Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Anachofanya Morice Abraham hakuna cha kushangaza, amezoea

JICHO Pict


HAKUNA kitu cha kushangaza sana kuhusu Morice Abraham. Mashabiki wa Simba wanashangaa kuhusu kipaji chake. Kiungo maridadi katika eneo la katikati pale Msimbazi. Kwa sasa anaendelea kuimbwa kuliko wachezaji wengi wa kigeni walionunuliwa dirisha kubwa.


Mfupi kama alivyo, Morice ni fundi. Anajua kucheza mpira rahisi. Ana nguvu na ni mpambanaji. Mguu wake wa kushoto anajua kuutumia vema. Ni kiungo wa kisasa kwa sababu anakuwa bora wakati timu ikiwa bora wakati ana mpira na wakati akiwa hana mpira.


Morice anaimbwa kama vile ni mchezaji wa kigeni. Hapana. Ni mtanzania tu. Kwanini imekuwa ghafla sana kwake kuimbwa? Kuna sababu kadhaa. Tuache unazi uliopitiliza katika mpira wetu. Kuna mashabiki wengi ambao hawafuatilii soka la vijana. Wanachowaza wao ni Yanga na na Simba tu halafu basi.

Nilikwenda na kikosi cha Taifa Stars Indonesia Februari mwaka jana katika pambano la kirafiki ambalo wachezaji wetu wakubwa walilidharau, mashabiki wakalidharau, na kila mtu akaonekana kulidharau.

Morice alikuwa mchezaji bora wa mechi katika pambano. Baadaye mawakala waliojitokeza kutazama mechi wakaniulizia sana kuhusu yeye ingawa wengi iliwakata maini kuhusu ukweli alikuwa tayari anacheza Ulaya.

Morice ni kijana wetu ambaye alikuwa staa katika ile timu ya vijana ambayo ilimtambulisha Kelvin John. Kwa sababu hatupendi soka la vijana huwa hatuwafuatilii vijana wetu. Kuanzia katika klabu zetu hadi wale vijana wa timu zetu za taifa za vijana. Watu wachache huwa wanajitokeza katika mechi zao na kutunza kumbukumbu.

JICH 01

Kwa waliomtazama Morice wakati ule wala hawashangazwi na anachokionyesha uwanjani. Ilikuwa ni suala tu la kufuatilia tu kwamba baada ya pale Morice angeenda wapi. Na hata baada ya hapo hakuna aliyejua Morice alikuwa amekwenda Ulaya.

Kama angekuwa mchezaji wa Simba au Yanga amekwenda Ulaya nadhani mashabiki wangelazimisha dunia ifahamu.

Aliyepata bahati ya kufahamika katika wale na akapata jina ni Kelvin John. Alikuwa mkubwa kwa wakati ule lakini pia alikwenda katika timu ambayo staa wetu mkubwa Mbwana Samatta alikuwa akicheza. Genk.

Hawa kina Morice hawakupata bahati ya kufahamika kwa sababu hawakwenda Genk. Kuna vijana pia walikwenda Ulaya Mashariki kama Morice lakini hawakupata bahati ya kufahamika.

Hainishangazi sana pia kuhusu Morice kwa sababu anaingia katika mkumbo wa mchezaji kama Erasto Nyoni. Erasto alikuwa hapa hapa nchini na alikuwa anacheza Azam na timu ya taifa ya Tanzania lakini mashabiki hawakujua ubora wake mpaka alipotinga Simba.

JICH 02

Alipotinga Simba tu ndio mashabiki mashabiki walijua Erasto alikuwa na kipaji kikubwa cha kumiliki mpira na kutumia akili kubwa katika mpira.

Wakati anavaa jezi ya Azam na timu ya taifa mashabiki walikuwa hawajali sana kuhusu uwezo wake. Alipotinga Simba ndipo mashabiki wakaanza kumzingatia.

Ni kama ambavyo sasa hivi tumeanza kumzingatia kijana wetu ambaye amechezea timu zote za taifa hapa nchini.

Kuanzia ile ya chini ya umri wa miaka 17, kisha chini ya miaka 20, halafu timu ya wakubwa.

Nenda kawaulize mashabiki wa Yanga kama walikuwa wanamfahamu mchezaji anayeitwa Edmund John kabla hajatua Yanga. Wengi walikuwa hawamfahamu kabla hajavaa jezi ya Yanga. Hili ndio tatizo la mashabiki wetu. Huwa wanaziangalia timu zao tu. Huwa hawaangalii mashabiki wa timu nyingine. Ni ugonjwa. Ni kansa.

Kitu kingine ambacho kimeendelea kutukumbusha mashabiki ni namna ambavyo wachezaji wetu wana safari ndefu ya kucheza kwa mafanikio barani Ulaya na kwingineko. Huyu Morice alikuwa anacheza soka la kulipwa nchini Serbia. Aliondoka zake kimya kimya lakini leo yupo nchini. Tunapomtazama kwa sasa tunaamini ni kipaji kinachopaswa kuonekana na kucheza Ulaya. Kumbe alikuwa anacheza Ulaya!.

Fikiria ni namna gani alishindwa kusonga mbele zaidi na kufikia hatua ambazo akina Claude  Makelele, John Obi Mikel, Jay Jay Okocha na wengine kutoka Afrika walifika. Ameishia Serbia kimya kimya na amerudi  nchini huku akionyesha kipaji chake maridhawa.

JICH 03

Kuna somo la kujifunza kwa vijana wetu. Maisha ya mafanikio nje ya Tanzania sio

Sio Morice tu, kuna vijana wengi ambao wamerudi nchini na wanaonyesha uwezo mkubwa lakini walishajaribu nje na wameshindwa kwenda mbele zaidi. Mfano ni mlinzi, Hamza Abdulrazak. Mashabiki wengi walishangaa uwezo wake alipotua uwezo wake kumbe alikuwa anacheza ligi kuu ya Afrika Kusini.

Hapo kuna mambo mawili tulikuwa hatuyafahamu. Kwanza hatukufahamu uwezo wake akiwa anacheza nchini lakini pia hatukufahamu alikuwa anacheza katika ligi kuu ya Afrika Kusini timu ya SuperSport ambayo sio timu ya kinyonge katika mpira wa nchi hiyo.

Tatizo lake ni hakucheza Simba wala Yanga kabla ya hapo.

Kitu kizuri kuhusu Morice na ambacho tunapaswa kukumbuka ni ukweli kuibuka kwake kuwa mchezaji muhimu ni faraja kwetu.

Hapo katika eneo lake kulikuwa na Jonas Mkude ambaye alituwakilisha vema katikati ya kundi la wageni. Walau Yusuf Kagoma alikuja kutufuta machozi.

Kimekuwa kitu cha nadra kwa wachezaji wazawa kuchomoza katika kundi la wachezaji umuhimu klabuni.

Morice anaweza kuingia katiia kundi la kina Kagoma, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Shomari Kapombe, Dickson Job, Ibrahim Bacca, Clement Mzize na wengineo ambao wana uhakika wa kupata nafasi katika timu kubwa ambazo kiukweli zimetawaliwa na wachezaji wa kigeni.

Maurice anapambana kuingia katika kundi hili.

Kila la kheri kwake. Nadhani pia atapendwa zaidi na mashabiki wa soka wakati akiwa amevaa jezi ya timu ya taifa kwa sababu sasa hivi watakuwa wamemtambua. Ni simulizi zile zile za kina marehemu Godfrey Bonny na wachezaji wengi ambao huwa tunawafahamu baadae na kuwashangilia pindi tunapofahamu wanapotokea katika klabu zetu.