Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyuma ya fujo za Lamar kuna Whitney

Muktasari:

  • Kwanza ni kushinda tuzo tano za Grammy na kumfanya kufikisha 22, kisha wiki inayofuatia anatumbuiza Shoo ya Super Bowl ambayo FoxSports wanaripoti ilivutia watazamaji milioni 126 ikiwa ni ongezeko la asilia 2 kutoka msimu uliopita. 

RAPA wa Marekani, Kendrick Lamar, 37, amefanya sana fujo katika ulimwengu wa muziki wiki hizi mbili akigonga vichwa vya habari kila kona ya dunia kufuatia matukio mawili makubwa yaliyoacha alama muhimu katika kazi yake.

Kwanza ni kushinda tuzo tano za Grammy na kumfanya kufikisha 22, kisha wiki inayofuatia anatumbuiza Shoo ya Super Bowl ambayo FoxSports wanaripoti ilivutia watazamaji milioni 126 ikiwa ni ongezeko la asilia 2 kutoka msimu uliopita.  Hata hivyo, Lamar anayezidi kutikisa na albamu yake ya sita, GNX (2024), nyuma wa mfulululizo wa mafanikio yake ya hivi karibuni kimuziki kuna binadamu mmoja anaiyeitwa Whitney Alford.

Rapa huyo alitambulika zaidi kupitia albamu ya pili, Good Kid, M.A.A.D City (2012) ikiwa ni baada ya kurekodi na Dr Dre chini ya Aftermath Entertainment, na sasa Billboard na Vibe wanamtaja kama rapa bora namba mbili duniani kwa muda wote. Katika tuzo za 67 za Grammy 2025 zilizotolewa Februari 2 huko Los Angeles, Lamar aliweka rekodi kupitia wimbo wake, Not Like Us (2024) ulioshinda tuzo tano ukiwa wa kwanza wa Hip Hop kufanya hivyo katika Grammy.            Halafu unajua nini?, Lamar anahitaji kushinda tuzo nne tu ili kuweka rekodi kama msanii wa Hip Hop aliyeshinda Grammy mara nyingi zaidi kwa muda wote akimpiku Kanye West mwenye 24 na Jay Z mwenye 25 ambaye ndiye kinara hadi sasa.

Albamu yake, GNX (2024) ambayo ilitoka Novemba 22 ikiwa tayari muda wa kuwasilisha kazi kwa Grammy 2025 umeshapita, ina nafasi ya kuwania Grammy 2026, na hapo ndipo inatazamiwa huwenda akampiku Kanye West kuifikia rekodi ya Jay Z au kuivunja.

Hilo linawezekana maana albamu hiyo bado inafanya vizuri, mathalani kwa mujibu wa Top Of The Charts, inakadiriwa kuwa ndani ya wiki moja tangu kuachiwa kwake, ilisikilizwa (streams) mtandaoni kati ya mara milioni 350 hadi 400.

Hiyo iliifanya kuwa albamu ya Hip Hop iliyosikilizwa zaidi ndani ya wiki moja kwa mwaka 2024, sawa na ile ya Drake, For All the Dogs (2023) ambayo ilisikilizwa mara milioni 514 pindi ilipotoka Oktoba 6, 2023.  Mafanikio hayo yalikuja mwezi mmoja baada ya Lamar kushinda tuzo nane za BET Hip Hop 2024 akiwa ndiye msanii aliyefanya vizuri zaidi, huku wimbo wake maarufu hadi sasa, Not Like Us (2024) ukishinda vipengele vitatu.

Wimbo huo, Not Like Us (2024) uliotoka kama diss kwa Drake, umeteka mazungumzo mtandaoni baada ya kuutumbuiza katika Super Bowl hapo Februari 9, huku Serena Williams, mchezaji mstaafu wa tenesi akicheza naye jukwaani.

Kucheza na Serena kumekuwa gumzo kutokana mrembo huyo aliwahi kuhusishwa kuwa na uhusiano na Drake, hivyo inaonekana ni mwendelezo wa Lamar kuzidi kumfanyia fujo Drake katika vita vyao vya kimuziki. Mdau wa muziki Marekani, Dame Dash akizungumza na Podcast ya Moguls In The Making hapo Mei 2024, alisema licha ya Jay Z na Nas kushambuliana katika nyimbo zao, hawakuwa na wasiwasi wa kuibuka vurugu kama ilivyotaka kuwa kwa Lamar na Drake.

Dame, mwanzilishi mwenza wa Roc-A-Fella Records aliutazama mvutano wa Lamar na Drake kama ilivyokuwa  The Notorious B.I.G na Tupac miaka ya 1990 hadi kusababisha mauaji na kusema hiyo ni mbaya zaidi katika utamaduni wa Hip Hop.

Je, Whitney aliyetajwa awali kuwa nyuma ya fujo za Lamar katika anga la muziki ni nani? Huyu ni mchumba wa Lamar na walikutana wakiwa wanafunzi wa Sekondari ya Centennial huko Compton, California, kusini mwa Los Angeles. Kwa miaka mingi wamefanya uhusiano kuwa wa faragha zaidi na kwa mara ya kwanza kuonekana hadharani wote wawili ilikuwa 2014 walipokanyaga zulia jekundu la kwanza kwenye tuzo za Grammy.

“Kila mtu ambaye amekuwa karibu nami amekuwapo tangu siku ya kwanza na siwezi kubadilisha hilo. Sibadiliki kwa ajili ya mtu yeyote, watu ambao wamekuwa upande wako siku zote unatakiwa kuwaheshimu,” Lamar aliiambia Power 105.1 Radio.

Akizungumza na Billboard mwaka 2015, Lamar alisema tangu mwanzo wa uhusiano wao hajawahi kumuita Whitney msichana wake, huyo ni rafiki yake mkubwa na mtu pekee ambaye anaweza kumwambia kuhusu hofu inayomkabili kwa wakati wowote ule.  Hivyo, kama wanavyosema kuwa kwenye kila mafanikio ya mwanaume nyuma yake kuna mwanamke hodari, ndivyo ilivyo kwa Lamar na Whitney aliyetokea katika jalada la albamu yake ya tano, Mr. Morale & the Big Steppers (2022).

Mwandishi wa Jarida la New York Times toleo la 2014, Lizzy Goodman alisema alipomuuliza Lamar kati ya watu wote yupi mwenye nguvu kubwa katika simu yake, jibu lake lilikuwa moja na la mara moja kuwa ni Whitney ambaye kazaa naye watoto wawili.