Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Jibebee’, wachezaji hawa hawana timu!

JIBEBEE Pict

Muktasari:

  • Huko sokoni unaambiwa kuna nyota wenye majina makubwa hawana timu na wako huru kusajiliwa na timu yoyote inayowataka katika kuimarisha vikosi vyao.

BRUSSELS, UBELGIJI: DIRISHA kubwa la usajili Ulaya lilishafungwa tangu Septemba Mosi, huku baadhi ya nchi zikimalizia malizia kuvuta nyota wapya.

Huko sokoni unaambiwa kuna nyota wenye majina makubwa hawana timu na wako huru kusajiliwa na timu yoyote inayowataka katika kuimarisha vikosi vyao.


Paul Pogba

Kiungo wa zamani wa Manchester United, Mfaransa Paul Pogba, 33, ambaye aliwahi kuwa mchezaji ghali zaidi ameachwa na Monaco baada ya kuvunjiwa mkataba.

Pogba amekuwa akiuguza majeraha mara kwa mara na tangu ametua katika klabu hiyo msimu uliopita aliichezea mechi sita, huku tano kati ya hizo akiingia kutokea benchi.  


Karim Benzema

Mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or 2022, kwa sasa hana timu baada ya kuondoka Al-Hilal ya Saudi Arabia.

Mchezaji huyo, 38, alijiunga na Al-Hilal mwezi Januari mwaka huu, lakini nafasi yake kikosini imechukuliwa na staa wa zamani wa Aston Villa Ollie Watkins. Hata hivyo, inadaiwa Benzema hana nia ya kurejea Ulaya.


JIBE 01

Riyad Mahrez

Mchezaji mwingine mwenye jina kubwa ambaye ameachwa na klabu za Saudi Arabia.

Mkataba wa Mahrez, 35,  na Al-Ahli ulisitishwa msimu huu wa joto, anaonekana kuwa tayari kubaki Mashariki ya Kati na kusaini mkataba mwingine wenye masilahi makubwa.

Hata hivyo, bado yupo mtaani mambo hayajawa mambo hadi sasa.


Raheem Sterling

Kwa upande mwingine, maisha ya soka ya yameingia katika kipindi kigumu na akiwa na umri wa miaka 31 bado hajaamua anakwenda klabu gani.

Aliachwa na Feyenoord baada ya kuitumikia kwa miezi mitatu akiichezea mechi nane.

Hata hivyo, nyota huyo wa zamani wa Manchester City, Chelsea na Liverpool bado ni mgodi mzuri unaotembea ambao iwapo utapata nafasi nzuri uwanjani na kutuliza akili, huenda ukatoa madini ya maana tu.


Philippe Coutinho

Amekuwa akihamahama klabu akitafuta kurejea kwenye kiwango chake cha zamani. Kwa sasa akiwa na amecheza klabu tano katika kipindi cha miaka minane tangu alipoondoka Liverpool kwenda Barcelona kisha alipita Bayern Munich, Aston Villa, Al-Duhail na Vasco da Gama. Hata hivyo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 hivi karibuni atafikisha klabu sita baada ya kuachwa na Vasco da Gama ya nchini kwao Brazil.


JIBE 02

Jadon Sancho

Mwamba mwingine anayesilizia ofa na alikuwa moja ya usajili mbaya zaidi katika historia ya Manchester United, baada ya Mashetani Wekundu kulipa Pauni 73 milioni kumnunua kutoka Borussia Dortmund.

Akiwa Man United baadaye aligoma kucheza, akagombana na kocha na hatimaye akashindwa kuonyesha kiwango kilichotarajiwa.

Alikwenda kwa mkopo Dortmund, Chelsea na Aston Villa, lakini hakurejesha kiwango cha ubora. Akiwa na umri wa miaka 26, Sancho anaonekana kuwa njiani kujiunga na Palmeiras ya Brazil, katika kile kinachoonekana kuwa moja ya usajili uliokatisha tamaa zaidi katika soka, ingawa dili hilo bado halijakamika hadi sasa.


