Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jay Melody amalizane na Qing Madi

JAY Pict

Muktasari:

  • Aliwahi kufanyiwa mahojiano na chombo cha habari hapa Bongo na akaulizwa huwa anasikiliza ngoma za Tanzania na msanii yupi anampenda na angependa kufanya naye kolabo.

MKALI wa kibao cha American Love, Qing Madi kutoka Nigeria, mara kadhaa amekuwa akisifu uwezo wa msanii wa Bongo Fleva, Jay Melody na kutamani siku moja kufanya naye kolabo.

Aliwahi kufanyiwa mahojiano na chombo cha habari hapa Bongo na akaulizwa huwa anasikiliza ngoma za Tanzania na msanii yupi anampenda na angependa kufanya naye kolabo.

Bila kupepesa macho, akamtaja Jay Melody ndiye anayemkubali na kufuatilia kazi zake na akaimba moja ya mistari kutoka kwenye wimbo wa msanii huyo ‘Nakupenda’ iliyotoka mwaka 2022.

Wimbo mwingine unaotamba ni ‘Mimi na Wewe’, alioshirikishwa na rapa na mtangazaji Frida Amani.

Sio kwa bahati mbaya kwani uwezo wa Jay Melody umekuwa tishio na kila ngoma anayotoa imekuwa ikifanya vizuri kwenye media.

JA 01

Nyota huyo amejidhihirishia ni msanii anayeweza kusimama mwenyewe na kufanya mashabiki wapende ngoma zake pasipo kutumia nguvu kubwa ya kiki.

Ikumbukwe ‘Nakupenda’ ndiyo wimbo pekee uliomtambulisha zaidi mkali huyo wa kibao cha Ankali kimataifa na ulitazamwa zaidi ya mara milioni 40 YouTube.

Kwa Bongo, amefanya kolabo na wasanii wakubwa kama Diamond Platnumz kwenye wimbo wa pamoja na Mr Blue, Mapozi, ulioachiwa mwaka jana, Nishalowa na Hatari akifanya na Ali Kiba, Rayvanny (Slow, Dance) na nyinginezo.

Kimataifa, hadi sasa, ameshirikishwa na Savara kutoka kwenye kundi la Sautsol la Kenya kwenye wimbo wa Asali Mbichi ulioachiwa miezi miwili iliyopita.

JA 02

Baada ya Qing Madi kufanya challenge ya wimbo wa Mimi na Wewe kwenye kipande cha Jay Melody, mashabiki wamekuwa wakitoa maoni mitandaoni kuhusu ni lini wawili hao watatoa kolabo ya pamoja.

Hata hivyo, Qing Madi alijibu swali la kolabo aliloulizwa na shabiki kwenye mtandao wa TikTok akisema: “Napenda uimbaji wa Jay Melody, naamini mwaka huu nitafanikiwa kolabo hiyo.”


QING MADI

Jina lake halisi ni Chimamanda Pearl Chukwuma, alizaliwa mwaka 2006 na kukulia jijini Benin City, Kusini mwa Nigeria. Alianza kuimba tangu akiwa mdogo, akishiriki katika mashindano ya vipaji shuleni, pia akiimba kwenye kwaya ya watu wazima ya kanisani.

Kama ilivyo historia ya muziki wa Tyla, Qing Madi alianza kupata umaarufu mitandaoni hasa TikTok baada ya kuachia wimbo wake wa kwanza mwaka 2022, See Finish, uliosambaa na kupata umaarufu.

Tangu hapo, safari yake ya muziki ikaanza na kuachia ngoma kama Ole, Vision, Goosebumps, You Believe in Love akimshirikisha Kizz Daniel, Namipa na nyinginezo.

JA 03

Nyota huyo, ambaye anaimba aina nne za muziki, ndani ya miaka mitatu tu ya kazi yake, amenyakua tuzo ya mwandishi bora wa mwaka zilizotolewa na The Headies mwaka huu.

Kwa Tanzania  amefanya kolabo na Jux African Boy na Didi B kwenye ngoma iitwayo Loca iliyotoka wiki chache zilizopita.


JAY MELODY

Jina lake halisi ni Sharif Said Juma, alizaliwa Mwananyamala, Dar es Salaam, Juni 1997. Ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo ambaye amekuwa maarufu kutokana na sauti yake.

Ni moja ya zao la THT, chuo cha kukuza vipaji vya waimbaji nchini, na aliingia rasmi kwenye tasnia hiyo mwaka 2020.

Kabla ya hapo, alikuwa akiandikia nyimbo wasanii mbalimbali, akiwemo Nandy kwenye wimbo wa Kivuruge, uliotoka miaka saba iliyopita na kufanya vizuri nchini.

JA 04

Wimbo wake wa kwanza aliouachia, Goroka, miaka saba iliyopita, ndiyo uliomfungulia njia na jina lake kuanza kujulikana.


AMALIZE KIPORO

Jay Melody hatumii nguvu kubwa ya kiki kwenye kupromote ngoma zake, kwani sauti yake imekuwa ikigusa hisia za baadhi ya mashabiki wanaopenda nyimbo za mapenzi.

Nyota huyo amejijengea heshima kupitia nyimbo zake kama Nakupenda, Sugar na Baridi, na ameshajipata kama mwimbaji wa sauti laini na mwenye uwezo wa kuandika mashairi yanayoeleweka kirahisi kwa mashabiki.

JA 05

Kwa upande wa Qing Madi, amekuwa akiwavutia mashabiki mbalimbali kwa mchanganyiko wa Afro-fusion na RnB, akiwakilisha kizazi kipya cha wanamuziki wa kike barani Afrika.

Kushirikiana na Jay Melody kutamwezesha kugusa soko la Afrika Mashariki, ambalo nyimbo za mapenzi na dansi zimekuwa na ushawishi mkubwa. Pia, ataongeza wafuasi wapya kupitia Kiswahili, lugha inayowavutia wageni wengi nchini.

Endapo itafanikiwa, inaweza kuwapa umaarufu mkubwa na kuunganisha sauti yenye ladha ya Bongo Fleva na Afrobeat. Kwa Jay Melody, hii itakuwa nafasi ya kupanua zaidi soko lake la Afrika Magharibi, hususan Nigeria, ambako ndio kitovu cha muziki wa Afrobeat.

JA 06

Pia inaweza kumsaidia kuingia rasmi katika soko hilo lililojaa mastaa wanaosikilizwa duniani kama Tiwa Savage, Wizkid, Davido na wengine, na hivyo kuongeza mashabiki ndani na nje ya Afrika.