Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Prodyuza wa Ditto atoa ushahidi wa saa tatu mahakamani

Lameck Ditto (mwenye kofia) akiingia kwenye moja ya court katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kusikiliza kesi yake ya madai dhidi ya Multi Choice Tanzania.

Muktasari:

  • Maungu aliyetoa ushahidi huo kuanzia saa 4:45 asubuhi hadi saa 7:47 mchana ni miongoni mwa mashahidi katika kesi ya mwanamuziki huyo ambaye jina lake halisi ni Dotto Bernard Bwakeya dhidi ya MultiChoice Tanzania Limited ambayo anadai imetumia wimbo wake wa Nchi Yangu katika matangazo yao ya biashara kipindi cha Kampeni ya Afcon 2019 bila ridhaa yake.

Emmanuel Maungu ambaye ni prodyuza wa wimbo wa Nchi Yangu wa mwanamuziki, Lameck Ditto ametoa ushahidi leo Alhamisi kwa muda wa saa tatu akielezea mahakama namna alivyotengeneza wimbo huo mwaka 2017.

Maungu aliyetoa ushahidi huo kuanzia saa 4:45 asubuhi hadi saa 7:47 mchana ni miongoni mwa mashahidi katika kesi ya mwanamuziki huyo ambaye jina lake halisi ni Dotto Bernard Bwakeya dhidi ya MultiChoice Tanzania Limited ambayo anadai imetumia wimbo wake wa Nchi Yangu katika matangazo yao ya biashara kipindi cha Kampeni ya Afcon 2019 bila ridhaa yake.


Mwanamuziki huyo alifungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akiiomba iamuru kampuni ya MultChoice Tanzania Limited maarufu DSTV imlipe fidia ya Sh 6 Bilioni kwa kutumia wimbo wa Nchi Yangu aliodai ni wake kwenye matangazo yao ya biashara bila ridhaa yake.


Pia ameiomba Mahakama iamuru alipwe Sh 200 Milioni kutokana na madhara ya jumla, pia alipwe riba ya asilimia 25 tangu siku alipofungua shauri hilo.


Leo kesi hiyo iliendelea kusikilizwa kwa mashahidi wa Ditto mbele ya jaji, Salma Maghimbi .


Prodyuza wa Wimbo huo, Emmanuel Maungu aliieleza Mahakama kwamba aliutengeza wimbo huo mwaka 2017 na alipigiwa simu na Ditto mwaka 2019 kumuuliza endapo yeye (Maungu) ndiye alitoa idhini kwa DSTV kuutumia kwenye matangazo yao.


Akitoa ushahidi wake wa maandishi, alidai alimwambia Ditto sio yeye ndipi akamtumia links kuona walivyoutumia kwenye matangazo hayo.


Alisema, alianza kutengeneza wimbo wa Nchi Yangu uliombwa na Ditto pekee, kisha akafanya remix ya wimbo huo huo wa Ditto na kushirikishwa wasanii wengine baadhi baada ya Ditto kuombwa ifanyike Remix kwa ajili ya tamasha la urithi.


Baada ya kutoa ushahidi wake, Wakili wa DSTV, Thomas Mathias alimuuliza shahidi huyo.


Wakili:Nikisema kwamba wewe ndiye uliyeingiza biti kwenye wimbo wa Nchi Yangu niko sahihi?


Shahidi:Niliingiza sauti


Wakili:Unafahamu masuala ya haki miliki?


Shahidi:Nazijua za kwangu kama producer


Wakili:Tutajie haki kadhaa kama producer


Shahidi:Ni kuwa na umiliki sehemu ya muziki nilioingiza


Wakili:Unataka kuiambia Mahakama katika wimbo wa Nchi Yangu una haki?


Shahidi:Hayo ni makubaliano yangu na Ditto.


Wakili:Ditto aliiambia Mahakama  hakuwahi kuwalipa wasanii wote walioimba kwenye huo wimbo ni sahihi


Shahidi:Ndio


Wakili:Kwa kuwa hakukulipa, zile haki bado ziko kwako?


Shahidi:Hayo ni makubaliano yangu na Dito


Wakili:Unaiambia Mahakama hii mlishindwa kuendelea na production sababu Mult Choice  kuitumia huo wimbo? unafahamu kama ulikuwa published na Clouds Media Group mwaka 2018?.


Shahidi:Ndio


Wakili:Soma hii email ni ya lini, ilitoka kwa nani na inakwenda kwa nani? (akimpa nyaraka)


Shahidi:Sio yangu ukisema niitambue!.


Wakili:Nimesema usome


Shahidi:Imetoka kwa Emmilian Mallya kwenda kwa Ditto ni forwaded meseji  ilitoka kwa Ruge Mutahaba tarehe 27 Agosti, 2018.


Wakili:Soma content.


Shahidi:Alisoma


Wakili:Umesema ulikuwa published mwaka 2018 na All Stars ni sahihi?


Shahudi:Ndiyo


Wakili:Nikisema kabla sehemu ya wimbo huo haujatumika na DSTV tayari ulishakuwa published muda mrefu ni sahihi?


Shahidi:Ndio


Shahidi:Ushahidi wa kwamba mlishindwa kuendelea na albamu sio kweli?


