Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Namba za Director Kenny zinavyotisha! 

Muktasari:

  • Pia amefanya kazi na wasanii wa nje akiwemo Wizkid, Burna Boy, Davido, Rema, Joeboy, Mr. Flavour, Koffi Olomide, Tanasha Donna, Innoss’B, Jah Prayzah, Sho Madjozi na Jose Chameleone. Fahamu zaidi.

JINA la Director Kenny ni maarufu hasa katika Bongofleva kwa sababu amefanya yenye heshima kubwa na wasanii wengi ambazo amewatengenezea video kali ambazo zimewapa sifa nzuri na kuvutia fursa.

Pia amefanya kazi na wasanii wa nje akiwemo Wizkid, Burna Boy, Davido, Rema, Joeboy, Mr. Flavour, Koffi Olomide, Tanasha Donna, Innoss’B, Jah Prayzah, Sho Madjozi na Jose Chameleone. Fahamu zaidi.


1. Director Kenny alipata umaarufu baada ya kufanya kazi na Harmonize kipindi bado yupo na WCB Wasafi. Yeye na mwimbaji huyo walifahamiana wakati anafanya kazi chini na Director Hanscana kama msaidizi wake.


2. Baada ya kuondoka kwa Hanscana, video ya kwanza kwa Kenny kufanya peke yake ni ya wimbo wake Lava Lava, Dede (2017), kisha ukafuata wake Harmonize, Nishachoka (2017).


3. Tayari ameshinda tuzo mbalimbali za kimataifa ikiwemo All Africa Music Awards (AFRIMA) 2019, African Entertainment Awards USA 2021, na African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) 2021.


4. Video pekee za Harmonize (Kwangwaru - 2018), Zuchu (Sukari - 2021) na Rayvanny (Number One - 2020) ambazo zimetazamwa zaidi mara milioni 100 YouTube, zote ameongoza Director Kenny.


5. Zaidi ya asilimia 70 ya video ambazo ameongoza tangu 2017 hadi 2024, zimetazamwa zaidi ya mara bilioni 2.5 YouTube akiwa ndiye Director pekee wa video za muziki Afrika Mashariki mwenye rekodi hiyo.


6. Kati ya video tano za Diamond Platnumz ambazo zimetazamwa zaidi ya mara milioni 100 YouTube, Kenny kaongoza nne ambazo ni Yope Remix (2019), Inama (2019), Waah! (2020) na Jeje (2020).


7. Hivyo hadi sasa kati ya video za nyimbo tisa za Bongofleva ambazo zimetazamwa zaidi mara milioni 100 YouTube, ni mbili tu ambazo hazijapita mikononi mwa Director Kenny. Video hizo ni za Diamond (Nana - 2018) ambayo imeongozwa na Godfather kutokea Afrika Kusini, na Jux (Enjoy - 2023) ambayo imeongozwa na Fole X, mshindi wa Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) na AFRIMA. 


8. Video ya kwanza ya Bongofleva kufanyika katika jangwa la Sahara ambalo ndilo kubwa zaidi la joto duniani, ni yake Mbosso, Maajab (2019) na imeongozwa na Director Kenny.


9. Kenny ndiye Director pekee Bongo ambaye ametokea katika video nyingi za muziki ambazo amezisimamia, na hufunya hivyo akiwa sehemu ya simulizi ya video husika. Tayari ameonekana kwenye video za mastaa kama Nandy (Totorimi), Hamonize (Single Again), Abigail Chams (Me Too), Jux (God Design), Aslay (Follo Me), Alikiba (Sumu) na kadhalika.


10. Hadi sasa amefanya kazi na mastaa kama Diamond Platnumz, Alikiba, Rayvanny, Marioo, Zuchu, Aslay, Nandy, Mbosso, Jay Melody, Vanessa Mdee, Mwana FA, Darassa, Ruby, Mac Voice, Mimi Mars na Jux.  Wengine ni Profesa Jay, Ben Pol, AY, Dully Sykes, Young Lunya, Baba Levo, Queen Darleen, Mr. Blue, Khadija Kopa, Q Chief, RJ The DJ, Barakah The Prince, Mrisho Mpoto, Lulu Diva, Abigail Chams na kadhalika.