame imara kutetea maslahi ya klabu na si kuwa sehemu ya mwekezaji au kuwa mtu anayekubali yaishe.

Naamini mashabiki na wanachama wa Simba hawamaanishi kile nachokielezea hapa, lakini hoja yao ndio iko huko. Kwamba, hadi sasa, mashabiki na wanachama hawajui nani wa kumwajibisha zaidi ya mwenyekiti waliyemchagua.

Huyo ndiye wana mamlaka naye na hao wengine wawajibishwe na upande uliowateua. Kwamba mageuzi ya umiliki na uendeshaji bado hayajakamilika kiasi kwamba waone uwajibikaji umehama kwa mwenyekiti waliyemchagua na umehamia kwa chombo kipya kinachoitwa Bodi ya Wakurugenzi.

Ndiyo maana ni kwa nadra sana, mwenyekiti wa bodi huwekwa kiti moto na mashabiki mitandaoni wakati mambo hayaendi sawa.

ZENG 04

Ni kwa jinsi hiyo, nimeanza kuwaelewa wanachama, mashabiki na wapenzi wa Simba wanapoelekeza shutuma zao kwa Mangungu kama mwenyekiti wao waliyemchagua ahakikishe klabu inaendeshwa kwa jinsi wanavyotaka.

Yaani Mangungu asikae kando akajitetea kuwa amehusikaje katika mwenendo mbovu wa timu au klabu, bali asimame imara kueleza yale anayoona si sawa na akemee na ikiwezekana ajitokeze kuwaeleza wanachama kilichotokea na hatua gani zimechukuliwa na upande wa klabu.

Mangungu asione ufahari kuzungumza hadharani kuhusu matatizo ya upande wa wapinzani wao kwa kuwa kazi hiyo anaifanya meneja habari na mawasiliano. Ajikite katika mambo muhimu ya klabu, kushughulikia kasoro za uendeshaji, usajili, umiliki na matumizi badala ya kugeuzwa mjumbe wa kawaida asiyeweza kuhoji chochote zaidi ya kuambiwa kilichotokea.

Wanachama hawataacha kuendelea kumsakama kwa kuwa wanajua mwenyekiti amewekwa pale kwa nguvu zao, kwa kura zao na ndiye pekee wanayeweza kumwajibisha na hivyo hana budi kusimama imara kuhakikisha masilahi ya klabu yanalindwa, kasoro zinaondolewa na pale inapobidi kuomba radhi kwa matokeo mabovu kwa kuwa ni kitendo cha uungwana na kinaonyesha uwajibikaji.