Shahidi:Ni kweli tulishindwa kuendelea


Wakili:Mheshimiwa naomba kama nitapata youtube chanell ya Clouds


Wakili Ditto, Ally Hamza alisema links zipo kwenye flash, zikaonyeshwa kwenye skirini na wakili wa DSTV kuendelea.


Wakili:Katika tasnia ya muziki unaweza kukubaliana na mimi unaweza kuwa mtunzi lakini sio mmiliki?


Shahidi:inawezekana


Wakili:Pia inaweza kuandika lakini sio kumliki?


Shahidi:Inategemea kama umeuza haki miliki.


Wakili:Usiseme inategemea, sema inawezekana au haiwezekani.


Shahidi:Inawezekana


Wakili:Kwa tafsiri rahisi unaweza kuwa mwandishi, lakini sio mmliki?


Shahidi:Inategemea kama uliuza, ulikubaliana na mmiliki kama uliuza hiyo haki miliki


Wakili:Katika hizi media unafahamu kama huwezi kupublish content kama huna haki miliki?


Shahidi:Hilo Sijui, lakini kwa mujibu wa email wimbo uliombwa kutumika ( akirudi kusoma email)


Wakili:Kwenye hiyo email kuna sehemu uliombwa?


Shahidi:Hii email hakuomba, ila Ruge alimuomba Ditto utumike kwenye urithi Festival, lakini kwenye email Ruge alikuwa akitoa maelekezo huko kwa watu wake.


Wakili:Ditto hakuleta hayo makubaluano, wewe umeyaleta hapa Mahakamani?


Shahidi:Hayo ni yeye (Ditto) na Ruge, alipokuja kwangu kuuomba nilimuuliza mmekubaliana akasema ndiyo, hivyo sijui walikubaliana kwa namna gani?.


Wakili:Asante mheshimiwa, tunaomba tufungulie akaunti ya Ditto ya Youtube, (baada ya  akaunti kufunguliwa, akaendelea).


Wakili:Ionyeshe Mahakama Wimbo wa Nchi Yangu ya All Stars kwenye akaunti ya Ditto.


Shahidi:Hapo haupo


Wakili mwingine wa DSTV, alimuuliza shahidi


Wakili:Nitakuwa niko sahihi kwamba ulisema wimbo huu una version mbili?


Shahidi:Ndio


Wakili:Ni upi ulitumika na Dstv?


Shahidi:Nchi yangu version ya pili ulitumika


Wakili:Hiyo iliimbwa na nani?


Shahidi:Uliimbwa na Ditto kwa kushirikiana na wasanii wengine.


Wakili:Unaweza kuwataja?


Shahidi:Ndio ila siwezi wote, sababu ni muda mrefu, lakini ni Joel Lwanga, J Melody, Jux, Nandy, Lameck Ditto mwenyewe, kundi la Weusi na vijana wengine walikuwa wanatoka chuo sio rahisi kuwakumbuka.


Wakili:Je kule Cosota ni wimbo upi ulisajiliwa


Shahidi:Nchi Yangu


Wakili:Version ipi?


Shahidi:Hakuna version, mfano Tanzania umeimbwa na watu wa ngapi? Mwenye orijino version ndiye ameandika.


Wakili:Jibu swali


Shahidi:Wimbo wa Nchi Yangu ndio ulioandikishwa Cosota.


Wakili:Mheshimiwa Nitaomba sasa ile Version anayomiliki Ditto (ikawekwa).


Wakili:Inasema Lameck Ditto-Nchi Yangu Official Audio
Naomba niambie ilikuwa  published lini


Shahidi:Januari 10, 2019


WakiliBado unaendelea kushikilia,  wimbo huu wakati unakwenda kusajiliwa haukuwa kwenye domain media?


Shahidi: Haikuwa na mantiki yeye (Ditto) kukàa nao wakati tayari ninyi mmeshautumia.


Wakili: Nitakuwa niko sahihi nikisema huo wimbo ilibidi usitoke kwa kuwa DSTV walikwishautumia ni kweli?


Shahidi:Sahihi


Wakili:Unakubaliana na mimi wimbo uliotumika sio uliosajiliwa na Cosota?


Shahidi:Hapana


Unavyodhani ni wimbo upi ulitumiwa na DSTV


Shahidi:Nchi yangu


Wakili:Version ipi?


Shahidi:Ya pili


Wakili:Unakubaliana huu wimbo ambao ni wa Nchi Yangu All Stars haupo kwenye machapisho ya Ditto?


Shahidi:Hizo ni chaneli zake mwenyewe Ditto siwezi kujua, zingekuwa zangu ningejua.


Wakili:Ulijuaje kama ulirushwa DSTV


Shahidi:Ditto alinipigia simu kuniuliza kama nimetoa idhini, sababu tulikubaliana usitoke bila idhini yake


Wakili:Utakubaliana na mimi, aliyekuwa anasambaza wimbo huu ni marehemu Ruge Mutahaba?.


Shahidi:Sikubaliani na wewe


Kesi hiyo itaendelea tena kesho Ijumaa, Machi 22 Mahakama Kuu, Ditto akiwakilishwa na mawakili wawili,  Elizabeth Mlemeta na Ally Hamza.