Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rekodi za Alikiba dhidi ya Alikiba!

ALIKIBA Pict

Muktasari:

  • Hadi sasa mwanamuziki huyo ameweka rekodi nyingi katika Bongofleva, lakini hizi ni zile ambazo ni kati ya Alikiba dhidi ya Alikiba mwenyewe. Fahamu zaidi.

MWANAMUZIKI wa Bongofleva kutokea Kings Music, Alikiba amekuwa na mwendelezo mzuri wa kufanya vizuri katika tasnia ukilinganisha na wasanii wengi ambao alitoka nao kimuziki kipindi hicho.

Hadi sasa mwanamuziki huyo ameweka rekodi nyingi katika Bongofleva, lakini hizi ni zile ambazo ni kati ya Alikiba dhidi ya Alikiba mwenyewe. Fahamu zaidi.


FAC 05

1. Tangu ameanza muziki miaka zaidi ya 20 iliyopita, tuzo kubwa ya kimataifa aliyoshinda Alikiba ni MTV Europe Music Awards (EMAs), ambapo alishinda mwaka 2016 kama Msanii Bora Afrika. Tuzo za MTV EMAs hufanyika kila mwaka katika nchi tofauti barani Ulaya, na huandaliwa na kampuni ya Paramount International Networks.


2. Alikiba ni mwanamuziki wa pili wa Bongofleva kushinda MTV EMAs akiwa ametanguliwa na Diamond Platnumz ambaye mwaka 2015 alishinda kwa mara ya kwanza akitakata katika vipengele viwili.


FAC 01

3. Hadi sasa Alikiba na Diamond ambao kila mmoja ameachia albamu tatu na Extended Playlist (EP) moja kwa kila mmoja, ndio wasanii pekee wa Bongofleva waliowahi kusinda MTV EMAs.


4. Kati ya albamu zake tatu, albamu ya mwisho ya Alikiba, Only One King (2021) ndio imefanya vizuri zaidi kwa ujumla akishinda tuzo na kutoa nyimbo nyingi maarufu. Albamu hiyo ilishinda Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) katika kipengele cha Albamu Bora ya Mwaka, huku ikitoa wimbo maarufu wa Alikiba, Utu ambo video yake imetazamwa (views) YouTube mara milioni 49.


FAC 02

5. Wimbo mrefu zaidi ambao Alikiba amewahi kuachia ni Naksh Naksh Mrembo (2006) akimshirikisha Hakeem 5. Wimbo huo uliotayarishwa na KGT na kujumuishwa kwenye albamu yake ya kwanza (Cinderella), una urefu wa dakika 5 na sekunde 19.


6. Ukimtoa mdogo wake Abdukiba, mwanamuziki aliyedumu kwa muda mrefu ndani ya lebo ya Alikiba, Kings Music, ni K2ga ambaye amefanya kazi na lebo hiyo kwa takribani miaka saba kabla ya kuondoka.


FAC 03

7. Video ya Alikiba iliyotazamwa zaidi YouTube kwa muda mfupi, ni ya wimbo wake, Mahaba (2023), ambapo ndani ya miaka mitatu imetazamwa zaidi ya mara milioni 61, na hakuna video yake nyingine yenye namba hizo.


8. Kati ya albamu tatu zake Alikiba, Only One King (2021) ndio yenye nyimbo nyingi zaidi zikiwa ni 20. Albamu ya Cinderella (2006) ina nyimbo 15, na Ali K 4Real (2009) ina nyimbo 17.


FAC 04

9. Mwanamuziki mkubwa wa kimataifa ambaye Alikiba amewahi kushirikiana naye, ni staa wa RnB kutokea Marekani, R Kelly ambaye walifanya kazi pamoja katika mradi wa One 8 uliotoa wimbo wa Hands Across The World (2010). Mbali na Alikiba, wasanii wengine waliosikika katika wimbo huo ni Amani (Kenya), Navio (Uganda), 2Face (Nigeria), 4x4 (Ghana), Fally Ipupa (DR Congo), Movaizhaleine (Gabon) na JK (Msumbiji).


10. Tukio kubwa zaidi la kimataifa ambalo Alikiba amewahi kutumbuiza, ni ufunguzi wa African Football League (AFL) uliofanyika Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, ambapo Simba SC ilicheza dhidi ya Al Ahly ya Misri hapo Oktoba 2023.