Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Charles Ahoua Mwamba aliyeondoka Simba akiacha namba za kutisha


ALIYEKUWA kiungo mshambuliaji wa Simba raia wa Ivory Coast, Jean Charles Ahoua, amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na CR Belouizdad inayoshiriki Ligi Kuu ya Algeria, inayonolewa na kocha mkuu wa zamani wa Yanga, Mjerumani Sead Ramovic.


Ramovic alijiunga rasmi na Yanga Novemba 15, 2024, baada ya kuachana na kikosi cha TS Galaxy ya Afrika Kusini kutokana na mwenendo mbaya ili kuchukua nafasi ya Miguel Gamondi, ingawa Mjerumani huyo aliondoka kikosini humo Februari 4, 2025.

Kiujumla, Ramovic aliiongoza Yanga katika jumla ya mechi 13, za mashindano mbalimbali kuanzia Ligi Kuu Bara, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na Kombe la Shirikisho la FA, ambapo kati ya hiyo alishinda tisa, sare miwili na kupoteza miwili.

Kwa upande wa Ahoua aliyejiunga na Simba Julai 3, 2024, akitokea Stella Club d’Adjame ya Ivory Coast, alikuwa mchezaji bora wa Ligi ya Ivory Coast msimu wa 2023-2024, baada ya kuhusika na mabao 21, akifunga 12 na kuchangia tisa (Assisti).

Ahoua aliyewahi kuzitumikia timu za LYS Sassandra na Sewe Sports kabla ya kukipiga Stella, amejiunga na CR Belouizdad, baada ya kuitumikia Simba mwaka mmoja na nusu, licha ya kubakisha mkataba wa miezi sita uliokuwa unaisha Juni 30, 2026.

Licha ya nyota huyo kucheza kwa kipindi cha msimu mmoja na nusu, ila ameacha rekodi za kibabe katika Ligi Kuu Bara na mashindano mbalimbali ikiwemo ya kimataifa ambayo itaendelea kukumbukwa, kama ambavyo Mwanaspoti linazielezea kwa kina.

MFUNGAJI BORA

Licha ya kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji, ila mojawapo ya jambo kubwa litakalokumbukwa kwa nyota huyo katika timu ya Simba ni kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita wa 2024-2025, ikiwa ni msimu wake wa kwanza kikosini.

Nyota huyo aliibuka mfungaji bora baada ya kufunga mabao 16 na kuirejesha tuzo hiyo Simba, baada ya msimu wa 2023-2024, kuchukuliwa na aliyekuwa kiungo wa Yanga, Stephane Aziz KI anayeichezea Wydad Casablanca ya Morocco aliyefunga mabao 21.

Kabla ya Ahoua, mara ya mwisho kwa mchezaji wa Simba aliyechukua ni aliyekuwa kiungo, Mrundi Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’, aliyefunga mabao 17, sawa na nyota wa zamani wa Yanga anayeichezea kwa sasa Pyramids ya Misri, Mkongomani Fiston Mayele.

Msimu wa 2024-2025, Ahoua alichangia mabao 25 kati ya 69, yaliyofungwa na Simba katika Ligi Kuu baada ya kufunga 16 na kuasisti tisa, huku akiiwezesha kumaliza ya pili na pointi 78, nyuma ya mabingwa watetezi Yanga iliyomaliza na pointi 82.

Kwa msimu huu, kiungo huyo ameondoka akiwa amechangia mabao mawili ya Ligi Kuu Bara, baada ya kufunga moja na kuasisti moja, ambapo yote yalikuwa katika ushindi wa timu hiyo wa 3-0, dhidi ya Fountain Gate, mechi ikipigwa Septemba 25, 2025.

REKODI YA KIMATAIFA

Katika michuano ya kimataifa ambayo Simba ilikuwa inashiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu wa 2024-2025, Ahoua alichangia mabao matano, baada ya kufunga matatu na kuasisti mawili, yaliyoiwezesha kufika hadi fainali baada ya miaka 32.

