Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pacome awavuruga mastaa Bongo Movie

PACOME Pict

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua amewavuruga baadhi ya mastaa wa Bongo Movie kutokana na boli alilotembeza msimu huu akiiwezesha timu anayoitumikia kutwaa taji la nne mfululizo la Ligi Kuu Bara, wakitaka aendelee kukipiga Jangwani ili wapate burudani zaidi.


Pacome anayeitumikia Yanga kwa msimu wa pili, amemaliza msimu akiwa na mabao 12 na asisti 10, ikiwamo katika Dabi ya Kariakoo walipoilaza Simba kwa mabao 2-0 akifunga bao kwa penalti na kumsetia Clement Mzize aliyefunga bao la pili na kuipa timu hiyo ubingwa wa 31 wa Ligi hiyo.


Kutokana na kiwango kikubwa alichokionyesha nyota huyo raia wa Ivory Coast, imewafanya baadhi ya mastaa wa Bongo Movie kumzungumzia na kutaka aendelee kusalia nchini ili kuwapa burudani na kuiwezesha Yanga kuendelea kutamba nchini na anga za kimataifa.

Baadhi ya mastaa hao, Wema Sepetu, Davina, Dora wa Jua Kali, Caren Simba na Kajala kwa nyakati tofauti wamepiga stori na Mwanaspoti na kusema wamefurahishwa na uwezo wa Pacome aliuonyesha kwenye mechi ya Simba na Yanga ya kumalizia msimu wa 2024-2025.

Hata hivyo, hii sio mara ya kwanza kwa wasanii hao kutamka kumkubali Pacome kwa kuwakosha kutokana na aina yake ya uchezaji uwanjani, lakini Wema alisema amefurahishwa na ushindi wa Yanga japo hakuweza kwenda uwanjani sababu alikuwa ziarani mkoani, lakini alivurungwa na uchezaji wa Pacome alipokuwa uwanjani.

“Sikuweza tu kwenda uwanjani lakini nilibahatika kuangalia mpira kupitia TV na niliona uwezo wa Pacome alivyokuwa anacheza alivyofunga bao na kutoa pasi iliyozaa la pili na alinivuruga sana nikasema hapa ushindi Yanga ni lazima,” alisema Wema, huku Caren Simba akisema; “Nikiwaambia hakuna kama Pacome naanza kuzushiwa ishu za mapenzi, ukweli mechi ya Simba na Yanga ya kumalizia Ligi Kuu, wakati Pacome amepewa ile kadi ya njano, alinivuruga sana. Nilikuwa naombea asifanye tena kosa akalambwa nyekundu, kwani ni mchezaji muhimu mno.”

Kwa upande wa Dora wa Jua Kali alisema; “Pacha wangu Pacome amejua kuwanyoosha wapinzani wetu, anatumia akili jinsi ya kutoa pasi na kutengeneza mashambulizi, lakini anaweka nywele blichi kama ninavyoweka mimi ndio maana namuita pacha, kwa kweli ananisuuza sana roho yangu.”

Kajala Masanja alisema; “Pacome ananivuruga sana pale anapokuwa anaanzishwa kwenye mechi, anatumia muda mwingi kuiangalia, anajua na kufanya dhidi ya wapinzani, anajituma, huo ndio ubora wa staa huyu, natamani msimu ujao aendelee kuichezea Yanga.”

Staa mwingine na shabiki mkubwa wa Yanga, Davina alisema; “Sio lazima niwaangalie waigizaji wenzangu ndipo nijifunze vitu muhimu, bali anayefanya kazi nje na ninayoifanya, najifunza ili niwe bora zaidi, hivyo Pacome huwa ananikosha sana akiwa uwanjani ila mechi yetu dhidi ya Simba alizidi kukivuruga alipofunga bao la kutoa pasi, ila ile kadi ya njano, ilinipa wasiwasi juu ya watani wetu.”


Davina aliongeza; “Pacome bado tunamihitaji sana Yanga asiondoke kwanza bado tuna kazi naye wananchi, ni mmoja ya nyota walioibeba timu msimu huu kwa kiwango alichonacho.”

Pacome alitua Jangwani msimu uliopita akitokea Asec Mimosas ya Ivory Coast na amekuwa na kiwango bora akishirikiana na wenzake kuifanya Yanga itishe katika michuano ya ndani na ile ya CAF ameiwezesha timu hiyo kutetea taji la Ligi Kuu.

Usiku wa jana kiungo mshambuliaji huyo na wenzake walikuwa uwanjani katika mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Singida Black Stars iliyopigwa visiwani Zanzibar.