Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili za mastaa zilizovunjika dakika za mwisho kimaajabu

DILI Pict

Muktasari:

  • Man United imeshuhudia ofa zao mbili zikikataliwa, ikiwamo ya Pauni 65 milioni kwa ajili ya mchezaji huyo na ripoti za hivi karibuni zinadai miamba hiyo ya Old Trafford, imeandaa ofa ya tatu ya Pauni 70 milioni.

LONDON, ENGLAND: MANCHESTER United imegoma kuingia kwenye mtego wa Brentford wa kupandisha bei ya mchezaji Bryan Mbeumo kila wanapokaribia kufikia makubaliano, jambo linaloibua wasiwasi wa dili hilo kuvunjika.

Man United imeshuhudia ofa zao mbili zikikataliwa, ikiwamo ya Pauni 65 milioni kwa ajili ya mchezaji huyo na ripoti za hivi karibuni zinadai miamba hiyo ya Old Trafford, imeandaa ofa ya tatu ya Pauni 70 milioni.

Mwishoni wa mwezi uliopita, mkurugenzi wa soka wa Man United, Jason Wilcox, anaamini Pauni 65 milioni ni pesa inayotosha kabisa kukamilisha dili la Mbeumo. Kama dili hilo la Mbeumo kwenda Man United likikwama, basi haitakuwa mara ya kwanza kwa uhamisho wa mchezaji kukwama kutokana na sababu zisizokuwa na maana.

Siku chache zilizopita, kuliripotiwa kuwapo kwa wasiwasi wa dili la straika Viktor Gyokeres la kwenda Arsenal kuvunjika, wakati likiwa kwenye hatua za mwisho kabisa kukamilika. Dili hilo bado lipo baada ya kuelezwa Arsenal imeshafikia makubaliano na Sporting Lisbon.

Hizi hapa dili za uhamisho wa wanasoka zilizokwama dakika za mwisho kutokana na sababu za kushangaza kabisa.

DIL 01

Nabil Fekir (Lyon – Liverpool)

Kufeli vipimo vya afya si kitu cha kushangaza kwenye soka la kisasa, lakini mazingira yaliyovunja dili la kiungo Nabil Fekir kwenda Liverpool mwaka 2018 linastua. Alikuwa kwenye hatua za mwisho kutua Liverpool, alipiga hadi picha akiwa na jezi za miamba hiyo ya Anfield. Lakini, dili hilo lilivunjika baada ya madaktari wa Liverpool kugundua historia ya majeraha ya goti ambayo yamekuwa yakimsumbua mchezaji huyo. Kwa sababu hiyo, Liverpool ikafuta dili hilo.

DIL 02

John Obi Mikel (Lyn Oslo – Man United)

Mwaka 2005, Manchester United ilitangaza usajili wa kiungo John Obi Mikel kutoka Lyn Oslo, lakini katika maelezo ya kushangaza, staa huyo wa Nigeria alidai kwamba alipigwa presha kujiunga na Mashetani Wekundu. Jambo hilo likafanya kuwapo kwa utata mkubwa, licha ya Mikel kwenda hadi Man United na kufanya mazoezi na wakali Roy Keane, Paul Scholes na Nicky Butt na kusaini mkataba wa awali. Lakini, Mikel alichagua kujiunga Chelsea na dili la Man United likafa.

DIL 03

Emmanuel Adebayor (Tottenham – Aston Villa)

Emmanuel Adebayor alikaribia kabisa kujiunga na Aston Villa kwa mkopo akitokea Tottenham Hotspur mwaka 2015, lakini dili hilo lilivunjika. Straika huyo wa Togo alifunga mabao 97 kwenye Ligi Kuu England alifanya vipimo vya afya na kupiga picha za dili hilo la kwenda Villa Park. Lakini, ghafla tu Adebayor alijitoa kwenye dili hilo akidai hakuwa amejiandaa kiakili kwa uhamisho huo baada ya kupewa ushauri wa mchungaji wake. Adebayor alidai alitaka ishara ya Mungu.

DIL 04

Roy Keane (Nottingham Forest – Blackburn)

Kabla ya kwenda kuwa gwiji wa Manchester United, Roy Keane alisaini mkataba wa awali na klabu ya Blackburn Rovers mwaka 1993, na alijiandaa kujiunga na timu hiyo, lakini dili likavunjika. Kocha wa Blackburn wa kipindi hicho, Kenny Dalglish alishindwa kukamilisha dili la kumnasa Keane baada ya kutokea makosa kwenye mashine ya faksi, hivyo dili likakwama na Keane akabaki Nottingham Forest. Baadaye Man United iliingia na kufanikiwa kunasa saini ya Keane.

