Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo 10 aliyopita nayo Wema Bongofleva

Muktasari:

  • Wema, Miss Tanzania 2006, ameshiriki na kuhusishwa na mambo mengi katika muziki huo, jambo ambalo linaonyesha mchango wake wa wazi kabisa katika tasnia hiyo. Fahamu zaidi.

Katika miaka yake 20 ya umaarufu, jina la Wema Sepetu halijahusishwa na urembo, mitindo na filamu pekee, bali hata katika muziki wa Bongofleva kuna mengi yanagusa wasifu wake moja kwa moja.

Wema, Miss Tanzania 2006, ameshiriki na kuhusishwa na mambo mengi katika muziki huo, jambo ambalo linaonyesha mchango wake wa wazi kabisa katika tasnia hiyo. Fahamu zaidi.


1. Jina la Wema Sepetu limetajwa katika nyimbo zaidi ya 20 za Bongofleva, huku Diamond Platnumz akifanya hivyo mara nyingi zaidi ukilinganisha na wasanii wenzake.


2. Baadhi ya wasanii waliomtaja Wema katika nyimbo zao ni Tundaman - Sio Demu (2012), Young Killer -  Mrs Superstar (2013), Nikki Mbishi - Kill Your Self (2013) na Gosby - Wema Sepetu (2015). Rayvanny - Natafuta Kiki (2016), Fid Q -  Sumu (2016), Alikiba - Aje (2017), Aslay - Natamba (2017), Rostam - Hivi Ama Vile (2017), Joh Makini - Mchele (2019), Harmonize - Mtaje (2021), Marioo - Tomorrow (2023) na kadhalika.


3. Katika wimbo wa hayati Haitham Kim, Play Boy (2019) uliotayarishwa na Daxo Chali chini ya MJ Records, ndani yake kuna sauti ya Wema ingawa kwenye video hakuonekana kutokana alishiriki sehemu ndogo sana.


4. Video ya kwanza ya muziki kwa Lulu Diva kutokea kama video vixen ni ya wimbo wa Mirror na Barakah The Prince, Naogopa (2016), na Wema ndiye alimpa Lulu Diva nafasi hiyo kwa sababu wakati huo alikuwa akimsimamia Mirror kupitia Endless Fame Label.


5. Wema ndiye mrembo aliyetajwa mara nyingi zaidi katika nyimbo za Diamond ambazo ni Nimpende Nani (2012), Kesho (2012) na Fire (2017) akimshirikisha Tiwa Savage kutokea Nigeria.


6. Baada ya Wema kutokea katika video ya wimbo wa Diamond, Moyo Wangu (2012), ndio ulikuwa mwanzo wa msanii huyo kuwatumia wapenzi wake katika video za nyimbo zake. 


7. Kwa hiyo baada ya Wema, Diamond alifanya hivyo kwa Zari The Bosslady aliyeonekana katika video mbili za Diamond, Utanipenda (2015) na Iyena (2018) ikiwa ni sawa na Hamisa katika video za nyimbo kama Mawazo (2012) na Salome (2016).


8. Mpenzi wa Wema, Whozu ambaye ni mwanamuziki wa Bongofleva, alitoa wimbo maalum, Namleta (2026) mara baada ya Mrembo huyo kujaliwa mtoto wake wa kwanza. Wimbo huo uliotayarishwa na S2kizzy katika studio za Pluto Republic, unazungumzia kuhusu kuzaliwa kwa mtoto wao wa kiume aliyepewa jina la Ollie Oscar.


9. Whozu anaungana na wasanii wengine kama Marioo na Jux ambao miaka ya hivi karibuni wametoa nyimbo kuhusu kuzaliwa kwa watoto wao.

Marioo alitoa wimbo wake, My Daughter (2024) ambao ni maalum kwa ajili ya mtoto wake na Paula, Princess Amarah, huku Jux akitoa Thank You (2025) kwa ajili ya mtoto wake na Prisiclla, Rakeem Mkambala.

10. Licha ya uhusiano wao kuwepo kwa miaka zaidi ya mitatu, Wema hajawahi kutokea katika video rasmi yoyote ya wimbo wa mwanamuziki huyo. Hata hivyo, aliyekuwa mpenzi wa Whozu kabla ya Wema, Tunda alitokea kwenye video ya wimbo wa msanii huyo uitwao Doko (2019), ikiwa imeongozwa na Director Joowzey, na hadi sasa imetazamwa YouTube mara milioni 1.8.