Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Asiyefunzwa na Hispania, Rodri, atafunzwa na ulimwengu

PAZIA Pict


NANI bingwa wa Ligi ya Mabingwa ya Ulaya? PSG. Arsenal waliutafuta mpira kwa tochi pale Budapest. Kocha wa PSG ni Luis Enrique Martinez. Mhispaniola. Sasa sikia. Kocha wa Arsenal alikuwa nani? Mikel Arteta. Mhispaniola.


Lakini ligi ya mabingwa ilikuwa ni kituo cha mwisho kwa Martinez. Kabla ya hapo alikuwa ameshachukua ubingwa wa Ufaransa. Unaweza kuudharau kwa sababu PSG wana misuli. Lakini vipi kuhusu ubingwa wa Ulaya?


Arsenal walichukua ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya miaka 22. Kocha nani? Mikel Arteta Mhispaniola. Kama wangeleta ujinga nusura Manchester City wangechukua tena ubingwa. Kocha wa Manchester City alikuwa nani? Pep Guardiola. Mhispaniola.

Huyo huyo ambaye alikuwa anamfukuza Arteta katika mbio za ubingwa alikuwa na jambo lake pembeni. Alikuwa na michuano ya FA ambayo alikwenda kuichukua na baadae akakosa ubingwa kwa Arteta na mwishowe akaamua kwenda zake kupumzika.

PAZ 02

Bingwa wa michuano ya Europa? Aston Villa. Kocha nani? Unai Emery. Mhispaniola. Lilikuwa kombe lao la kwanza kubwa Ulaya baada ya miaka 44. Umri wa mtu mzima. Wahispaniola wametukaba kooni.

Ina maana pambano la ufunguzi wa Ligi Kuu England kama Pep asingeondoka England lingekuwa kati ya Wahispaniola wawili. Pep na Arteta. Bingwa wa Ligi na bingwa wa kombe la FA.

Kama ambavyo pambano la ufunguzi wa michuano ya Ulaya litakuwa kati ya Wahispaniola wawili. Unai na Martinez. Watakutana kupimana ubavu kuhusu nani zaidi kati yao. Washipaniola wametutawala katika dunia ya leo.

Kuna wengine pia. Xabi Alonso ameenda zake Chelsea. Real Madrid walimchelewesha pale La Liga lakini kabla ya hapo alikuwa amewapa  ubingwa wa Bundesliga Bayer Liverkusen. Kabla ya Bayer Leverkusen kutwaa ubingwa huo kumbuka Bayern Munich alikuwa ametwaa mara 11 mfululizo.

PAZ 01

Halafu kule Como Italia kuna Cesc Fabregas. Muhispaniola mwingine huyo. Alipewa timu ndogo tu ya Como lakini ameipeleka katika ligi ya mabingwa kwa mara ya kwanza tangu ianzishwe mwaka 1907. Huu ni wakati wa Wahispaniola.

Mpira wao unatamba. Hauwezi kubishana na mpira wao. Haikunishangaza sana wakati Luis de la Fuente alipoendelea kufanya kile kile ambacho makocha wa Hispaniola wanakifanya katika ligi mbalimbali.

Pale New Jersey kando kidogo ya New York, De la Fuente hakufanya maajabu mapya. Aliendelea kumalizia kazi ambayo makocha wa kihispaniola wameifanya katika msimu uliopita na wamekuwa wakifanya katika miaka ya karibuni.

PAZ 03

Waargentina walikuwa uwanjani na mpira na mpira walikuwa hawauoni. Cristiano Ronaldo alishutumiwa sana kwa kutemba katika mechi nyingi za kombe la dunia mwaka huu, lakini kumbe rafiki yake Lionel Messi alikuwa anasubiri kutembea katika pambano la fainali.

Haikushangaza sana. Hakuna timu ilitutisha kama Ufaransa. Namna ambavyo walikuwa wanafunga mabao kama vile wanakaanga mayai. Kylian Mbappe, Ousmane Dembele na Michael Oliseh. Hata hivyo walikuja kufundishwa adabu na Wahispaniola.

Baada ya kutazamana tu pambano lile dhidi ya Ufaransa asilimia tisini ya viumbe hai duniani walijua kombe la dunia lilikuwa limeishia pale. Kama fainali yenyewe ambayo ilikuwa usoni ilikuwa dhidi ya Argentina basi ni wazi bingwa angekuwa Mhispaniola.

PAZ 04

Walau kidogo angeenda Muingereza. Tatizo kubwa la vijana wa Mfalme Charles ni kocha wao, Thoma Tuchel hakuwa na akili nzuri ya mpira. Alipopata bao lake la Anthony Gordon katika pambano la nusu fainali dhidi ya Lionel Messi akaamua kukaa nyuma kulinda bao.

Mpira wa Hispania haushikiki siku hizi. Kuna wakati utapoteza ladha na labda kuna watu wengine watakuja na mpira mwingine. Huu wa Hispania wa akina Pep na wenzake unatusumbua sana. Unamfanya adui akimbie bila ya mpira wakati wao Wahispaniola ndio wana mpira.

Wafaransa walikimbia bila ya mpira na wahispaniola walitembea na mpira wao. Rodri alipiga pasi 756 akiongoza kwa kupiga pasi katika michuano hii. Katika timu yake bado Pau Cubarsi akapiga pasi 698. Aymeric Laporte akapiga pasi 659. Wote hawa wanatoka timu timu.

Wahispaniola wametufundisha kucheza mpira rahisi. Walishawahi kutufundisha katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 walipotwaa taji pale Soweto. Hapa katikati sijui walipata kichaa gani wakatoweka.

PAZ 05

Labda hawakuweza kutuletea wachezaji wa aina ya Xavi Hernandez au Andres Iniesta. Labda wamewapata tena sasa hivi. Inasemwa Barcelona ndio inailisha vema timu ya taifa ya Hispania pale wanapokuwa vizuri. Ni kama wakati ule au wakati huu. Mpira wao katika miaka ya karibuni daima unajulikana.

Na zaidi ni kwamba lazima wawe na kiungo mmoja ambaye ni msingi wa kila kitu. Msingi wa zile pasi ambazo Tanzania waliwahi kuzipachika jina la ‘kampa kampa tena’. Hapa ndipo anapokuja Rodri.

Wahispaniola huwa hawana viungo kama Zinedine Zidane. Wana viungo kama Rodri. Anakupa anaachia, unampa tena, anaachia, unampa tena anakupa tena. Wapinzani wanaona kizunguzungu.. huu ndio msingi ambao unawatesa wapinzani wengi wanapokutana na soka la Kihispaniola.

Kitu kizuri katika hili ni kwamba dunia nyingine pia inajaribu kuiga kitu ambacho Wahispaniola wanafanya. Ndio maana leo tunawasifia makipa wengi kwa kutumia miguu zaidi kuliko mikono. Tunawasifia walinzi wengi ambao wanajua kumiliki mpira kuliko kubutua.

Kama hatutajifunza kwa Wahispaniol abasi hatutajifunza tena. Kuna yule muhenga ambaye aliwahi kutuambia kwamba ‘asiyefunzwa na mamae ufunzwa na ulimwengu’. Huku katika mpira ukweli ni ‘asiyefunzwa na Wahispaniola atafunzwa na ulimwengu’.