Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ghana iko tayari kwa vita Kombe la Dunia U-20

GHANA Pict

Muktasari:

  • Ghana imefuzu kwa mara ya nane mfululizo kwenye Kombe la Dunia la U-20 la Wanawake, ikiwa moja ya timu nne za Afrika zilizopata tiketi ya Poland 2026. FIFA imethibitisha kuwa Black Princesses wamekuwa wakifika kwenye fainali za dunia tangu mwaka 2010, lakini katika mashindano yao saba yaliyopita hawajawahi kuvuka hatua ya makundi,Hapo ndipo ukubwa wa changamoto yao ulipo.

GHANA haendi Poland kama mgeni, wala haendi kwa ajili ya kujifunza mazingira ya Kombe la Dunia la Wanawake U-20. Badala yake, Black Princesses wanaingia kwenye mashindano hayo wakiwa na uzoefu wa kutosha wa jukwaa la dunia, lakini safari yao ya Poland 2026 imebeba swali moja kubwa; je, safari hii wanaweza kuvuka hatua ya makundi na kuandika historia mpya?

Ghana imefuzu kwa mara ya nane mfululizo kwenye Kombe la Dunia la U-20 la Wanawake, ikiwa moja ya timu nne za Afrika zilizopata tiketi ya Poland 2026. FIFA imethibitisha kuwa Black Princesses wamekuwa wakifika kwenye fainali za dunia tangu mwaka 2010, lakini katika mashindano yao saba yaliyopita hawajawahi kuvuka hatua ya makundi,Hapo ndipo ukubwa wa changamoto yao ulipo.

Ghana ilianza kuonekana kwenye fainali za Kombe la Dunia la U-20 la Wanawake mwaka 2010. Tangu wakati huo, imekuwa ikirudi kwenye mashindano hayo kwa ukawaida, ikishiriki mwaka 2012, 2014, 2016, 2018, 2022 na 2024.

Lakini pamoja na uwepo huo wa muda mrefu, Black Princesses bado wana kazi kubwa ya kufanya ili kubadilisha historia yao. Kwenye kila mechi zao za awali za dunia, wameishia katika hatua ya makundi. Hiyo ina maana kwamba timu hii ina uzoefu mkubwa wa mashindano, lakini bado haijapata mafanikio ya kufika hatua ya mtoano. Kwa hiyo Poland si safari nyingine tu ni nafasi ya Ghana kuvunja ukuta ambao umekuwa mbele yao kwa miaka mingi.

GHAN 01

Safari ya Ghana kuelekea Poland haikuwa nyepesi, Katika hatua za kufuzu za Afrika, Black Princesses walikutana na wapinzani tofauti kabla ya kufikia raundi ya mwisho. Miongoni mwa mitihani mikubwa ilikuwa dhidi ya Afrika Kusini, ambapo Ghana ilipita kwa ushindi wa jumla wa 3-2 na kufuzu hatua ya mwisho.

Ghana ilishinda mchezo wa kwanza kwa mabao 2-1 na hivyo kwenda kwenye mchezo wa marudiano ikiwa na faida ndogo. Uganda ilipata bao la mapema katika mchezo wa pili mjini Kampala, lakini Black Princesses walipambana hadi mwisho na kusawazisha, matokeo yaliyowatosha kufuzu kwa jumla ya 3-2.

Kilichovutia zaidi ni kwamba Ghana ilifanya hivyo ikiwa imebaki na wachezaji 10 baada ya Margaret Yeboah kutolewa kwa kadi nyekundu. Hapo ndipo moja ya sifa kubwa za kikosi hiki ilipoonekana uwezo wa kupambana katika mazingira magumu.

Kama kuna kitu Ghana imeonyesha katika safari yake ya kufuzu ni uwezo wa kutokata tamaa.Mchezo dhidi ya Uganda ni mfano wa wazi Walikuwa nyuma kwenye ubao wa matokeo, wakacheza sehemu ya mchezo wakiwa pungufu, lakini bado wakapata matokeo yaliyowapeleka Poland.Hiyo inaweza kuwa silaha muhimu kwenye Kombe la Dunia.

GHAN 02

Mashindano ya U-20 mara nyingi huamua mambo kwa tofauti ndogo,Timu inayoweza kubaki imara baada ya kufungwa bao au kukutana na changamoto inaweza kuwa na nafasi kubwa ya kuendelea.

Pia Ghana ina uzoefu wa kutosha wa mashindano ya kimataifa, wachezaji wake wanaingia Poland wakijua uzito wa kuvaa jezi ya Black Princesses kwenye jukwaa kubwa.

Black Princesses wamefika Kombe la Dunia mara saba kabla ya Poland, lakini hawajawahi kuvuka hatua ya makundi. Hilo linaweza kuwa pengo lao kubwa zaidi wanapokutana na timu ambazo tayari zimezoea kucheza mechi za hatua ya pili.

Mbele ya kazi hiyo yupo kocha Charles Sampson, ambaye anaiongoza Black Princesses kwenye kampeni hii.

GHAN 03

Sampson amekuwa akisimamia maandalizi ya Ghana kuelekea mashindano hayo, huku timu ikianza maandalizi mapema na baadaye kuhamia Poland kwa kambi ya mwisho. Ghana Football Association ilithibitisha kuwa kikosi kilikuwa kambini tangu Julai 5 kabla ya kuondoka kuelekea Poland Agosti 16.


GHANA KATIKA MITIHANI MITATU

Poland 2026, imeiweka Ghana katika Kundi C, pamoja na France, Korea Republic na Ecuador.

France ni timu yenye historia na mfumo mzuri wa soka la vijana, Korea Republic ni mpinzani ambaye Ghana italazimika kumheshimu, wakati Ecuador nayo itataka kutumia nafasi yake kwenye jukwaa la dunia.

Ghana itaanza kampeni yake dhidi ya Ecuador Septemba 6, kabla ya kukutana na Korea Republic na baadaye France.Kwa hiyo, mwanzo mzuri utakuwa muhimu.

Miongoni mwa majina yaliyojitokeza kwenye safari ya kufuzu ni Linda Owusu Ansah, aliyefunga bao muhimu lililosaidia Ghana kupata tiketi ya Poland.

GHAN 04

FIFA imeangazia mchango wake na namna bao hilo lilivyokuwa muhimu katika kuhakikisha Black Princesses wanafuzu baada ya mtanange mkali dhidi ya Uganda.Hivyo, macho yatakuwa kwake pia Ghana itakapoanza kampeni yake Poland.

Black Princesses tayari wana uzoefu, Wana historia ya kufuzu, Wana mechi nyingi za kimataifa, Wana kocha anayejua umuhimu wa maandalizi.

Kinachokosekana ni hatua moja kubwa kuvuka makundi,Kama wataweza kutumia nguvu yao ya kupambana, kuwa na nidhamu wanapokuwa hawana mpira na kutumia nafasi wanazopata, Ghana inaweza kujikuta ikiingia kwenye historia mpya. Poland 2026 ni mara yao ya nane,Mara saba zilizopita ziliishia kwenye makundi,Safari hii, Black Princesses hawataki kurudi nyumbani mapema. Wanataka kuvuka ukuta.

Na kama walivyofanya dhidi ya Uganda, Ghana imeonyesha tayari kwamba hata ikiwa mambo yatakuwa magumu, hawajui maana ya kukata