Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbosso, Bonge la Dada kazi inaongea!

Muktasari:

  • Mbosso, mwanzilishi wa Khan Music, tayari ametoa albamu na EP ambazo zimefanya vizuri zikizidi kulipa jina lake umaarufu mkubwa, kitu kinachomfanya kuwa na nguvu ya ushawishi. Fahamu zaidi.

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mbosso amejijengea sifa nzuri kutokana na utunzi na uimbaji wa viwango vya juu kabisa wa nyimbo zake akigusia hasa mada za mapenzi na starehe.

Mbosso, mwanzilishi wa Khan Music, tayari ametoa albamu na EP ambazo zimefanya vizuri zikizidi kulipa jina lake umaarufu mkubwa, kitu kinachomfanya kuwa na nguvu ya ushawishi. Fahamu zaidi.


1. Nyimbo za Lava Lava na D Voice ambazo video zake zimetazamwa zaidi YouTube (most viewed) kwa muda wote, ni zile ambazo wamemshirikisha Mbosso ambazo ni Basi Tu (2021), na Tunapendana (2024).


2. Kwa mara ya kwanza Mbosso alipata umaarufu akiwa Yamoto Band baada ya kuachia wimbo wao, Ya Moto (2013) uliotengenezwa Vibe Records na Shirko na kuanzia hapo jina lake limekuwa juu kimuziki.

3. Video ya wimbo wa Mbosso, Pawa (2025) inashikilia rekodi ya kuwa wimbo wa kwanza wa Bongo Fleva ambao umetazamwa YouTube mara milioni 74 ndani ya mwaka mmoja.


4. Hadi kufikia Desemba 31, 2025, Pawa ndio ulikuwa wimbo namba moja katika orodha ya video za Bongo Fleva zilizofanya vizuri zaidi YouTube kwa mwaka huo licha ya kutoka karibia katikati ya mwaka.

Pawa ilifuatiwa na video kama Nairobi (Marioo), Tete (Marioo), Furaha (Harmonize), Me Too (Abigail Chams), Salama (Barnaba), Looking For Love (Darassa), Jirani (Jay Melody), Amanda (Zuchu) na Katam (Diamond Platnumz).


5. Akiwa ana miaka zaidi ya 10 katika muziki, Mbosso ametoa albamu moja, Definition of Love (2021) pamoja na EP mbili, Khan (2022) na Room Number 3 (2025), huku akishinda tuzo mbili za muziki Tanzania (TMA) peke yake, na moja akiwa na Yamoto Band.


6. Katika wimbo wa Mbosso, Darasa la Saba (2026)  kuna kionjo cha maneno ya Kihindi. Maneno hayo ni 'tere rireh tere sanaam:, yakiwa na maana ya 'kwa ajili yako, mpenzi wangu'.

Hata hivyo, si wimbo huo pekee ambao Mbosso ametumia lugha ya Kihindi, bali hata katika wimbo wake, Ozalima (2026) amefanya hivyo pia.

7. Mbosso ameshirikishwa na wasanii wengi wakubwa, baadhi yao ni Rayvanny (Mon Amour), Diamond Platnumz (Oka), Darassa (Looking For Love), Harmonize (Leo), Alikiba (Bhuju), Jux (Kipepeo), na Zuchu (Ashua).


8. Pawa umeweka rekodi ya kuwa wimbo wa Mbosso ambao video yake imetazamwa zaidi YouTube kwa muda wote, hivyo sasa hiyo ndio kazi yake namba moja katika mtandao huo ulioanza kufanya kazi Desemba 2015.


9. Video ya Pawa imekuja kuzipita nyingine za Mbosso kama Baikoko (2021), Hodari (2018), Tamu (2019), Nadekezwa (2018), Amepotea (2023) na Fall (2020).


10. Dansa maarufu Bongo, Queen Fraison 'Bonge la Dada', ndiye mrembo ambaye ameonekana katika video za nyimbo nyingi za Mbosso hadi sasa.

Baadhi ya hizo ni Aviola (2025), Ozalima (2026) na Oka (2022), wimbo wake Diamond Platnumz akimshirkisha Mbosso, ukipatikana katika EP yake ya kwanza, First of All (2022).