Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DJ Khaled anazidi kuukunja tu mkwanja

ATM Pict

Muktasari:

  • Bidhaa hiyo ambayon imeanza kuuzwa Marekani inaatarajiwa kumpa utajiri maradufu Khaled ambaye kwa sasa ni miongoni mwa watu maarufu wanaopata pesa nyingi katika kiwanda cha muziki Marekani.

MIAMI, MAREKANI: WIKI iliyopita, msanii H Khaled Mohammed Khaled ‘DJ Khaled’ aliachia biadhaa yake ya shampoo ambayo ina uwezo wa kubadilisha nywele rangi kwa watumiaji.

Bidhaa hiyo ambayon imeanza kuuzwa Marekani inaatarajiwa kumpa utajiri maradufu Khaled ambaye kwa sasa ni miongoni mwa watu maarufu wanaopata pesa nyingi katika kiwanda cha muziki Marekani.

Hapa tumekuletea utajiri kamili wa nyota huyu na kiasi cha pesa anachoingiza kutokana na muziki na madili mbalimbali.


AT 04

ANAPIGAJE PESA

Kijumla anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Dola 95 milioni. Alianza safari ya utajiri wake kwakutengeneza ngoma za wasanii mbalimbali wakubwa Marekani kama Jay-Z, Lil Wayne, na Kanye West.

Mbali ya kutengeneza nyimbo za watu, Khaled pia anaimba na ameshaachia  albamu kadhaa zilizompa pesa za kutosha.

Albamu ya kwanza  iliyouza vizuri ilikuwa ni ile ya ‘Major Key’ iliyotoka mwaka 2016 ambayo ndani ya marekani tu, ilinunuliwa mara milioni tatu.

Kijumla inatajwa ilimpa kiasi kisichopungua Dola 20 milioni kutokana na mauzo yake.

Khaled huyu pia amekuwa akipewa kazi ya kuwa DJ kwenye matamasha mbali mbali duniani ambako amekuwa akikunja zaidi ya Dola 1 milioni kwenye kila shoo.

AT 05

Pia ana kipindi chake binafsi kiitwacho The Khaled Khaled Show ambacho kinaruka kupitia App ya  Apple Music.

Kijumla kwa mwaka inadaiwa kukunja Dola 10 milioni kutokana na kipindi chake na U Dj.

Anapata kiasi kisichopungua Dola 30 milioni kutokana na mikataba ya udhamini na biashara zake binafsi.

Khaled kwa sasa ana ubalozi wa kampuni za Apple, Ciroc na Weight Watchers, pia anamiliki kampuni yake ya mavazi iitwayo ‘We the Best’.€

Amewahi pia kuandika vitabu viwili ‘The Keys’€  na ‘The Gift’€ambavyo vimempatia zaidi ya Dola 7 milioni kwenye mauzo.

Kutokana na mitandao yake ya kijamii huwa anatumia kutangaza muziki na biashara zake kwa jumla na kwa mujibu wa taarifa, anakunja Dola 2 milioni kwa mwaka kutokana na akaunti yake ya Instagram.

AT 02

MJENGO

Januari, 2017, alinunua  nyumba  ya zamani ya Robbie Williams iliyopo huko Mulholland Estates, Los Angeles kwa Dola 9.9 milioni na akaiuza Aprili, 2021 kwa 12.5 milioni, ikiwa ameingiza faida ya Dola 1.5 milioni.

Mwaka 2018, alinunua mjengo wa kifahari uliopo kwenye fukwe ya bahari huko  Miami kwa Dola 25.9 milioni.

AT 03

MAISHA NA BATA

Kwa sasa yupo kwenye ndoa na  Nicole Tuck ambaye alifunga naye pingu hizo za maisha mwaka 2017 baada ya kumchumbia mwaka 2016.

Wawili hao wamebahatika kupata watoto wawili pamoja ambao wote ni wakiume  Asahd na Aalam.