Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Singeli ndiyo utambulisho wa Hamisa Mobetto

MOBETTO Pict

Muktasari:

  • Moja ya utambulisho wake ni muziki wa Singeli, ambao umeonyesha Hamisa ni nani na kipi anaweza kukifanya kwa ufanisi zaidi kwa upande huo ambao sasa ameamua kumpa kisogo.

KWA kipindi cha takribani miaka miwili ambacho mwanamitindo na mshawishi wa chapa, Hamisa Mobetto alijihusisha na muziki akiwa kama mwimbaji, alifanya vingi na kujenga utambulisho wake kwa kiasi chake.

Moja ya utambulisho wake ni muziki wa Singeli, ambao umeonyesha Hamisa ni nani na kipi anaweza kukifanya kwa ufanisi zaidi kwa upande huo ambao sasa ameamua kumpa kisogo.

Julai 2021, Hamisa kwa mara ya kwanza alisikika katika wimbo wa Singeli uitwao ‘Ex Wangu’ ambao alishirikiana na mwimbaji wa muziki huo, Seneta Kilaka huku ukitayarishwa na Kenny.

Hamisa alikuwa msanii wa tatu wa kike Bongo ndani ya mwezi huo kuachia wimbo wa Singeli  na alianza Zuchu na wimbo wake ‘Nyumba Ndogo’, kisha akafuatia Menina na wimbo wake, Nyumba Kubwa.

MOBE 05

Umaarufu wa wimbo huo uliotokana hasa na ujumbe uliopo ndani yake na Hamisa alidai kusumbuliwa na mpenzi wake zamani (ex). Anahoji nani yupo naye maana anapiga sana simu kwake!?.

Kwa haraka mashabiki wengi wakaanza kumhusisha na Diamond Platnumz maana ndiye alikuwa mpenzi wake wa mwisho kutambulika mbele ya umma ingawa uhusiano wao ulighubikwa na usiri mwingi.

Wengine walienda mbali na hata kumhusisha Majizzo lakini wakati huo tayari DJ huyo alikuwa ameshafunga ndoa na mwigizaji Elizabeth ‘Lulu’ Michael miezi mich ache tu iliyopita, hivyo hakutajwa sana kama ilivyokuwa kwa Diamond.

Ikiwa ni miaka mitano imepita tangu wimbo huo kuachiwa, hadi sasa ndio wimbo wa Hamisa ambao amepata namba za juu zaidi katika majukwaa ya kidijitali (digital streaming), rekodi ambayo pia inaubeba muziki wa Singeli. Kwanini?.

MOBE 03

Video ya wimbo huo (Ex Wangu) ambayo imeongozwa na Creator Pro, tayari imeshatazamwa YouTube zaidi ya mara milioni 13.9, ukiwa ni wimbo namba tatu wa Single kufanya vizuri katika mtandao huo kwa muda wote.

Wasanii waliomtangulia Hamisa na Seneta Kilaka ni Zuchu, Nyumba Ndogo (2021), na Rayvanny na Dulla Makabila, Miss Buza (2022), ambao ni wimbo wa kwanza wa Singeli kutazamwa YouTube mara milioni 1 ndani ya siku tatu.

Mwigizaji Hemedy PHD ambaye pia ni mshiriki wa mashindano ya uimbaji, Tusker Project Face msimu wa pili nchini Kenya mwaka 2008, alicheza uhusika katika video hiyo ya Hamisa.

MOBE 04

Lakini hiyo si mara ya kwanza kwa wawili hao kushirikiana katika kazi ya sanaa kwani hapo awali walicheza pamoja filamu, Vocha (2014) iliyotayarishwa na kampuni ya Steps Entertainment. Ikumbukwe tangu mwanzoni mwa miaka ya 2010, muziki wa Singeli ilianza kujizoelea umaarufu ukitengeneza mastaa wake kama Msaga Sumu, MC Sudi, Dulla Makabila, Man Fongo, Meja Kunta, Sholo Mwamba n.k.

Umaarufu wa Singeli uliwavutia mastaa wa Bongo Fleva kama Professor Jay, Harmonize, Rayvanny, Alikiba, Jux, na Zuchu, ambao nao kwa nyakati tofauti waliamua kutoa nyimbo za mahadhi yao na nyingi zilipokelewa vizuri.

Mtayarishaji muziki kutoka studio za Imagination Sound, Mocco Genius ambaye ametengeneza nyimbo kadhaa za Singeli, amesema Singeli ni utambulisho wa muziki wa Kitanzania na ndiyo sababu unazidi kushika kasi na kila muziki una wakati wake. 

“Kuna kipindi wasanii walikuwa wanashauriwa kuupa nguvu muziki wa Singeli kwa sababu unaona ndio muziki ambao inaibeba asili yetu na ukisikiliza hamna nchi yoyote ambayo inaupiga,” amesema.

MOBE 02

“Kwa hiyo sasa wakitokea wasanii wa Bongo Fleva wakafanya Singeli ni kwamba wanafanya muziki ambao unaweza kusikilizwa na mtu yeyote kutoka taifa lolote, kwa hiyo kwangu ni kitu kizuri na waendelee kufanya,” ameeleza Mocco.

Kwa upande wake mtayarishaji muziki kutoka ‘Combination Sound’, Man Water amesema bado Singeli sio muziki wa Tanzania kama baadhi ya watu wanavyosema kutokana unasampo aina nyingine za muziki.

“Bado naamini sio muziki wetu, yaani pale kama tumetafuta kaladha fulani na kusema ndio muziki wetu lakini tuje mpaka kwenye sampo zimetoka wapi?, ukifuatilia Singeli ni kuchukua wimbo wa mtu na kuuminya na kuunda kitu,” amesema.

Utakumbuka Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) ambazo zilianzishwa mwaka 1999 na Baraza la Sanaa Taifa (Basata), ziliijumisha Singeli katika tuzo hizo kuanzia msimu wa 2021, na hii ni kwa sababu ya ushawishi wake.