David Alaba

Beki aliyekuwa akikipiga Real Madrid, ni usajili unaofaa kwa klabu ambayo imeshindwa kutatua matatizo yake ya ulinzi. Huenda hiyo ndiyo sababu Man United ni miongoni mwa timu zinazopewa nafasi kubwa ya kumsajili, kwa mujibu wa mitandao mbalimbali.

Mchezaji huyo, 34, aliondoka Real Madrid mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kuitumikia kwa miaka mitano.


Mauro Icardi

Anakumbukwa zaidi kutokana na uhusiano wake uliojaa drama na mrembo Wanda Nara, lakini akiwa na miaka 33 bado anaendelea kutafuta timu na huenda hatimaye akatua mojawapo pale England.

Mshambuliaji huyo aliondoka Galatasaray baada ya kumalizika kwa mkataba wake na sasa anatafuta mwanzo mpya. Vyombo vya habari vya Uturuki vilimtaja kama “tamthilia ya mtu mmoja inayotembea” kutokana na mambo yake ya nje ya uwanja.


JIBE 03

Anthony Martial

Mshindi wa tuzo ya Golden Boy 2015, Anthony Martial, hana timu baada ya kuondoka kwa makubaliano ya pande zote katika timu ya Monterrey ya Mexico.

Akiwa na miaka 30 inaonekana kama mshambuliaji huyo Mfaransa amekuwa kwenye soka kwa muda mrefu sana, lakini sasa anatafuta klabu ya tatu katika kipindi cha miaka mitatu tangu alipoondoka Manchester United kama mchezaji huru 2024.


Wilfried Zaha

Ni mchezaji ambaye huenda alichelewa sana kuondoka katika klabu yake aliyokuwa akiipenda ya Crystal Palace.  Zaha aliwahi kuhusishwa na karibu kila timu kubwa Ligi Kuu England alipoonekana kuwa tayari kuondoka Palace.

Hata hivyo, baada ya uhamisho wake kwenda Galatasaray 2023 kama mchezaji huru kushindikana, aliishia kucheza Ligi Kuu Marekani (MLS) akiwa na Charlotte. Na sasa akiwa na miaka 33 amekuwa akifanya mazoezi na Crystal Palace ili kurejesha utimamu wa mwili, lakini anaonekana kuwa tayari kuendelea na maisha yake ya soka nje ya England.


Oleksandr Zinchenko

Nyota wa kimataifa wa Ukraine, aliyesajiliwa na Arsenal chini ya Mikel Arteta kwa lengo la kuongeza uzoefu katika mbio za kuwania ubingwa dhidi ya Manchester City.

Hata hivyo, baada ya kuondoka kwa mkopo kwenda Nottingham Forest na baadaye Ajax, ndipo Arsenal hatimaye iliposhinda ubingwa wa Ligi Kuu England. Akiwa na miaka 29, beki huyo wa kushoto anayeweza kucheza nafasi mbalimbali bado hana klabu baada ya kuachwa na vigogo hao wa Amsterdam.


JIBE 04

Yves Bissouma

Ni mfano mwingine wa jinsi ambavyo maisha ya soka yanaweza kubadilika kwa kasi. Miaka michache iliyopita alionekana mmoja wa wachezaji muhimu katika kiungo cha Tottenham Hotspur, lakini sasa nyota huyo, 30, hana timu baada ya Spurs kuamua kutomwongezea mkataba.

Atahitaji kutatua changamoto za utimamu wa mwili na kiwango katika klabu yake inayofuata, lakini anaweza kuipa timu itakayomhitaji uzoefu wake wa kucheza Ligi Kuu.


Tyrell Malacia

Wakati Man United ilishindwa kumsajili beki wa kushoto baada ya kukubali kushindwa mapema katika jitihada za kumnunua Lewis Hall kutoka Newcastle United, mchezaji mmoja katika nafasi hiyo, Tyrell Malacia aliruhusiwa kuondoka.

Mchezaji huyo, 27, amekuwa akipitia kipindi kigumu kutokana na majeraha na sasa anahitaji klabu mpya itakayomsaidia kurejesha kiwango na kujiamini.