Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyimbo ambazo video zake zimetoka baada ya miaka 15

Muktasari:

  • Hata hivyo, miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia baadhi ya nyimbo hizo zikitengenezewa video, kitu ambacho kinazidi kuongeza thamani ya nyimbo hizo. Hizi ni nyimbo ambazo video zake zimetoka zaidi ya miaka 15 baadaye.

KUNA nyimbo zilizovuma katika Bongofleva miaka ya nyuma lakini wasanii wake hawakuweza kuachia video zake kwa wakati huo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ufinyo wa teknolojia na bajeti.

Hata hivyo, miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia baadhi ya nyimbo hizo zikitengenezewa video, kitu ambacho kinazidi kuongeza thamani ya nyimbo hizo. Hizi ni nyimbo ambazo video zake zimetoka zaidi ya miaka 15 baadaye.


1. Ferooz - Boss (2004): Video 2024

Ni kati ya nyimbo zilizoibeba vizuri albamu yake ya kwanza, Safari (2005) chini ya Bongo Records. Wimbo huo aliyouandika akiwa kidato cha sita umetayarishwa na P-Funk Majani kwa kushirikiana na Bizman.

Video yake ilikuja kutoka Oktoba 2024 ikiwa ni miaka 20 tangu kuachiwa kwa wimbo huo. Katika mtandao wa YouTube umeshatazamwa (views) mara milioni 2.3.

Hata hiyo, ni Ferooz na Juma Nature ndio waliotokea katika video hiyo, huku Solo Thang ambaye naye alishirikishwa akishindwa kushuti kwa sababu hakuwepo nchini, na kuna matakwa yake alitaka yatimizwe kwanza.


2. Mad Ice - Baby Gal (2003): Video 2025

Mwanamuziki huyu kutokea Uganda alirekodi wimbo huu nchini Tanzania chini ya utayarishaji wake Miikka 'Mwamba' Kari kutokea Finland, moja ya watayarishaji wenye mchango mkubwa katika kuikuza Bongofleva.

Wimbo huo ulifanya vizuri sana Bongo na kwao Uganda, na ndio uliobeba jina la albamu ya kwanza yake Mad Ice, ambayo ilikuwa na nyimbo 14.

Hatimaye Oktoba 2025, ndipo ikaachiwa video yake ikiwa ni miaka 22 tangu wimbo ulipotoka. Video hiyo ambayo imeongozwa na Simon SPK Films, imeshatazamwa YouTube zaidi ya mara 880,000.


3. Mandojo na Domokaya - Nikupe Nini (2005): Video 2020

Ndio wimbo ukiowatambulisha wanamuziki hao katika Bongofleva ikiwa ni baada ya kukutana na P-Funk Majani mkoani Arusha katika ziara (tour) ya albamu ya pili ya Juma Nature, Ugali (2003).

Majani alivutiwa na uwezo wao ndipo akawakaribisha Bongo Records ambapo walirekodi albamu yao, Taswira (2005) ambayo ilikuwa na nyimbo kama Nikupe Nini, Digi, Niaje na Wanok Nok wakimshirikisha Lady Jaydee.

Miaka 17 baadaye, ndipo Mandojo na Domokaya wakaachia video ya wimbo wao 'Nikupe Nini' ambayo ilitoka Oktoba 2020 ikiongozwa na Director Ez Brown, na tayari YouTube imeshatazamwa mara milioni 1.2.


4. Juma Nature - Mtoto Iddi (2005): Video 2024

Septemba 2024, ndipo Juma Nature aliachia video ya wimbo wake, Mtoto Iddi (2005) ambao umetayarishwa na P-Funk Majani. Video ilikuja miaka 19 tangu wimbo huo ulipojizolea umaarufu kwa mashabiki.

Video hii pamoja na ile ya Ferooz (Safari), ulikuwa ni mradi wa Bongo Records ambao kwa sehemu ulilenga kutangaza bidhaa (product placement) fulani ndani yake.

Ikumbukwe, Mtoto Iddi ni wimbo unaopatikana katika albamu ya tatu yake Juma Nature, Ubinadamu Kazi (2005), ambayo pia ilikuwa na ngoma yake maarufu hadi leo, Hakuna Kulala.


5. Z Anto - Mpenzi Jini (2007): Video 2026

Ni kati ya nyimbo nane zinazopatikana katika albamu ya kwanza ya Z Anto, Binti Kiziwi (2007) iliyotoka chini ya usimamizi wa Tip Top Connection, na kwa sehemu kubwa ulichangia mauzo ya albamu hiyo.

Miaka 19 baadaye, ndipo Z Anto akaachia video ya wimbo 'Mpenzi Jini' ambayo ilitoka Septemba 2026 ikiwa imeongozwa na Director Trust. YouTube imeshatazamwa mara 646,000.

Ikumbukwe katika albamu hiyo, Z Anto aliachia video ya wimbo mmoja tu, ambao ni Binti Kiziwi, na mrembo aliyetokea katika video hiyo ameonekana pia katika video nyingine ya msanii huyo, Nichape (2020).