Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cheki Lamar anavyokimbiza mfukoni na jukwaani

ZENG 07

Muktasari:

  • Mbali ya mafanikio ambayo ameyapata katika muziki na tuzo, Lamar pia amefanikiwa sana kiuchumi akiwa miongoni mwa wasanii wenye pesa za kutosha duniani.

CALIFORNIA – MAREKANI: WIKI chache zilizopita, rapa wa Marekani, Kendrick Lamar, alirudi kwenye vichwa vya habari baada ya kushinda tuzo za Grammy na kuweka rekodi ya kuwa rapa aliyefanya hivyo mara nyingi zaidi (27).

Mbali ya mafanikio ambayo ameyapata katika muziki na tuzo, Lamar pia amefanikiwa sana kiuchumi akiwa miongoni mwa wasanii wenye pesa za kutosha duniani.

Leo tumekusogezea undani wa utajiri wa mkali huyu na jinsi anavyopiga pesa kupitia muziki wake na miradi mbalimbali.

AT 03 (1)

ANAPIGAJE PESA

Kwa sasa ana utajiri unaokadiriwa kufikia Dola 200 milioni ambao kwa asilimia kubwa umetokana na muziki pamoja na madili mengine.

Kwanza kabisa jamaa amepata pesa nyingi kupitia ngoma zake zilizofanikiwa kimataifa kama good kid, m.A.A.d city, To Pimp a Butterfly, DAMN. na Mr. Morale & the Big Steppers kila moja zimempa zaidi ya Dola 20 milioni.

Anaingiza pia mkwanja wa kutosha kupitia matamasha na ziara zake za kimataifa ambapo shoo moja kubwa humwingizia hadi Dola 15 milioni.

Jamaa ana kampuni yake iitwayo pgLang inayojihusisha na utengenezaji wa muziki, filamu, mitindo na sanaa kwa ujumla.

Kupitia kampuni hiyo, Lamar alishiriki kama mmoja kati ya watayarishaji wa muziki wa filamu ya Black Panther, kazi ambayo iliingiza takribani Dola 20 milioni.

Kwa sasa Lamar ni balozi wa kampuni ya Nike na American Express, lakini pia awali aliwahi kushiriki katika matangazo ya kampuni kadhaa ikiwamo  Calvin Klein, Converse, na Cash App.

Mwaka 2018, jarida la Forbes lilimtaja kama mmoja wa wasanii wanaolipwa zaidi duniani.

AT 01

MIJENGO

Kendrick anamiliki nyumba kadhaa za kifahari, likiwamo, jumba kubwa lililopo Compton, California lenye thamani ya Dola 9 milioni, likiwa na studio binafsi ya muziki, Gym ya kufanyia mazoezi na bustani ya kisasa.

Nyumba nyingine ipo maeneo ya Manhattan Beach na ina thamani ya Dola 6 milioni, ambayo mara nyingi amekuwa akiitumia kupumzika.

AT 02

NDINGA

Kendrick huwa hapendi sana kuonyesha mali zake lakini hadi sasa ameonekana akiwa anaendesha magari kadhaa ya kifahari ambayo ni pamoja na,

Rolls-Royce Phantom – Dola 450,000

Range Rover – Dola 120,000

Lexus SUV – Dola 90,000

Buick GNX – Dola 300,000

AT 03

MSAADA KWA JAMII

Lamar amekuwa akitoa sana misaada katika taasisi na watu wasiojiweza kwenye mji wake alikozaliwa Compton.

Kupitia kampuni yake pgLang na baadhi ya kampuni washirika huwa anatoa zaidi ya Dola 2 milioni kwa mwaka kama sehemu ya msaada.


FAMILIA NA MAISHA BINAFSI

Kendrick yupo kwenye uhusiano wa muda mrefu na mchumba wake Whitney Alford, na wamejaliwa watoto wawili ambao wa kwanza ni wa kike aitwaye Uzi aliyezaliwa mwaka 2019 na wa pili anaitwa Enoch aliyezaliwa mwaka 2022.