Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wamebambwa utamu!

Diamond na Zari

Muktasari:

  • Katika nguzo hii, waumini hujizuia kula na kunywa mchana kutwa, sambamba na kujipinda katika kutenda mambo mema na kuepuka maovu, huku pia wakiomba msamaha kwa Mola wao kwa matendo yote waliyofanya miezi 11 iliyopita.

WAUMINI wa dini ya Kiislam duniani wapo katika mfungo wa Mwezi wa Ramadhani. Mfungo huo ni moja kati ya nguzo tano za dini ya Kiislam, ikiwa ni nguzo ya nne.

Katika nguzo hii, waumini hujizuia kula na kunywa mchana kutwa, sambamba na kujipinda katika kutenda mambo mema na kuepuka maovu, huku pia wakiomba msamaha kwa Mola wao kwa matendo yote waliyofanya miezi 11 iliyopita.

Kwa waumini wanaojitambua na kufahamu umuhimu wa ibada hii, huwa hawafanyi utani, hutumia muda mwingi kuepuka machafu yote ambayo walikuwa wakiyatenda.

Hata baadhi ya mastaa nchini ambao ni waumini wa dini hiyo, hawapo nyuma katika kutekeleza ibada hiyo, wakibadili aina ya maisha waliyokuwa wakiishia siku za nyuma. Kuna walioachana na matumizi ya vilevi kwa sasa na wengine kutengana na wenza wao waliokuwa wakiishi nao kama mke na mume, ili tu kupata wasaa wa kujikita katika ibada hiyo ya mfungo wa Ramadhan.

Ingawa kwa mafundisho ya Kiislam vitendo vyote haramu vimekatazwa, lakini kwa kujishtukia mastaa hao wanaona ni vyema kutafuta fadhila za Mola wao kwa kuepuka baadhi ya dhambi.

Ndiyo maana wapo walioamua kuoa kabla ya kuingia mfungoni ili kupata fadhila, kwa wale ambao wameshindwa kuoa wamewatema kwa muda wenzao wao na Mwanaspoti linakuletea baadhi ya mastaa hao.

JUX NA VANESSA

Wawili hao ni wenza wa siku nyingi na kati ya mastaa wanaokimbiza kwenye fani ya sanaa. Jux yeye ni muumini wa Kiislam, majina yake kamili yakiwa ni Juma Mussa ‘Jux’, katika kuhakikisha avurugi funga yake imedaiwa kwa sasa ametengana kwa muda na Vanessa Mdee ‘Vee Money’ ili kupisha mfungo wa Ramadhan.

HARMONIZE NA WOLPER

Wenza hawa wamekuwa gumzo kwa siku za karibuni, kutokana na penzi lao kumea ghafla kama uyoga. Harmonize staa kutoka Lebo ya Wasafi (WCB) anayejipenyeza kwa kasi kwenye Bongo Fleva ameangukia mikononi mwa mwigizaji nyota, Jacklyne Wolper.

Harmonize ni muumini wa Kiislam na majina yake kamili ni Rajab Abdulrahman, kwa sasa inadaiwa ameamua kujiweka kando na Wolper, ili kupisha mfungo, yaani mfungo umemnasa utamu wakati ndiyo kwanza penzi lake likichipukia.

DUDE NA EVA

Mtayarishaji na mwigizaji wa filamu nchini, Kulwa Kikumba ‘Dude’ naye yumo kwenye orodha hii ya kutengana na mwenza wao. Inadaiwa Dude kwa sasa ametengana kwa muda na mchumba wake Eva, aliyejaliwa naye kupata watoto wawili.

Dude alikaririwa na mwandishi huyu akisema anaona siku zinazidi kwenda toka aseme atafunga ndoa na Eva, hivyo hadi mwezi mtukufu umefika imemkuta akiwa hajatekeleza ahadi yake. Hivyo anaendelea kuteseka kwa kula futari kwa mama ntilie, tofauti na mipango ya kupikiwa na kula nyumbani. Atafanyaje na mwezi umemnasa bhana! Dude alifunguka na kusema kutokana na sheria za Kiislamu kwamba hairuhusiwi mwanamume kupikiwa futari na mwanamke anayeishi naye tu bila kufunga ndoa. Sio kula tu, hata kulala naye pia ni mitihani na hivyo kwa sasa analazimika kulala nyumba ya wageni, ili tu kuupisha mfungo.

IDRISA NA WEMA

Hawa ni wapenzi wanaofuatiliwa na mashabiki wao kwa karibu mno. Nao wapo kwenye orodha hii kwa sababu wameamua kutengana kwa muda kwa ajili ya kufunga mwezi wa Ramadhani. Kabla mwezi kuingia walikuwa pamoja kila mahala kama kumbi kumbi, lakini kwa sasa kila mtu anafanya mambo kivyake ili tu kuupisha mwezi wa Ramadhan.

DIAMOND NA ZARI

Staa wa kimataifa wa Bongofleva, Diamond Platinumz kabla ya kuanza mwezi alikuwa Afrika Kusini kwa mzazi mwenzie, Zarina Hassan ‘Zari thebosslady’ aliyezaa naye mtoto mmoja wa kike, Latifa ‘Tiffah’.

Inaelezwa kuwa Diamond alienda kuweka mambo sawa ya kukubaliana na mweza wake huyo kuwa wanapaswa kutokuwa karibu kwa sasa ili kupisha mfungo.

Diamond anasema pamoja na mambo mengine yote, huwa hakosi funga ya mwezi wa Ramadhan, hivyo haipendezi kwake kuona anaendelea kuwa karibu na Zari wakati bado hawajafunga ndoa. Bahati mbaya zaidi ni kwamba wote ni waumini wa Kiislam tofauti na wenza wengine ambao ni mseto wa dini tofauti.

Kwa taarifa zaidi nunua gazeti lako la Mwanaspoti au soma mtandaoni kupitia www.epaper.mcl.co.tz