Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanamuziki Bongo waliopata watoto pamoja!

JIACHIE Pict

Muktasari:

  • Kuna orodha ndefu tu ya wanamuziki wa Bongo Fleva ambao katika ndoa au uhusiano wao walipata mtoto au watoto.
  • Hawa ni wachache kati yao, kuanzia Marlaw, mzee wa kupiga honi barabarani akimuwahi Besta, hadi Zuchu, kiboko ya vigagura wanaomnyemelea mumewe Diamond ambaye pia ni bosi wake kimuziki.

Kwa sasa Zuchu na Diamond Platnumz wameteka mazungumzo mtandaoni baada ya kujaliwa mtoto wao wa kwanza, lakini hawa si wanamuziki pekee wa Bongo Fleva waliofanya hivyo.

Kuna orodha ndefu tu ya wanamuziki wa Bongo Fleva ambao katika ndoa au uhusiano wao walipata mtoto au watoto.

Hawa ni wachache kati yao, kuanzia Marlaw, mzee wa kupiga honi barabarani akimuwahi Besta, hadi Zuchu, kiboko ya vigagura wanaomnyemelea mumewe Diamond ambaye pia ni bosi wake kimuziki.

JIACH 01

BESTA & MARLAW

Mwaka 2019, Marlaw alisema katika ndoa yake na Besta tayari walikuwa wamejaliwa kupata watoto watano, idadi ambayo bado haijajulikana kama imeongezea au laah?

Besta aliyetamba na wimbo wake, Baby Boy (2006) aliyorekodi akiwa masomoni Uganda, alifunga ndoa na Marlaw mwaka 2011.

Hivyo wakati huo wote walikuwa wanamuziki wenye majina huku Marlaw akiwa tayari ametoa albamu zake mbili, Bembeleza (2007) na Bidii (2009) ambazo zilifanya vizuri.

JIACH 02

AIKA & NAHREEL

Wawili hawa wamekuwa pamoja tangu mwaka 2008 wakisoma Punjab College nchini India,  pia walianza kushirikiana katika muziki ingawa kundi la Navy Kenzo lilikuja kuanzishwa mwaka 2013.

Navy Kenzo waliotamba kupitia nyimbo zao kama Game (2015), Kamatia Chini (2015) na Katika (2018), tayari amejaliwa kupata watoto wawili wa kiume, Gold (2017) na Jamaika (2019).

Kwa sasa wanajitambulisha kama Aika na Nahreel na si Navy Kenzo, huku wakiwa wameshatoa albamu tatu, AIM (Above Inna Minute) (2016), Story Of The African Mob (2020) na Most People Want This (2023).

JIACH 03

ABELA & IZZO BIZNESS

Mwaka 2016, Izzo Bizness na Abela, mwimbaji mwenye makazi yake nchini Marekani lakini akiwa na asili ya Bukoba, Tanzania, walianza kufanya kazi pamoja na wengi waliwatabiria kufika mbali kimuziki.

Baadaye walianzisha kundi lao, The Amazing ambapo wimbo wao wa kwanza kuachia kama kundi uliitwa Dangerous Boy (2018) ukitayarishwa na Dupy, huku video ikiongozwa Nick Dizzo.

Kipindi wakifanya kazi pamoja ilidaiwa walikuwa na uhusiano ila mara nyingi walikanusha, lakini baada ya Abela kujifungua watoto pacha hapo Aprili 2018 akiwa Marekani, ndipo ukapatikana uthibitisho kuwa wawili hao walikuwa na uhusiano. 

JIACH 04

RUBY & KUSAH

Waimbaji hawa walianza kufanya muziki pamoja kama wanamuziki baada ya Kusah kuomba kujitolea kumwandikia Ruby nyimbo, lakini baadaye wakaja kuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Mwaka 2019, Ruby na Kusah walijaliwa kupata mtoto akiwa ni wa kwanza kwa wote wawili. Hata hivyo, walikuja kuachana na Kusah alienda kuwa na mwigizaji Aunty Ezekiel ambaye tayari wana watoto wawili kwa sasa.

Ikumbukwe kipindi cha uhusiano wao walishirikiana katika nyimbo tatu, Chelewa (2018), Kelele(2019) na Nadondosha (2019), huku Kusah akiandika wimbo maarufu wa Ruby, Ntade (2018) ambao ulifanya vizuri.

JIACH 05

NANDY & BILLNASS

Takribani mwezi mmoja baada ya kufunga ndoa, ndipo Nandy na Billnass walijaliwa mtoto wao wa kwanza, Naya ambaye alizaliwa mnamo Agosti 2020, ikiwa ni miaka minne tangu walipokutana kwa mara ya kwanza.

Mwaka mmoja baadaye, ndipo sura ya mtoto wao ilionekana katika mitandao ya kijamii na anafuatiliwa na watu wengi akiwa na wafuasi zaidi ya 839,000 katika ukurasa wake wa Instagram.

Billnass na Nandy ambao wameshirikiana katika nyimbo kama Bugana (2019), Do Me (2020), Party (2021), Bye (2022) na Hallo (2026), ni moja ya 'kapo' zenye utulivu mkubwa hapa Bongo, hawatumii uhusiano wao kufanya drama.

JIACH 06

ZUCHU & DIAMOND PLATNUMZ

Ikiwa ni mwaka mmoja na miezi miwili baada ya kutangaza kufunga ndoa, ndipo Zuchu na Diamond wanamkaribisha mtoto wao wa kwanza katika familia yao. Mtoto huyo wa kike bado hajapewa jina ingawa mwanzo ilisemekana ataitwa Sanura.

Tetesi za uhusiano wao zilikuwepo tangu mwaka 2020 na Diamond alimsaini Zuchu katika lebo yake ya WCB Wasafi, ingawa mara zote walikwepa kuthibitisha ukweli wa jambo hilo.

Mastaa hao walioshirikiana katika nyimbo tano - Litawachoma (2020), Cheche (2020), Mtasubiri (2022), Raha (2024) na Inama (2025), walitangaza kuzaliwa kwa mtoto wao hapo Agosti 2 kupitia post ya pamoja katika mtandao wa Instagram.