Katarina wa Karatu ni mtamuuu balaa!
Katarina kutoka Karatu.
Muktasari:
“Mimi kwa jina ninaitwa Katarina kutoka Karatu. Natokea Dar yaani Dareda Misheni kama unaenda Singida. Kama unaenda Singida ukishapita Babati mbele kidogo kuna misheni kuna centa lakini kwetu ni pale Misheni. Hahahahah Kwetu Dar Dareda Misheni.” Ndivyo anavyoanza kujitambulisha mbele ya Mwanaspoti. Huyo ni Rosemary Massawe Urio, mwanadada mchekeshaji anayekuja juu kwa kasi kwa sasa katika fani hiyo. Mwanaspoti ilikutana na mvunja mbavu huyo anayechipukia ambapo, alifunguka mambo kadhaa ikiwamo alipotokea na unazi wake wa Yanga na Arsenal.
HANA muda mrefu tangu ajitose kwenye fani ya uchekeshaji, lakini tayari ameanza kuwashika mashabiki kutokana na kipaji kikubwa cha vunja mbavu.
“Mimi kwa jina ninaitwa Katarina kutoka Karatu. Natokea Dar yaani Dareda Misheni kama unaenda Singida. Kama unaenda Singida ukishapita Babati mbele kidogo kuna misheni kuna centa lakini kwetu ni pale Misheni. Hahahahah Kwetu Dar Dareda Misheni.” Ndivyo anavyoanza kujitambulisha mbele ya Mwanaspoti. Huyo ni Rosemary Massawe Urio, mwanadada mchekeshaji anayekuja juu kwa kasi kwa sasa katika fani hiyo. Mwanaspoti ilikutana na mvunja mbavu huyo anayechipukia ambapo, alifunguka mambo kadhaa ikiwamo alipotokea na unazi wake wa Yanga na Arsenal.
Hapo chini ndio mazungumzo yetu yalivyokuwa ambayo kwa kiasi fulani yalinifanya nibaini kipaji kikubwa cha mwanadada huyu kisura. Endelea...!
Mwanaspoti: Kwa mara ya kwanza kabisa ni lini uliingia kwenye uchekeshaji?
Katariana: Safari yangu ya uigizaji katika uchekeshaji ilianza rasmi mwaka 2012, ilikuwa katika mashindano fulani hivi, tulienda kwenye mchujo wa kuchaguliwa kuigiza kwenye tamthilia moja ya ITV iitwayo Pembe Nne.
Mwanaspoti: Ni wachekeshaji gani unawakubali zaidi?
Katarina: Ninawakubali wengi akiwemo Mc pilipili, Joti, Eric Omondi na Mamito.
Mwanaspoti: Ilikuwaje ukaingia kwenye fani hii ya uchekeshaji?
Katarina: Kuingia kwenye komedi ni baada ya watu wangu wa karibu kunishawishi na kuonyesha kwamba nina nafasi japo ni kitu nilikuwa nikipenda kukifanya, ila baada ya kuona watu wamenipokea vizuri nikapata nguvu na kujitosa jumla.
Mwanaspoti: Kwa nini Katarina wa Karatu?
Katarina: Kwasababu Wairaq wengi wanatoka Karatu nikaamua kujiita Katarina wa Karatu, japo sio Muiraq mimi ni Mmeru.
Mwanaspoti: Wazo la kuigiza na HD uliipata wapi?
Katarina: HD ni High Definition. Tulikutana Pub kila mmoja akiwa na rafiki zake, so ikawa mi ninaongea na marafiki zangu wanacheka na upande wa pili yeye akiongea na washkaji zake wanacheka....tukajumuika maana kila mmoja alikuwa anafurahisha upande wake ndipo wazo la kufanya kazi pamoja ikazaliwa. HD ndio ninayeweza kufanya naye kazi vizuri zaidi.
Mwanaspoti: Umesema uko singo? Je ni mwanaume wa aina gani ungependa kuwa naye?
Katarina: Mwanaume atakayenipenda mimi na mtoto wangu aelewe umuhimu wa kazi yangu na thamani yangu. Asinipende kwa sababu ya kipaji changu, ila anipende kwa dhati.
Mwanaspoti: Hivi huwa huoni aibu unapofanya shughuli zako?
Katarina: Hapana sioni aibu kabisa.
Mwanaspoti: Kitu gani kimewahi kukuhuzunisha zaidi maishani?
Katarina: Msiba wa shangazi yangu mpenzi Enezael Urio.
Mwanaspoti: Kitu gani hutakisahau maishani mwako?
Katarina: Dah! Uchungu wa kujifungua. Siwezui kuusahau katika maisha yangu.
Mwanaspoti: Katika komedi zako unadhani ni ipi uliitendea haki zaidi?
Katarina: Ya Sukari
Mwanaspoti: Katika mwili wako ni kiungo gani unakipenda zaidi?
Katarina: Macho aisee asikuambie mtu nayathamini na kuyapenda mno.
Mwanaspoti: Ikitokea ukakutana uso kwa uso na Rais Magufuli unadhani unaweza kumwambia mambo gani matatu?
Katarina: Hongera kwa kazi kama alivyosema HapaKaziTu. Pili ningemwambia tunaomba afufue viwanda, ili tupate ajira vijana na la mwisho tunaomba nchi itambue thamani ya wasanii, ituwezeshe tuna vipaji vingi , isipokuwa hakuna supoti
Mwanaspoti : Ni wapi huwa unatoa mawazo yako ya vichekesho?
Katarina: Maisha yanayotuzungua ndo ninapopata idea zangu.
Mwanaspoti : Nchi gani ungependa kutembelea na kwa nini?
Katarina: Natamani kwenda England, ili nikaione klabu ya Arsenal naizimia sana.
Mwandishi: Katarina wa miaka mitano ijayo atakuwa wapi?
Katarina: Katarina wa miaka 5 ijayo ni msanii mkubwa wa komedy nje na ndani ya Tanzania.
Mwanaspoti: Wewe ni mshabiki wa timu gani?
Katarina: Aisee ni Yanga wa kutupwa, Arsenal wa kugaragara kwenye matope.
Mwanaspoti: Ukipewa nafasi ya kushukuru waliokuwezesha kufika hapa utamshukuru nani?
Katarina: Baada ya Mungu na wazazi wangu, namshukuru sana meneja wangu Mc Pilipili. Yeye ndiye aliyenipa ujasiri wa kufika hapa.
Kwa taarifa zaidi nunua gazeti lako la Mwanaspoti au soma mtandaoni kupitia www.epaper.mcl.co.tz