Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wema Sepetu atoa neno birthday ya kwanza akiwa mama

WEMA Pict

Muktasari:

  • Wema amesema hayo leo Septemba 28, 2026 wakati akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa, ikiwa ni birthday yake ya kwanza tangu aanze safari ya kuwa mama, hatua ambayo kwake imebeba maana kubwa baada ya muda mrefu wa kutamani kupata mtoto.

MWIGIZAJI na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, amesema kupata mtoto kwake ni sherehe kubwa kuliko sherehe yoyote ambayo angeweza kuandaa katika siku yake ya kuzaliwa.

Wema amesema hayo leo Septemba 28, 2026 wakati akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa, ikiwa ni birthday yake ya kwanza tangu aanze safari ya kuwa mama, hatua ambayo kwake imebeba maana kubwa baada ya muda mrefu wa kutamani kupata mtoto.

“Nafurahia sana kusheherekea birthday yangu nikiwa mama. Kuhusu kufanya sherehe kubwa, kwangu hili la kuwa na mtoto ni sherehe tosha,” amesema Wema.

WE 01

Kauli hiyo inaonyesha namna ujio wa mtoto ulivyobadilisha mtazamo wake kuhusu siku yake ya kuzaliwa, ambapo mwaka huu ameamua kuithamini zaidi furaha ya kuwa mama kuliko ukubwa wa sherehe.

Kwa Wema, Septemba 28 ya mwaka huu si kumbukumbu ya kuongeza mwaka pekee, bali ni siku inayomkuta katika ukurasa mpya wa maisha akiwa na jukumu la umama ambalo limekuwa moja ya mambo aliyoyatamani kwa muda mrefu.

WE 02

Hatua hiyo imeifanya birthday yake ya mwaka huu kuwa tofauti na zile alizowahi kusherehekea hapo nyuma, kwani safari hii anaadhimisha akiwa na jambo ambalo kwa muda mrefu lilikuwa sehemu ya matarajio yake.