Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cristiano Ronaldo anavyoanza kuaga taratibu..!

CR7 Pict

Muktasari:

  • “Huenda huu ukawa mwaka wangu wa mwisho kucheza soka, na nataka kuacha urithi wa kipekee,” anasema Ronaldo maarufu pia kama CR7.

MADEIRA, URENO: CRISTIANO Ronaldo anakaribia kuanza msimu ambao unaweza kuwa wa mwisho kwake kama mchezaji wa soka la kulipwa, jambo alilolisema mwenyewe kwenye mahojiano na jarida la Vogue, katika makala iliyolenga zaidi ndoa yake ya hivi karibuni na Georgina Rodríguez pamoja na maisha yao ya kifamilia.

“Huenda huu ukawa mwaka wangu wa mwisho kucheza soka, na nataka kuacha urithi wa kipekee,” anasema Ronaldo maarufu pia kama CR7.

Nyota huyo ana maelngo mengi mapya katika maisha yake baada ya soka, akisema ana miaka kadhaa ya kuvutia mbele yake.

Anasema: “Nimepanga kikamilifu maisha yangu ya baadaye. Nina mambo mengi sana yatakayonishughulisha kiasi kwamba siwezi kutaja jambo moja tu. Kwa sababu soka linaweza kuacha pengo kubwa, hivyo unatakiwa kulijaza kwa mambo kadhaa. Siyo jambo moja pekee.”

CR 02

“Itakuwa jambo la kufurahisha kusafiri zaidi, kucheza na kutazama padel (mchezo unaochanganya mbinu za tenisi na skwashi. Huchezwa na wachezaji wanne kwa pamoja wawili kila upande kwenye uwanja mdogo uliovungwa kwa kuta za glasi au wavu wa chuma ambazo huruhusu mpira kudunda na kuendelea kuchezwa), mchezo ninaoupenda sana, na kuendelea kufurahia kile nilichokipata, au kile tulichokipata. Kwa sababu, baada ya yote, miaka hii 25 (katika soka) imehusisha kujitoa na kujinyima sana.”

CR 01

MKATABA WA RONALDO NA AL NASSR

Ronaldo ana mkataba na Al Nassr hadi Julai 2027 na kufikia wakati huo, staa huyo wa Ureno atakuwa tayari ametimiza umri wa miaka 42.

Pia anatarajiwa kuwa amefikia hatua ya kihistoria ya kufikisha mabao 1,000 katika maisha yake ya soka, huku kwa sasa akiwa amebakiza 30  kufikia idadi hiyo.

CR 05

Al Nassr ilicheza mchezo wake wa kwanza wa ligi msimu huu juzi, Jumamosi na kushinda kwa urahisi mabao 3-0 bila Ronaldo kuwepo uwanjani.

Mchezaji huyo aliwasili Saudi Arabia siku chache zilizopita na alishuhudia mchezo huo akiwa jukwaani pamoja na Georgina na baadhi ya watoto wao.

CR 04

NDOA YA CR 7 NA GEORGINA

Ronaldo na Georgina walioana siku chache zilizopita katika sherehe ya faragha. Hata hivyo, mwanamitindo huyo mwenye asili ya Hispania na Argentina alifichua kuwa: “Katika siku zijazo, tunataka kufanya harusi kubwa na kusherehekea pamoja na familia na marafiki zetu.”

Anasema mwaka huu umekuwa wa shughuli nyingi kutokana na majukumu ya kikazi, mashindano na malezi ya watoto. Kwa sasa, familia ya Ronaldo na Georgina ina watoto watano ikiwa ni Cristiano Jr, Eva, Mateo, Alana na Bella.

CR 03

Lakini, mwanasoka huyo alipoulizwa na jarida hilo kama angependa kupata watoto zaidi, Ronaldo alijibu: “Watoto zaidi? Siwezi kukataa.”

Georgina anaongeza: “Kupata mtoto mwingine sasa hivi tutakuwa na watu wengi sana nyumbani. Lakini watoto wadogo watakapofikisha miaka 15 au 16, bado tutakuwa vijana, kwa hiyo kwa nini isiwezekane? Ni kweli kwamba siwezi kufikiria nikiwa sina watoto wadogo, hivyo tutaona.”

Hilo huenda pia likawa sehemu ya maisha ya wanandoa hao siku za baadaye ambayo huenda hayatahusu tena kucheza soka la kulipwa.