Diamond aweka wazi picha ya Zuchu baada ya kujifungua
Muktasari:
- Zuchu amejifungua Agosti 2, 2026, huku taarifa za ujio wa mtoto huyo zikithibitishwa na familia. Mtoto huyo amepewa jina la Sanura, kwa heshima ya mama mzazi wa Diamond Platnumz, Sanura Kassim maarufu Mama Dangote.
MSANII wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, amewaacha mashabiki wakimiminika kwa pongezi baada ya kuweka picha ya mke wake, Zuchu, akiwa amelala kitandani hospitalini, baada ya kujifungua mtoto wao wa kwanza wa kike.
Zuchu amejifungua Agosti 2, 2026, huku taarifa za ujio wa mtoto huyo zikithibitishwa na familia. Mtoto huyo amepewa jina la Sanura, kwa heshima ya mama mzazi wa Diamond Platnumz, Sanura Kassim maarufu Mama Dangote.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Diamond amechapisha picha ya Zuchu akiwa hospitalini na kuambatanisha ujumbe mfupi uliojaa hisia za furaha kwa kumkaribisha mtoto wao duniani.
"Welcome to the world, our precious little angel. You are already loved more than words can ever say!"
Kwa Kiswahili ujumbe huo unamaanisha: "Karibu duniani, malaika wetu wa thamani. Tayari unapendwa zaidi ya ambavyo maneno yanaweza kueleza."
Muda mfupi baada ya chapisho hilo kuwekwa mtandaoni, mashabiki, wasanii na watu mbalimbali walifurika kwenye sehemu ya maoni wakitoa salamu za pongezi kwa Diamond na Zuchu, huku wengi wakiwatakia kila la heri katika safari yao mpya ya ulezi.
Chapisho la Diamond sasa limezidi kuthibitisha furaha inayotawala ndani ya familia hiyo, huku picha ya Zuchu akiwa chumba cha kujifungulia ikiendelea kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na kuibua maelfu ya salamu za pongezi kutoka kwa mashabiki ndani na nje ya Tanzania.