Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwani familia ya Diamond Platnumz inamtaka nani?

FAMILIA Pict


Kwa miaka mingi, jina la msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz limeendelea kutawala vichwa vya habari. Si kwa mafanikio yake ya muziki pekee, bali pia kwa maisha yake ya uhusiano na wanawake tofauti.


Wanawake wengi wamehusishwa na Diamond kwa nyakati tofauti na kuacha maswali mengi ya nani hasa ndiye atakuwa mama watoto wa msanii huyo ambaye amejizpolea umaarufu ndani na nje ya Tanzania akiibeba Bongo Fleva mabegani mwake.


Alianza na uhusiano na mastaa wa Bongo kwa wasanii wa kike kuhusishwa naye huku wengine wakionekana kumpa umaarufu 'kiki' na wengine kufikia mbali na kuzaa nao.

Ni katika harakati zake hizo za kimuziki, umaarufu ulimfanya atoke kimapenzi na hadi wanawake kutoka nje ya nchi na kuzidi kujulikana, lakini hakuna aliyejua ni nani hasa atakuwa mkewe kama walivyotabiri kwa kila aliyekuwa naye.

Hata hivyo, linaloacha maswali ni nani hasa ataingia katika familia ya nyota huyo baada ya sintofahamu zilizotokea kwa kila aliyefika kwao.

Inaelezwa baadhi yao wamezaa naye lakini wakifika katika familia hiyo kumekuwa na maelewano duni yaliyosababisha waishie njiani na inatajwa mara nyingi ni kutokana na kutoelewana na baadhi ya watu wa familia yake, hususan mama yake Sanura Kassim maarufu kama Mama Dangote na wakati mwingine dada yake Esma Platnumz.


Je, ni bahati mbaya?

Kwani familia hiyo inamtaka nani hasa? Hili ndiyo swali ambalo wengi wanajiuliza baada ya orodha ya wanawake walioingia na kutoka kuwa ndefu. Hawa hapa walioishia njiani.

FAMI 04

Zari The Boss Lady (2014–2018)

Diamond alianza uhusiano na mfanyabiashara kutoka Uganda, Zarina Hassan maarufu Zari The Boss Lady mwaka 2014. Wawili hao walipata watoto wawili, Latifah Dangote (Princess Tiffah) mwaka 2015 na Prince Nillan mwaka 2016.

Katika miaka ya mwanzo ya uhusiano wao, Zari alionekana kuwa karibu na familia ya Diamond. Mara kadhaa walionekana pamoja kwenye sherehe za kifamilia na shughuli mbalimbali.

Hata hivyo, baada ya wawili hao kutengana mwaka 2018, hali ilibadilika. Kulikuwa na nyakati za vijembe mitandaoni na taarifa mbalimbali zilizoripotiwa kuhusu tofauti za kimtazamo kati ya pande hizo, ingawa baadaye uhusiano wa Zari na Diamond ulitulia kwa masilahi ya malezi ya watoto wao. Hata hivyo, hakukubalika kuingia mjengoni.

FAMI 02

Hamisa Mobetto (2017)

Ndiye aliyefungua ukurasa mwingine wa mjadala baada ya kuthibitishwa amezaa mtoto wa Diamond, Dylan Abdul Naseeb.

Katika mahojiano mbalimbali yaliyowahi kuripotiwa na vyombo vya habari, Hamisa alidai alikuwa hana maelewano mazuri na Mama Dangote, akieleza kilichomuumiza zaidi ni kile alichodai mjukuu wake Dylan alikuwa akitengwa.

Kauli hizo ziliibua mjadala mkubwa nchini, huku mashabiki wakigawanyika katika mitazamo tofauti.

Ingawa familia ya Diamond imewahi kujibu baadhi ya tuhuma hizo kwa nyakati tofauti, mjadala huo uliendelea kwa muda mrefu na ukabaki kuwa moja ya visa vilivyozungumziwa zaidi kwenye burudani za Tanzania. Baada ya hapo kila mmoja aliendelea na maisha yake na kwa sasa Hamisa ametulia kwa nyota wa zamani wa Yanga Stephanie Aziz Ki baada ya kufunga ndoa.

