Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Walipaswa kusikika katika nyimbo hizi ila ndo hivyo...!

VIB 01

Muktasari:

  • Moja ya mambo hayo ni jinsi wanamuziki hao hufanya mabadiliko ya watu waliowashirikisha au waliopanga kuwapa nafasi hiyo, kisha baadaye kuja na mpango mwingine kama ifuatavyo.

Kuna mambo mengi huendelea nyuma ya pazia kabla ya wanamuziki wa Bongofleva kuachia nyimbo zao ambazo hutokea kuzipenda na kutuachia kumbukumbu muhimu katika maisha.

Moja ya mambo hayo ni jinsi wanamuziki hao hufanya mabadiliko ya watu waliowashirikisha au waliopanga kuwapa nafasi hiyo, kisha baadaye kuja na mpango mwingine kama ifuatavyo.


1. Matonya alipaswa kuwepo katika wimbo wa kundi la Roma na Stamina (Rostam), Now You Know (2018) ft. Khaligraph Jones, na alisharekodi wakiwa Nairobi, Kenya ila sauti yake ikaja kuondolewa dakika za mwisho kabla wimbo huo kutoka.


2. Abigail Chams tayari alisharekodi vesi yake katika wimbo wa Marioo, Love Song (2023) lakini baadaye inadaiwa ilitokea kutoelewana ndipo ikatolewa na nafasi hiyo kupewa Alikiba kutokea Kings Music.

FACT 01

3. Wimbo wa Harmonize, Kwangwaru (2018) awali alipanga kumshirikisha Davido kutokea Nigeria lakini akabadili maamuzi yake na kumshirikisha Diamond Platnumz ambaye alivutiwa na wimbo huo.

Tayari Harmonize alianza kurekodi akiwa Nigeria huku akimsubiria Davido ambaye alikuwa Marekani, ila alivyorejea Tanzania, Diamond aliupenda wimbo huo na ukawa mwanzo wa kufanya pamoja.


4. Wimbo wa Professor Jay, Nikusaidieje (2005) tayari kiitikio chake alikuwa amesharekodi Suma Lee ila baadaye wakashauriana na P-Funk Majani wamuweke Ferooz kutokana alikuwa anafanya vizuri, hivyo Ferooz akakaja na kurekodi kiitikio kingine.


5. Kundi la Wakali Kwanza linaloundwa na Joslin, Makamua na Q Jay ndio walitakiwa kusikika katika wimbo wa Fid Q, Usinikubali Haraka (2009), ila Matonya alipousikika akaupenda wimbo huo na kurekodi kiitikio, na Marco Chali akaona alichonya kinatosha.

FACT 02

6. Rayvanny alikuwepo katika wimbo wa Zuchu, Siji (2024) ila vesi yake ikachomolewa dakika za jioni kabisa kabla ngoma hiyo kutoka, huku nafasi yake ikichukuliwa na Toss wa Afrika Kusini.


7. Si mara ya kwanza kwa Rayvanny kutolewa katika wimbo, nyingine alizotolewa ni Riziki (2012) wa Tip Top Connection, Pombe Yangu (2013) wa Madee, Nitakupwerepweta (2015) wa Yamoto Band na Shikorobo (2015) wa Shetta.


8. Mwasiti alishapanga kumshirikisha Professor Jay katika wimbo wake, Hao (2007) lakini rapa huyo alikuwa amesafiri nje ya nchi. Mwasiti alimsubiri kwa muda na baadaye akashauriana na Ruge kuwa nafasi hiyo apewe Chid Benzi ambaye aliitendea haki.

FACT 03

9. Rama Dee ndiye alitakiwa kusikika kwenye kiitio cha wimbo wa Nikki Mbishi, Punchline (2011) badala ya Grace Matata ambaye amesikika pia kwenye ngoma nyingine ya Nikki, Nyakati za Mashaka (2011).

Na katika ngoma ya Nyakati za Mashaka (2011) ya Nikki Mbishi, alichoimba Grace Matata, ni sehemu ya wimbo wake ‘Nyakati’ uliobeba jina la albamu yake ya kwanza iliyotoka mwaka 2013.


10. Professor Jay ndiye aliombwa kushiriki katika wimbo wa Tundaman, Neila (2006) ila akampendekeza Chid Benzi ambaye alikuwa na ukaribu naye. Basi Chid akakubali na kuibuka Baucha Records ambapo Bob Manecky alikuwa anafanya kazi wakati huo.