Mose Iyobo, Masha Love mahaba niue
Muktasari:
- Akizungumza na Mwanaspoti, Mose Iyobo alisema alichokifuata kwa Masha Love anakijua yeye hivyo ameweka pamba masikio kwa kutosikiliza maneno ya watu na kejeli zinazosemwa na watu juu ya mpenzi wake huyo.
SIKU chache tangu kusambaa kwa tetesi kwamba Mose Iyobo, dansa wa Diamond anatoka kimapenzi na staa wa Bongo Movie, Masha Love mwenyewe amevunja ukimya na kukiri ni kweli ni mtu wake na jkwamba anampenda jinsi alivyo licha ya kuchukuliwa hajatulia.
Akizungumza na Mwanaspoti, Mose Iyobo alisema alichokifuata kwa Masha Love anakijua yeye hivyo ameweka pamba masikio kwa kutosikiliza maneno ya watu na kejeli zinazosemwa na watu juu ya mpenzi wake huyo.
"Kama ule usemi usemao mapenzi ni upofu basi mimi ndo kipofu, sababu baada ya watu kufahamu kuwa nipo na Masha, kwanza walijua ni utani, tulipothibitisha wameanza kuleta kejeli kuwa, Masha hanifai sababu ni mapepe sana na hajiheshimu, mimi niwaambie tu watu hayo wanayosema mimi ndo nimependa hivyo hivyo, wasihangaike kumaliza maneno hawataweza kunirudisha nyuma," alisema Mose Iyobo.
Mose Iyobo na Masha Love walivyoanza uhusiano baadhi ya watu wengi walijua ni utani, haswa Masha Love alipoonekana katika mitandao akigombana na mwanamke aliyekuwa anadaiwa ni wa dansa huyo hadi kufikia hatua ya kuachana na wakarudiana na hadi sasa.