Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Philippe Coutinho pesa sio shida zake

ATM Pict

Muktasari:

  • Kwa sasa yupo huru na hajaonyesha kiwango chake bora kwa muda sasa, lakini bado ameendelea kuwa miongoni mwa wachezaji wenye pesa.

RIO DE JANEIRO, BRAZIL: WIKI iliyopita kiungo mshambuliaji wa Brazil, Philippe Coutinho, alitamba katika vichwa vya habari baada ya kuvunja mkataba wake na klabu ya Vasco da Gama ya Brazil kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutoona upendo kutoka kwa mashabiki ambao mara kadhaa wamekuwa wakimzomea.

Kwa sasa yupo huru na hajaonyesha kiwango chake bora kwa muda sasa, lakini bado ameendelea kuwa miongoni mwa wachezaji wenye pesa.

Leo tumekusogezea undani wa utajiri wake na jinsi anavyopiga pesa.

AT 03

ANAPIGAJE PESA?

Utajiri wa Philippe Coutinho unakadiriwa kufikia zaidi ya Dola 60 milioni ambao kwa asilimia kubwa umetokana na mshahara na baadhi ya vyanzo vyake vya mapato.

Coutinho alikuwa akipokea mshahara mnono wa Pauni 470,000 kwa wiki akiwa na Barcelona, kiasi ambacho kilimfanya atajirike zaidi kwa wakati huo.

Akiwa na Vasco da Gama alikuwa akilipwa takribani Pauni 135,000 kwa wiki ambayo pia ilikuwa ikifikia Pauni 150,000 kwa wiki kwa mjumuisho wa bonasi.

Mbali ya mshahara Coutinho amekuwa na mikataba ya udhamini na kampuni kubwa za vifaa vya michezo

Nike ambayo kwa mwaka inakadiriwa kumlipa Dola 2 milioni.

Vilevile jamaa ni balozi wa kampuni ya Pro Evolution Soccer na ana ubalozi wa kampuni kadhaa za vinywaji na chakula kutoka Brazil.

Kwa ujumla, kupitia udhamini na matangazo, Coutinho hupata takribani Dola 2 hadi 3 milioni kwa mwaka.

AT 02

MIJENGO

Anadaiwa kuwekeza sana katika mijengo ambapo mbali ya nyumba za kuishi mwenyewe pia ana nyumba ambazo amekuwa akizitumia kufanya biashara.

Ana jumba la kifahari jijini Barcelona lenye thamani ya takribani Dola 6 milioni, alilolinunua kipindi akiwa bado anachezea klabu hiyo.

Pia anamiliki nyumba Brazil, katika Jiji la Rio de Janeiro, ambalo ndio amekuwa akilitumia kwa ajili ya mapumziko ya familia yake. Mjengo huo una thamani ya Dola 4 milioni.

Nyumba zake zina gym binafsi, bwawa la kuogelea maeneo ya kupumzika kwa ajili ya familia.

AT 04

NDINGA ZAKE

Porsche Panamera – Dola 150,000

Audi RS7 – Dola 120,000

Mercedes-Benz G-Wagon – Dola 150,000

Range Rover Sport – Dola 110,000

AT 01

MSAADA KWA JAMII

Coutinho amekuwa akirejesha sana kwa jamii, hasa nchini kwao Brazil. Ni mdau mkubwa wa kutoa misaada wa vituo vya watoto yatima na shule za soka kwa vijana.

Huchangia misaada ya afya na elimu kwa watoto kutoka familia zisizo na uwezo.

Mara kadhaa ametoa misaada kimya kimya bila kutangaza.

AT 05

FAMILIA NA MAISHA BINAFSI

Jamaa yupo kwenye ndoa na mke wake aitwaye Aine Coutinho na wamejaliwa kupata watoto watatu, ambapo wawili ni wa kike -- Maria na Esmeralda pamoja na mmoja wa kiume aitwaye Jose.

Coutinho anajulikana kama mtu mtulivu, anayependa familia na maisha ya faragha mbali na kelele za soka la kisasa.

Licha ya kupanda na kushuka kwa kiwango chake uwanjani, Coutinho tayari ameshajihakikishia maisha mazuri nje ya soka. Kwa kifupi, kwa nyota huyu wa Brazil, pesa sio shida zake, bali changamoto kubwa imekuwa ni kurejea katika kiwango chake akiwa na umri wa miaka 33 sasa.