Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tumpe spesi Chidi Benz ajikusanye

Muktasari:

  • Wakasogea mbele wakakutana na majirani wengine, majirani walipoona dingi anatembea huku mtoto amekaa kwenye punda wakasema;

DINGI mmoja alikuwa na kazi ya kumpeleka mtoto wake shule, akachukua punda, akampandisha mtoto wake na yeye akapanda wakaanza safari. Wakakatiza mitaa miwili mitatu wakakutana na majirani, majirani wakasema; “Dah! Cheki yule mzee alivyo katili, yaani yeye na mwanaye wamepanda punda mmoja, si watamvunja mgongo huyo punda!” Dingi akawasikia, ili kuwaridhisha, akateremka, akamuacha mwanaye juu ya punda, yeye akawa anaongoza njia tu.

Wakasogea mbele wakakutana na majirani wengine, majirani walipoona dingi anatembea huku mtoto amekaa kwenye punda wakasema;

“Dah! Watoto wa siku hawana adabu wala huruma, yaani kweli dogo anaacha mzee kama yule atembee kwa miguu wakati yeye amepanda punda, ye si kijana, ana nguvu, kwanini asishuke atembee kwa miguu amuache mzee ndo apande punda.” Dingi akawasikia, ili kuwaridhisha akamteremsha mwanaye kisha yeye ndo akapanda punda, safari ikaendelea.

Mbele tena wakakutana na majirani wengine, walipoona Dingi kapanda punda huku mtoto anatembea wakasema; “Dah! Huyu mzee ana roho mbaya, yaani mtoto anatembea kwa miguu huku yeye amepanda punda?” Dingi akawasikia, ili kuwaridhisha akateremka, ikawa sasa yeye na mwanaye wote wanatembea kwa miguu huku wanamkokota punda, safari ikaendelea.

Mbele kidogo wakakutana na majirani wengine, walipoona Dingi na mwanaye wanatembea kwa miguu huku wanakokota punda wakasema; “Dah! Hii familia chenga kweli. Yaani watu mna punda halafu mnatembea kwa miguu? Sasa huyo punda wa nini? Wa mapambo au?” Mzee akawasikia lakini sasa hakujua cha kufanya kwa sababu alikuwa ameshamaliza machaguo yote.

Ingekuwa nawasimulia hii stori usiku chini ya mbalamwezi ningewauliza hadithi inatufundisha nini? Lakini kwa sababu tunapiga hizi stori kwa gazeti nitakwenda moja kwa moja na kusema, hadithi hii inatufundisha kwamba hakuna kitu utafanya kwenye hii dunia watu wakakosa cha kusema kuhusu kitu hicho.

Rashid Abdallah maarufu kama Chidi Benz alikuwa msanii mzuri sana aliyekamilika kila idara. Kwa bahati mbaya akateleza na kuingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya. Chidi akawa teja, akapoteza kiasi kwamba akawa anaokota makopo barabarani ili akauze ili apate dusko za kununua mihadarati. Watu tukamsema sana, maneno ya kila aina; “Kuiga umarekani kumeponza. Ushamba wa ustaa umemponza. Sijui hivi, sijui vile. Maneno kibao.”

Chidi akapambania maisha yake mara kadhaa lakini alifeli, alikuwa anapelekwa rehab lakini akitoka baada ya siku mbili tatu unamkuta tena anafanya intavyuu na online media na majibu anayotoa ni kama mtu amedata hivi.

Lakini majuzi kati Chidi ametoka rehab kwa mara nyingine tena huku akiwa na muonekano mpya kabisa. Amenawiri, amenenepa lakini pia amekuwa na tumbo kubwa sana… lakini ishu ni kwamba, wadau mitandaoni, badala angalau kwanza ya kumpongeza mshikaji wetu kwa kuvuka kiunzi cha dawa hatari — watu wanapiga kwenye mshono na kudhihaki tumbo lake; “Hilo tumbo mlikuwa mnamlisha nini huko rehab?”, “Yaani hapo hakuna mlichomsaidia, mmetoa kwenye madawa mmeenda kumuongezea tatizo la kiafya, manake hilo tumbo linaonekana la maradhi.”

Komenti za kujifanya ‘madokta’ kama hizi hazijengi. Tungempa mshikaji muda wa kujikusanya ili kwanza angalau ajiridhishe kwamba ni kweli sasa ameacha mihadarati kisha atarudi kusghulikia hayo mengine!