Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kubandika nywele kunaweza kugharimu afya yako

Muktasari:

  • Wakati mwanamke anabandika nywele ili kuongeza mvuto na mwanaume anafanya hivyo kubadilisha muonekano, mizizi ya nywele inaweza kuwa inalipa gharama ya urembo huo.

KAMA unadhani nywele ndefu, nzito na zilizobandikwa vizuri ndizo tiketi ya kuonekana umepangiliwa, ngoja kwanza! Huenda unachokiona kwenye kioo ni urembo, lakini kichwani kuna vita ambavyo huwezi kuviona kwa macho.

Wakati mwanamke anabandika nywele ili kuongeza mvuto na mwanaume anafanya hivyo kubadilisha muonekano, mizizi ya nywele inaweza kuwa inalipa gharama ya urembo huo.

Kubandika nywele, weaving, extensions na mitindo mingine inayovuta nywele inaweza kuleta mvutano wa muda mrefu kwenye ngozi ya kichwa. Wataalamu wa ngozi wanaonya kuwa mvutano huo ukijirudia mara kwa mara unaweza kusababisha tatizo linalojulikana kitabibu kama traction alopecia, aina ya upotevu wa nywele unaoweza kuwa wa kudumu endapo hautadhibitiwa mapema.


MZIZI UNAVUTWA KILA SIKU

Daktari wa ngozi Neelam Khan, pamoja na wataalamu wengine wanaeleza kuwa.”Mitindo inayovuta nywele kwa muda mrefu inaweza kuharibu afya ya vinyweleo.  Anaeleza kuwa extensions na weave, hasa zinapowekwa kwa kuvuta sana nywele, zinaweza kusababisha nywele kukatika au kuanguka na kuharibika baada ya kusukwa.”

Tatizo huanza pale nywele zinapowekwa katika mvutano mkali. Mtu anaweza kuanza kuona maumivu, kuwashwa, ukavu au hisia ya kuvutwa kwenye ngozi ya kichwa. Maumivu wakati wa kutengeneza nywele si jambo la kujivunia, bali ni ishara kwamba mtindo huo unaweza kuwa mkali sana.


ZICHOANZA KUPOTEA

Kwa wanawake wengi, eneo linaloathirika mapema ni sehemu ya mbele ya kichwa, maarufu kama edges. Hii ni kwa sababu nywele hizo huwa laini na dhaifu zaidi, hivyo kuvutwa mara kwa mara kunaweza kuzifanya zikatikakatika na hatimaye kupungua.

Daktari wa ngozi Crystal Aguh ambaye ni mtaalamu wa matatizo ya upotevu wa nywele, anasisitiza kuwa:”Umuhimu wa kutambua mapema aina ya tatizo la nywele na kutafuta matibabu sahihi.

Kwa mujibu wa wataalamu wa inaweza kuonekana zaidi katika maeneo yanayovutwa mara kwa mara na inaweza kuwa ya kudumu ikiwa mizizi itaharibiwa.


WANAWAKE WASIDHANI WANAUME WAMEACHWA

Tatizo hili si la wanawake pekee. Wanaume wanaotumia extensions, kusuka nywele kwa mtindo unaovuta sana au kuvaa mitindo inayoweka mvutano mkubwa kwenye mizizi nao wanaweza kupata madhara.

Mmoja wa madaktari wa ngozi anaeleza kuwa upotevu wa nywele unaweza kuwa na sababu nyingi na si kila tatizo la nywele linapaswa kulaumiwa kwa mtindo wa kutengeneza nywele. Hata hivyo, utunzaji sahihi wa nywele na utambuzi wa mapema ni muhimu ili kuzuia tatizo kuendelea.

HILI LINAWEZA KUWA TATIZO

Kubandika nywele mara nyingi huhusisha matumizi ya gundi, jambo ambalo linaweza kuongeza changamoto nyingineWataalamu  wanapendekeza tahadhari katika matumizi ya weave na extensions, ikisisitiza kuwa mitindo inayosababisha maumivu au kuwasha inapaswa kulegezwa au kuondolewa.

Wataalamu pia wanashauri mtu kuzingatia usafi wa nywele na ngozi ya kichwa wakati wa kutumia extensions. Nywele zinapaswa kusafishwa kulingana na mahitaji yake, huku bidhaa kali na matumizi ya kupita kiasi yakiepukwa


USIVALE KWA MUDA MREFU

Tatizo jingine ni kuvaa mtindo mmoja kwa muda mrefu bila kuipa nywele nafasi ya kupumzika. Wataalamu wanashauri kubadilisha mitindo na kupunguza muda wa kutumia weave au extensions inapendekeza mitindo hiyo itumike kwa muda mfupi na nywele zipewe mapumziko kabla ya kurudia.

Kwa mitindo ya nywele inayovuta, wataalamu pia wanashauri kulegeza sehemu za mbele, kutumia mistari mipana zaidi na kuepuka nywele kuwa nzito kupita kiasi kwa sababu uzito huongeza mvutano kwenye mizizi.


MAUMIVU SI SEHEMU YA UREMBO

Daktari wa ngozi mmoja amewahi kusisitiza kuwa;”Moja ya maswali muhimu kwa mtu anayesuka au kutengeneza nywele ni kama anaumia wakati wa kutengenezwa. Kwa mtazamo wa kitabibu, nywele hazipaswi kusababisha maumivu kwa sababu ya mtindo unaotengenezwa. Maumivu yanaweza kuwa ishara ya mvutano mkubwa unaoweza kuchangia kukatika nywele.”

UKIONA NYWELE ZINAPUNGUA, CHUKUA HATUA

Mtu akianza kuona nywele zikikatika, hairline ikirudi nyuma, maeneo fulani kuwa mepesi au ngozi ya kichwa kuwa na maumivu na kuwasha, si vizuri kuendelea na mtindo huo kwa kulazimisha.

Wataalamu wanashauri kuwa;”Ukuona mabadiliko baada ya kubandika harakisha kumuona daktari wa ngozi mapema kwa sababu chanzo cha kupotea kwa nywele kinaweza kuwa tofauti. Kwa baadhi ya watu, kuondoa mvutano mapema kunaweza kusaidia kuzuia madhara zaidi, lakini zikiharibika kwa muda mrefu, upotevu wa nywele unaweza kuwa wa kudumu.”