Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Babra Banda na rekodi kibao

BABRA Pict

Muktasari:

  • Miongoni mwa nyota mwenye mchango mkubwa kwenye kikosi hicho ni mshambuliaji Babra Banda anayekipiga katika klabu ya Orlando Prides ya Ligi Kuu ya Wanawake Marekani akiwa mchezaji muhimu kwenye kikosi hicho.

HAKUNA ubishi juu ya ubora wa Timu ya Taifa ya wanawake, Zambia unachangiwa na ubora wa wachezaji wake wanaokipiga kwenye Ligi kubwa barani Ulaya.

Miongoni mwa nyota mwenye mchango mkubwa kwenye kikosi hicho ni mshambuliaji Babra Banda anayekipiga katika klabu ya Orlando Prides ya Ligi Kuu ya Wanawake Marekani akiwa mchezaji muhimu kwenye kikosi hicho.

Hivi karibuni alimbwa sana baada ya kuonyesha kiwango bora kwenye mechi yake ya kwanza kufunga mabao manne kwenye ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Misri katika mchezo wa Kundi C wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026.

Mabao hayo yalimfanya nahodha huyo kuchaguliwa malkia wa mchezo na kusema kuwa kazi ndio imeanza ya kusaka historia nyingine kwenye mashindano hayo.

Haikuwa mara ya kwanza kwa Banda kuibeba Zambia mabegani. Alianza  kuitumikia timu ya taifa mwaka 2016 na amekuwa na mchango mkubwa kwenye mafanikio ya timu hiyo.

Kila mashindano makubwa yamekuwa yakimpa nafasi ya kuonyesha ubora wake, huku akiweka rekodi ambazo zimemfanya kuwa moja ya nyota wakubwa wa kike Afrika.

"Kila ninapoingia uwanjani, nataka kuweka historia kwa ajili ya nchi yangu.Ninajivunia nilichokifanya, lakini jambo muhimu zaidi ni kuisaidia Zambia kufanikiwa kila mwaka," anasema Banda.


BAB 01

REKODI ZAKE

Nyota huyo alianza kupata umaarufu mkubwa zaidi mwaka 2021 alipoiwezesha Zambia kufuU kwa mara ya kwanza kwenye michezo ya Olimpiki ya Tokyo.

Mashindano hayo yaliyofanyika nchini Japan Banda aliweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza  kufunga Hat-trick mbili mfululizo kwenye Olimpiki.

Alifunga mabao matatu dhidi ya Uholanzi, kisha akafanya hivyo tena dhidi ya China, rekodi ambayo hadi sasa haijavunjwa. Ilikuwa siku ambayo dunia ilianza kumtambua.

Tangu aanze kuitumikia Zambia kwa mara ya kwanza mwaka 2018 Banda ameichezea mechi 23 akifunga mabao 25.

"Rekodi zipo ili zikutie hamasa kufanya kazi kwa bidii zaidi, si kukufanya uridhike, kama mshambuliaji kazi yangu ni kufunga mabao, lakini kila bao lina thamani zaidi linaposaidia timu kushinda."

BAB 02

KOMBE LA DUNIA

Mwaka 2023 aliandika historia baada ya kufunga bao kwenye mechi za makundi za Kombe la Dunia nchini Australia na New Zealand ambao ndio walikuwa waandaaji wa fainali hizo.

Miongoni mwa bao lake alifunga dhidi ya Costa Rica kwa mabao 3-1na kupata ushindi wake wa kwanza kabisa katika historia ya michuano hiyo, mafanikio yaliyoongeza heshima ya taifa hilo kwenye ramani ya soka la wanawake duniani.

"Labda siku moja, nani anajua, tunaweza kushinda Kombe la Dunia au Olimpiki. Lazima tuendelee kuota ndoto kubwa lakini kwa upande wangu mimi kuandika rekodi kwenye mashindano hayo makubwa."

BAB 03

LIGI YA MAREKANI

Mbali na timu ya taifa, Banda anafanya vizuri pia akiwa na kikosi cha Orlando Pride, ambapo amekuwa mmoja wa washambuliaji wanaogopwa zaidi ndani ya ligi hiyo.

Msimu uliopita akiwa na timu hiyo alifunga mabao 12 na asisti moja kwenye mechi 15 alizocheza kwa dakika 1101.

Akiitumikia Orlando, amekuwa mmoja wa washambuliaji bora  katika Ligi ya NWSL kutokana na kasi yake, nguvu, uwezo wa kupiga mashuti kwa miguu yote miwili na kumalizia nafasi kwa utulivu.

Ubora huo ulimfanya ashinde tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kupitia tuzo za CAF.heshima inayotolewa kwa mchezaji bora wa Afrika, na kuthibitisha kuwa ndiye sura ya kizazi kipya cha soka la wanawake barani.

Kabla ya kuitumikia Orland aliwahi kuichezea Dux Lugrono ya Hispania msimu wa 2018/20 akifunga mabao 15 kwenye mechi 28.

"Nataka watu wajue kwamba Barbra Banda yuko uwanjani ninapocheza. Nataka kujenga jina langu mwenyewe na kuacha alama duniani," anasema Banda.

BAB 03 (1)

Kinachomtofautisha Banda na washambuliaji wengi sio upachikaji wa mabao. Ana uwezo wa kubeba majukumu ya uongozi akiwa nahodha wa Zambia, kuwatengenezea nafasi wenzake na kubadilisha matokeo ya mechi ndani ya dakika chache.

Mabeki wengi wamekuwa wakipata tabu kumkaba nyota huyo jambo linalowaachia nafasi wachezaji wengine wa Zambia kushambulia.

WAFCON ya mwaka huu inaweza kuwa  upande wake. Zambia haijawahi kutwaa ubingwa wa Afrika kwa wanawake, lakini kizazi hiko kinachoongozwa na Banda kinaonekana kuwa na uwezo wa kuvunja ukuta wa mabeki.

Ushirikiano wake na mshambuliaji mwenzake, Racheal Kundananji, umeifanya Zambia kuwa moja ya timu zenye safu kali zaidi ya ushambuliaji katika mashindano haya.

BAB 04 (1)

Iwapo Banda ataendelea na kasi aliyoianza dhidi ya Misri, ana nafasi kubwa ya kumaliza akiwa mfungaji bora wa mashindano. Pia anaweza kuvunja baadhi ya rekodi za mabao katika WAFCON na kuipeleka Zambia hatua ambayo haijawahi kufikiwa.

Pamoja na ushindani mkali kutoka kwa nyota wengine wa Afrika kama Ghizlane Chebbak wa Morocco, Rasheedat Ajibade wa Nigeria na Thembi Kgatlana wa Afrika Kusini, Banda bado anaonekana kuwa mchezaji ambaye anaweza kubadili sura ya mashindano kwa uwezo wake binafsi. Anahitaji nafasi chache tu kuwaadhibu wapinzani, na hilo limedhihirika katika karibu kila mashindano makubwa aliyoshiriki.

Sasa, macho ya Afrika yako kwa nahodha huyo wa Zambia. Je, ataendelea kuandika historia nyingine nchini Morocco?