DIL 05

David De Gea (Man United - Real Madrid)

Kila mtu anajua hii stori ya David De Gea kukwama uhamisho wake wa kwenda Real Madrid mwaka 2015. Kipa huyo Mhispaniola aliachana na Manchester United mwaka 2023 wakati mkataba wake ulipofika tamati na miamba hiyo ya Ligi Kuu England, lakini miaka minane nyuma alikaribia kabisa kujiunga na Real Madrid. Dili la De Gea lilikwama baada ya karatasi ya mwisho ya kuthibitisha usajili kuwasilishwa dakika 28 baada ya dirisha la usajili Hispania kufungwa kwa kosa la faksi.

DIL 06

Fabio Borini (Liverpool – Sunderland)

Straika wa Liverpool, Fabio Borini alikuwa kwenye hatua za mwisho kabisa za kukamilisha uhamisho wa jumla wa kutua Sunderland mwaka 2014, baada ya kucheza kwa mkopo kwenye timu hiyo, lakini dili lilivunjika. Kilichoripotiwa ni kwamba sababu iliyosababisha dili hilo kufutika ni Borini kubadili mawazo na kugoma kuondoka Liverpool, akisisitiza kwamba atabaki ili kupigania nafasi kikosini. Mmoja wa washambuliaji wa Liverpool kwa wakati huo alikuwa Fernando Torres.

DIL 07

Loic Remy (QPR – Liverpool)

Dili jingine la kuhamia Liverpool ambalo lilikwama ni la Loic Remy, ambaye alikaribia kabisa kujiunga na miamba hiyo ya Anfield akitokea QPR mwaka 2014, ambapo alikuwa akitazamwa kama mbadala wa Luis Suarez, lakini dili hilo lilivunjika. Kama ilivyokuwa kwa Fekir, madaktari wa Liverpool waligundua mchezaji huyo ana tatizo na kuwashauri viongozi wa klabu kusitisha dili hilo. Lakini, baada ya hapo, Remy alikwenda kujiunga na Chelsea na kucheza mechi kibao huko.

DIL 08

Ronaldinho (PSG – Man United)

Kabla ya kujiunga na Barcelona, Ronaldinho alikaribia kabisa kujiunga na Manchester United akitokea PSG mwaka 2003. Ripoti zinafichua kwamba Man United ilikaribia kabisa kunasa saini ya Mbrazili huyo, ambapo ilikuwa ikimtazama kama mtu mwafaka wa kwenda kuchukua mikoba ya David Beckham, ambaye alitimkia Real Madrid. Lakini, dili hilo lilivunjika kwa sababu Mbrazili huyo aliona si vyema kwenda kucheza soka Manchester kwa sababu kuna mvua nyingi sana.

DIL 09

Robert Lewandowski (Lech Poznan – Blackburn)

Straika, Robert Lewandowski alikuwa mmoja wa mastaa matata na wamaliziaji hodari kabisa duniani, akitamba kwenye klabu kadhaa ikiwamo Bayern Munich na Barcelona. Lakini, kabla ya hapo, staa huyo wa Poland alikaribia kujiunga na Blackburn Rovers wakati huo akiwa anakipiga Lech Poznan. Lakini, mlipuko wa volcano huko Eyjafjallajokull ulisababisha kukwama kwa usafiri wa anga na kukosekana kwa ndege za kwenda England na kufanya dili kushindikana.

DIL 10

Zlatan Ibrahimovic (Malmo – Arsenal)

Zlatan Ibrahimovic alikaribia kabisa kujiunga na Arsenal mwaka 2000. Kocha wa Arsenal wa kipindi hicho, Arsene Wenger, alihitaji saini ya staa huyo wa kimataifa wa Sweden, lakini dili lilikwama kwa sababu kocha huyo Mfaransa alihitaji mshambuliaji huyo afanye majaribio na staa huyo alisema, "Zlatan hafanyi majaribio ", na kugomea ofa ya kujiunga na miamba hiyo ya Emirates. Baada ya dili hilo kukwama, Zlatan alikwenda kujiunga na Ajax na kuwa mmoja wa staa matata.

DIL 11

Neymar (Santos – Man City)

Kama ilivyo kwa Mbrazili mwenzake, Ronaldinho, Neymar inaaminika kwamba aligomea kujiunga na klabu nyingine ya jiji la Manchester kutokana na hali ya hewa. Safari hii ilikuwa Manchester City ambao walikuwa na mpango wa kumsajili Neymar wakati huo akiwa Santos mwaka 2013, lakini dili hilo lilishindwa kukamilika. Neymar aligomea kwenda kucheza soka Man City kutokana na hali ya hewa kuwa mvua nyingi na mchezaji atahitaji kuwa na viatu maalumu kucheza huko.