Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

John Cena amestaafu, akaunti inasoma mabilioni ya fedha

ATM Pict

Muktasari:

  • Gwiji huyo raia wa Marekani alitangaza kustaafu Desemba 13 ikiwa ni baada ya kuhudumu katika mchezo huo kwa karibia miaka 20 akishinda mikanda mbalimbali ikiwamo ya ubingwa wa dunia alioutwaa mara 16.

FLORIDA, MAREKANI: BAADA ya kutangaza rasmi kustaafu mieleka (WWE), jina la John Cena limeendelea kubaki juu kama mmoja wa mastaa waliowahi kutengeneza historia kubwa katika mchezo huo.

Gwiji huyo raia wa Marekani alitangaza kustaafu Desemba 13 ikiwa ni baada ya kuhudumu katika mchezo huo kwa karibia miaka 20 akishinda mikanda mbalimbali ikiwamo ya ubingwa wa dunia alioutwaa mara 16.

Cena kwa sasa anadaiwa kuwa atajikita zaidi katika kuigiza. Lakini kwa miaka hiyo aliyopigana katika ulingo wa mieleka, mbabe huyu ameingiza kiasi kikubwa cha pesa kinachotakana na kazi hiyo kiasi cha kuwa mmoja kati ya mamilionea na wapiganaji mieleka wenye pesa za kutosha. Leo tumekusogezea hapa katika ATM.

AT 01

ANAPIGAJE PESA?

Kwa miaka mingi, sehemu kubwa ya kipato cha John Cena ilitokana na mikataba yake na WWE, ambapo aliwahi kulipwa takribani Dola 10 milioni.

Mbali na mieleka, Cena amejijengea jina kubwa katika tasnia ya filamu, akishiriki kwenye filamu maarufu kama Fast & Furious 9, The Suicide Squad, Peacemaker, Bumblebee na nyingine nyingi.

Kupita ugizaji hadi sasa anakadiriwa kupata takribani Dola 150 milioni.

Cena pia ni balozi wa kampuni kadhaa kubwa zikiwamo za Gillette, Capri Sun, Honda, Hefty, Fruity Pebbles na Experian. Kupitia matangazo na mikataba ya udhamini, Cena anakadiriwa kuingiza zaidi ya Dola 20 milioni kwa mwaka. Kwa ujumla, utajiri wake unakadiriwa kufikia Dola 90 milioni.

AT 04

NYUMBA

Anamiliki jumba kubwa la kifahari huko Tampa, Florida, lenye thamani ya zaidi ya Dola 4 milioni. Nyumba hiyo ina vyumba 10, sehemu ya kufanyia mazoezi binafsi, bwawa kubwa la kuogelea, gereji kubwa ya magari na eneo maalum la kuburudika.

Pia anaripotiwa kumiliki nyumba nyingine ndogo kwa matumizi binafsi huko California, karibu na maeneo ya studio za filamu, kwa ajili ya kurahisisha shughuli zake za uigizaji.

AT 02

NDINGA

Ford GT - Dola 500,000

Dodge Viper - Dola 120,000

Chevrolet Corvette ZR1 - Dola 135,000

Ferrari 599 GTB Fiorano - Dola 310,000

Lamborghini Gallardo - Dola 200,000

Mercedes-Benz SLS AMG - Dola 200,000

Rolls-Royce Phantom - Dola 450,000

AT 03

MSAADA KWA JAMII

John Cena ni mmoja wa mastaa waliotoa msaada mkubwa kwa jamii. Kupitia taasisi ya  Make-A-Wish Foundation ambayo wagonjwa walio kwenye siku zao za mwisho pamoja na walemavu huweka ndoto zao za wasanii au watu maarufu wanaotaka wawatembelee, John Cena ametembelea zaidi ya watu 650 ikiwa ni idadi ya juu zaidi kuliko mtu mwingine yeyote.

Staa huyu pia amekuwa akishiriki kampeni za kusaidia wanajeshi wastaafu, watoto yatima na miradi ya elimu, huku mara nyingi akifanya misaada hiyo kimya kimya bila macho ya vyombo vya habari.

AT 05

MAISHA BINAFSI NA BATA

Awali, John Cena alikuwa katika ndoa na Elizabeth Huberdeau, lakini walitalikiana mwaka 2012. Baadaye alihusishwa kuwa katika uhusiano na mwanamieleka Nikki Bella ambao uliovunjika kabla hawajafunga ndoa.

Mwaka 2020, Cena alifunga ndoa na Shay Shariatzadeh, mhandisi raia wa Canada, na hadi sasa bado anaishi naye.

Licha ya umri kumtupa mkono, Cena hadi sasa hana mtoto hata mmoja.