Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gofu Afrika yawapa darasa kina Madina

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye mashindano ya Gofu ya Ridhaa Afrika, yaliyomalizika Jumamosi iliyopita kwenye viwanja vya Leopard Creak, Afrika Kusini, wamekiri kujifunza vitu vingi vya kiufundi.

Mashindano hayo ya ridhaa yaliyofanyika kwa mara ya kwanza yalianza Februari 21 na kumalizika Februari 24, ikishikisha washiriki 72 wa kiume na wachezaji gofu wa kike 20 kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

Kwa upande wa Tanzania ikiwakilishwa na nyota wanne wakiwamo Madina Idd, Vicky Elias kwa upande wa wanaume na Isiaka Daudi na Ally Mcharo kwa wanaume ambao hata hivyo walishindwa kutamba, lakini wakiwa wametoka na somo kubwa kupitia mashindano hayo.

Madina na Vicky walichuana na wacheza gofu wengine wa nchi 19 zikiwamo  Afrika Kusini, Morocco, Kenya, Zimbabwe na Tanzania.
Kwa wanaume walikuwa ni Isiaka Daudi na Ally Mcharo, waliochuana na wenzao wengine 70 wa nchi mbalimbali na kutokana na idadi kuwa kubwa, raundi ya pili walipunguzwa 31 waliopata grosi nyingi akiwemo Mtanzania Mcharo aliyepata grosi 163 (84,79), hivyo wakawa wamebakia 41 kwenye kinyang’anyiro cha kusaka washindi.

Isiaka kwa upande wake alikamata nafasi ya 34
Nchi zilizoshiriki kwa upande wa wanaume ni Malawi, Zambia, Kenya, Afrika Kusini, Namibia, Zimbabwe, Morocco, Nigeria, Uganda, Misri, Tunisia, Madagascar, Rwanda, Senegali, Mauritius, Ghana, Eswatini, Shelisheli, Ghana, Ethiopia na Botswana.
Mzuka wa Gofu kupitia Gazeti la Mwanaspoti lilikuwa live kufuatilia michuano hiyo na likafanya mahojiano na wachezaji Watanzania, walikuwa na haya ya kusema.
Madina anasema viwanja vya Afrika Kusini, vipo kwenye ubora wa juu kuilinganisha na vilivyopo Tanzania na iliwabidi wapate muda wa kujifunza jinsi ya kupiga mipira.

“Changamoto ilikuwa joto na jua kali, jambo la pili  green zao ziko fasta ukilinganisha na green za Tanzania, tulichojifunza hadi  ni namna mpya ya kufanya putting kwenye green, inabidi tupunguze nguvu wakati wa kupiga putting kwenye green pia tumejifunza tukicheza mipira yetu tuwe tunaiweka fairway ili tuweze kupiga vizuri.”

Vicky anasema; “Kwanza tumeona ushindani ulivyokuwa mkubwa, vipo vitu ambavyo tutatakiwa kuvifanyia kazi, kwenye mashindano mbalimbali.”
Isihaka anasema Afrika Kusini ni kama Ulaya, kwani miundombinu yao ni mizuri na kuna vyuo vya gofu, jambo linalowasaidia wachezaji wa nchi hiyo kufanya vizuri kimataifa.

“Afrika Kusini ni kama Ulaya, tofauti na kwetu kwa maana ya Viwanja vyao vina standadi ya juu, pamoja na hayo yote tumejifunza vitu vingi ambavyo tutavifanyia kazi, naamini kuna siku moja tutachukua mataji ya dunia,” anasema Isihaka.
Mcharo anasema; “Ingawa nilitoka raundi ya pili, haikunizuia kujifunza, kwanza tumekutana mataifa tofauti, wenye viwango tofauti, hivyo kwa vyovyote hapawezi kukosekana elimu hapo.”


MATOKEO YAO
Mashindano hayo upande wanawake yalifanyika kwa muda wa siku tatu, na kwa upande wanaume yalifanyika kwa siku nne na hapo chini ni matokeo ya wawakilishi hao wa Tanzania.
Madina Iddy siku 3 nafasi ya 13 grosi 247 (79,83,85), Vicky Elias siku 3 nafasi ya 16 grosi  254 (81,83, 90)
Isiaka Daudi siku 4 nafasi 34 grosi 314 (78, 79, 78,79) na Ally Mcharo siku 2 grosi 163 (84,79) alishindwa kufuzu akayaaga mashindano.

Kombe limebaki kwa wenyeji Afrika Kusini kwa wanaume na wanawake na bingwa kwa upande wa wanawake kuanzia mshindi wa kwanza hadi wa tatu wote walikuwa na Wasauzi.
Kyra Van Kan aliyemaliza kwa grosi 215 (72,71,72), akifuatiwa na Bobbi Brown aliyepata grosi 224 (75, 78, 71) huku Gia Road akivuna 225 (79,70,76) wakati upande wa wanaume nafasi zote tatu za juu zilinyakuliwa na Wasauzi pia.

Altin Van der Merwe aliibuka kidedea kwa kupata grosi 275 (69,65,71,70), huku Christian Maas na Ivan Verster kila mmoja akipata pia grosi 275, lakini Maas akipiga 71, 69, 63 na 72 wakati mwenzake alipiga 66, 69, 67 na 73.

Imeandaliwa na Olipa Assa, Brown Msyani na Nevumba Abubakar