FAMI 02 (1)

Tanasha Donna (2018–2020)

Baada ya kuachana na Zari, Diamond alianza uhusiano na mtangazaji na mwanamuziki kutoka Kenya, Tanasha Donna. Mwaka 2019 walipata mtoto wao wa kiume, Naseeb Junior (NJ).

Baada ya kuvunjika kwa uhusiano huo mwaka 2020, Tanasha aliwahi kueleza kwenye mahojiano kuwa moja ya changamoto alizokutana nazo ilikuwa kutokuwa na maelewano mazuri na Mama Dangote, akidai familia na baadhi ya watu wa karibu wa Diamond walikuwa wanaingilia uhusiano wao. Kauli hizo ziliripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari na kuzua mjadala mpana mtandaoni.

FAMI 01

Zuchu (2021–2026)

Mahusiano ya Diamond na Zuchu ndiyo yaliyodumu kwa muda mrefu zaidi baada ya Zari na ndiyo yaliyokuwa yakifuatiliwa kwa karibu zaidi.

Katika kipindi chote cha uhusiano wao, mara kadhaa kulizuka uvumi wa kutokuelewana kati ya familia za pande hizo, huku Mama Dangote na mama mzazi wa Zuchu, Khadija Kopa, wakitajwa kwenye mijadala ya mitandaoni. Hata hivyo, baadhi ya madai hayo yalikanushwa na wahusika.

Mwaka 2025, baada ya Diamond kuweka wazi alikuwa tayari amefunga ndoa na Zuchu, Mama Dangote alizungumza hadharani akisema watu walipaswa kufurahia hatua hiyo badala ya kuendelea na mijadala kuhusu maisha binafsi ya mwanawe. Kauli yake ilitafsiriwa na wengi kama ishara ya kumuunga mkono Zuchu na ndoa hiyo.


FAMI 05

Je, familia inamtaka nani?

Hili ndilo swali ambalo limeendelea kuulizwa na mashabiki kwa miaka mingi.

Kwa upande mmoja, kila mwanamke aliyekuwa na uhusiano mkubwa na Diamond amewahi, kwa namna moja au nyingine, kuhusishwa na tofauti na familia yake. Kwa upande mwingine, hakuna ushahidi wa wazi unaothibitisha familia hiyo imekuwa ikipinga kila mwanamke anayekuwa karibu na msanii huyo.

Wachambuzi wa burudani wanaamini umaarufu mkubwa wa Diamond unafanya kila tofauti ndogo ya kifamilia kuonekana kubwa zaidi mbele ya umma. Wengine wanaona Mama Dangote ni mzazi anayelinda masilahi ya mwanawe, huku wengine wakiamini ushawishi wa familia katika mahusiano ya Diamond umekuwa ukichangia migogoro inayojitokeza.

Jambo lisilopingika ni Diamond amezaa na wanawake watatu maarufu: Zari The Boss Lady ambaye amezaa naye Princess Tiffah na Prince Nillan, Hamisa Mobetto ambaye amezaa naye Dylan Abdul Naseeb na Tanasha Donna ambaye amezaa naye Naseeb Junior. Baadaye, Diamond alitangaza kuwa amefunga ndoa na Zuchu, hatua iliyofungua ukurasa mpya katika maisha yake ya kimapenzi na ni juzi tu wametangaza kumpata mtoto wao wa kwanza baada ya ndoa yao.


Hitimisho

Historia ya mahusiano ya Diamond Platnumz inaonyesha kuwa karibu kila uhusiano wake mkubwa umewahi kuambatana na mijadala kuhusu nafasi ya familia yake.

Hata hivyo, hadi sasa hakuna ushahidi wa kuthibitisha familia hiyo humkataa kila mwanamke anayekuwa kwenye maisha ya Diamond. Kilichopo ni mlolongo wa matukio, kauli za wahusika na tafsiri za mashabiki ambazo zimeendelea kujenga simulizi hilo kwa miaka mingi.

Swali linaendelea kubaki palepale: "Kwani familia ya Diamond Platnumz inamtaka nani?"