Simba iliichukua miaka 32, tangu mara ya mwisho kikosi hicho kilipocheza fainali ya Kombe la CAF mwaka 1993, dhidi ya Stella Abdijan ya Ivory Coast na kuchapwa jumla ya mabao 2-0, chini ya aliyekuwa Kocha Mkuu, Abdallah ‘King’ Kibadeni.

Katika fainali ya msimu wa 2024-2025, Simba ilicheza na RS Berkane kutoka Morocco na kuchapwa ugenini mabao 2-0, Mei 17, 2025, huku marudiano visiwani Zanzibar, Mei 25, 2025, zikatoka sare ya bao 1-1 na kukosa ubingwa kwa jumla ya mabao 3-1.


ANGA ZA MAXI NZENGELI

Licha ya kuondoka, ila Ahoua alifikia rekodi iliyowekwa na nyota wa Yanga, Maxi Mpia Nzengeli katika msimu wa kwanza wa Ligi Kuu kwenye mechi 10 za mwanzo, huku wakitoka kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu ‘MVP’ katika timu walizotokea.

Ahoua aliyejiunga na Simba msimu wa 2023-2024, akitokea Stella Club Adjame ya kwao Ivory Coast, katika mechi 10 za Ligi Kuu na timu hiyo, alifunga mabao matano na kuasisti manne, sawa na Maxi Nzengeli aliyefanya hivyo, msimu wa 2023-2024.

Nyota huyo aliyezitumikia timu za LYS Sassandra na Sewe Sports kabla ya kukipiga Stella, alikuwa mchezaji bora wa Ligi ya Ivory Coast msimu wa 2023-2024, baada ya kuhusika na mabao 21 ya timu hiyo, akifunga 12 na kuchangia tisa (assisti).

Kwa upande wa Maxi ambaye pia alikuwa mchezaji bora wa msimu ‘MVP’ wa Ligi ya DR Congo msimu wa 2020-2021, msimu wake wa kwanza na Yanga akitokea AS Maniema Union, katika mechi 10 za mwanzo za Ligi Kuu alihusika na mabao tisa sawa na Ahoua.

Ujio wa Ahoua ulimfanya kufikisha nyota watatu waliotoka Ivory Coast na kuibuka wachezaji bora wa msimu (MVP), baada ya Stephane Aziz KI msimu wa 2022-2023, aliyetua Yanga akitokea ASEC Mimosas, kisha kutimkia Wydad Casablanca ya Morocco.

Mwingine ni kiungo mshambuliaji, Pacome Zouzoua aliyejiunga pia na Yanga kwa mara ya kwanza msimu wa 2023-2024 akitokea ASEC Mimosas ya kwao Ivory Coast, ambapo nyota huyo anaendelea kuonyesha kiwango kizuri katika mashindano mbalimbali.

REKODI YA CHAMA

Licha ya mashabiki kutokuwa na imani na Ahoua baada ya kuondoka kwa Clatous Chama ‘Triple C’ aliyejiunga na Yanga kisha msimu huu kujiunga na Singida Black Stars kabla ya kurudi Msimbazi, nyota huyo msimu wake wa kwanza amemfunika mwamba huyo wa Lusaka.

Ahoua aliletwa Simba ili akawe mbadala wa Chama aliyefanya makubwa na kikosi hicho cha Msimbazi na kujizoelea umaarufu mkubwa, kuanzia michuano mbalimbali ikiwemo Ligi Kuu Bara na ile ya Kimataifa ambayo alikuwa mwiba kwa wapinzani zaidi.

Tangu atue ndani ya kikosi cha Msimbazi, Ahoua ameivunja rekodi ya mabao ya Chama aliyoiweka msimu wa kwanza wa 2018-2019, akitokea Lusaka Dynamos ya kwao Zambia, alipochangia 16 ya Ligi Kuu Bara, baada ya kufunga saba na kuasisti tisa.

Msimu wa 2024-2025, alichangia mabao 25 kati ya 69 yaliyofungwa na Simba katika Ligi Kuu baada ya kufunga 16 na kuasisti tisa, akiiwezesha kumaliza ya pili na pointi 78, nyuma ya mabingwa watetezi Yanga iliyomaliza na pointi 82.