Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mama Mobetto afichua siri ya muziki wa Kongo

SIRI Pict

Muktasari:

  • Kauli hiyo inaonyesha kuwa ladha ya muziki ya Mama Mobetto inagusa pande mbili, huku muziki wa dansi wa Kongo ukiwa sehemu ya muziki anaoutafuta zaidi wakati wa mapumziko na muziki wa Tanzania ukiendelea kuwa sehemu ya burudani yake.

MAMA Mobetto amefichua upande mwingine wa maisha yake ya burudani, akisema muziki wa Kongo ni miongoni mwa vitu anavyovipenda wakati anapotaka kupumzika na kupata utulivu.

Akizungumza na Mwanaspoti  jijini Mwanza, Mama Mobetto amesema anaipenda sana muziki wa dansi, lakini muziki unaotoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) una nafasi ya kipekee katika burudani yake.

Mama Mobetto amesema anapokuwa amepata muda wa kupumzika na kutaka kuwa katika mazingira ya utulivu, huamua kusikiliza nyimbo nzuri za Kongo, akieleza kuwa muziki huo ni sehemu ya burudani anayofurahia.

“Napenda sana muziki wa dansi, hasa muziki wa Kongo, nyimbo nzuri za Kongo huwa nazisikiliza wakati wa kupumzika, napenda utulivu,” amesema.

Mbali na kusikiliza nyimbo hizo wakati wa mapumziko, Mama Mobetto amesema anawakubali wanamuziki wengi wa Kongo, akionyesha jinsi muziki wa nchi hiyo ulivyoingia kwenye ladha yake ya burudani.

Kwa mujibu wa Mama Mobetto, muziki wa Kongo una kitu kinachomvutia na kumfanya autafute hasa pale anapohitaji muda wa kujituliza na kufurahia muziki bila pilikapilika.
Hata hivyo, mapenzi yake kwa muziki wa Kongo hayamaanishi kwamba muziki wa Tanzania haumvutii, kwani amesema pia husikiliza muziki mzuri unaofanywa na wasanii wa hapa nchini.

Katika muziki wa Tanzania, Mama Mobetto amemtaja pia staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, akisema nyimbo zake ni miongoni mwa kazi anazopenda kuzisikiliza.
“Hapa Tanzania pia napenda kusikiliza muziki mzuri, na huwa nasikiliza nyimbo za Diamond Platnumz,” amesema.

Kauli hiyo inaonyesha kuwa ladha ya muziki ya Mama Mobetto inagusa pande mbili, huku muziki wa dansi wa Kongo ukiwa sehemu ya muziki anaoutafuta zaidi wakati wa mapumziko na muziki wa Tanzania ukiendelea kuwa sehemu ya burudani yake.