Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kutoka mitindo hadi Podcast: Huyu ndiye Laura Schmitt wa Dani Olmo

Muktasari:

  • Olmo na Laura waliweka wazi uhusiano wao kwa mara ya kwanza kupitia Instagram mnamo Januari 2024, ingawa taarifa zinaonyesha kuwa walianza kuwa pamoja tangu mwaka 2023.

KWA takribani miaka miwili sasa, Dani Olmo, 28, yupo kwenye uhusiano na mwanamitindo wa Ujerumani, Laura Abla Schmitt, 27. Wawili hao wamekuwa pamoja tangu staa huyo akiichezea RB Leipzig ya Ligi Kuu Ujerumani (Bundesliga).

Olmo na Laura waliweka wazi uhusiano wao kwa mara ya kwanza kupitia Instagram mnamo Januari 2024, ingawa taarifa zinaonyesha kuwa walianza kuwa pamoja tangu mwaka 2023.

Mbali na kiwango chake bora uwanjani, maisha binafsi ya Olmo hasa uhusiano wake na Laura, ni moja ya mambo yanayofanya mchezaji huyo kuzungumziwa mara kwa mara katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.

Utakumbuka Olmo ameendelea kuwa nguzo muhimu katika safu ya kiungo ya Barcelona pamoja na timu ya taifa ya Hispania ambayo ilishinda Kombe la Dunia 2026 huko Marekani ukiilaza Argentina goli 1-0 katika uwanja wa MetLife uliyopo New York.

Baada ya Olmo kuhamia Barcelona mwaka 2024 kwa ada ya uhamisho ya Euro 50 milioni, Laura pia alihamia Barcelona, na kwa sasa wanaishi pamoja katika mji huo wa Catalonia.

Tangu ahamie Hispania, Laura ameonekana mara kwa mara akiwa pamoja na Olmo katika matukio makubwa ya soka, mathalani alikuwepo wakati wa utambulisho rasmi wa Olmo kama mchezaji wa Barcelona.

Miongoni mwa matukio kutokea kwao yaliyowavutia wengi, ni kitendo cha wao kuhudhuria hafla ya 68 ya tuzo za Ballon d'Or iliyofanyika katika ukumbi wa Theatre du Chatelet jijini Paris mnamo Oktoba 2024.

Katika hafla hiyo, wawili hao walipiga picha pamoja kwenye zulia jekundu ikiwa ni moja ya kumbukumbu za awali kabisa za uhusiano wao.

Wakati wa fainali za Euro 2024 na hata kuelekea Kombe la Dunia 2026, Laura alikosolewa sana nchini Ujerumani kwa kuiunga mkono Hispania kwa sababu tu ana uhusiano na Olmo, na kusahau kuwa yeye ni raia wa Ujerumani.

Lakini Laura ni nani hasa?, huyo ni mwanamitindo, mshawishi wa chapa mitandao na mtangazaji wa Podcast, alizaliwa mwaka 1998 huko Ostfriesland, kaskazini mwa Ujerumani. Kazi zake za mitindo zinasimamiwa na kampuni ya Attached Agency.

Umaarufu wake uliongezeka baada ya kutokea katika ukurasa wa mbele wa Jarida la mitindo la Tush, toleo ambalo linaripotiwa kuuzwa sana, kitu ambacho kilimtangaza zaidi katika tasnia ya mitindo.

Tangu wakati huo Laura amefanya kazi na kampuni na chapa kubwa za urembo na mitindo duniani ikiwemo Dior, L'Oréal Paris, Guerlain, Dyson, Lever Couture na H&M.

Mara nyingi anatumia mitandao kutangaza kazi zake akiwa na wafuasi zaidi ya 566,000 katika ukurasa wake wa Instagram, vilevile anatumia TikTok ambapo kila mara huposti maudhui yanayohusu maisha yake ya kila siku, burudani na mitindo.

Aliwahi kueleza kuwa ndoto yake ni kuanzisha chapa ya mitindo, kupitia Podcast alisema anatamani kuzindua mavazi ya kuogelea na nguo za ndani za wanawake, lengo likiwa ni kuwapa wanawake kujiamini na kujivunia miili yao.

Tayari Laura ameweka wazi kuwa hapendi watu wamtambue kupitia uhusiano wake na Olmo pekee bali kupitia kazi zake binafsi. Mwaka 2024, aliiambia tovuti ya Tribuna kuwa bado hajakubali kuitwa WAG kama ilivyokuwa kwa kina Georgina Rodriguez ambaye ni mchumba wa Cristiano Ronaldo.

Utakumbuka neno WAG linamaanisha wives and girlfriends (wake na wapenzi wa wachezaji) na lilianza kutumika kuelezea wenza wa wanasoka wa kulipwa kabla ya kuenea pia katika michezo mingine.

"Video zangu fupi ninazoposti kila mara hazihusu soka, zinanihusu mimi au mpenzi wangu. Sizungumzii soka kwa sababu si eneo langu. Sina uelewa wa kutosha kuhusu mchezo huo. Sifanyi uchambuzi wala kuzungumzia klabu fulani.

"Watu wengi huniambia mimi ni mke wa mchezaji, lakini mimi sijioni hivyo. Mara nyingi nalichukulia jambo hilo kuwa utani," alisema Laura.

Hata hivyo, alikiri kuwa maudhui ya soka yana watazamaji wengi zaidi kuliko yale ya mitindo na mara chache anapoposti kuhusu soka hupata watazamaji wengi.

"Watu wasichokielewa ni kwamba ninapoposti kitu kinachohusu soka, nafanya hivyo kwa makusudi kwa sababu najua kitapata mamilioni ya watazamaji kutokana na ukosoaji ninaoupata. Ukiniambia klabu anayochezea mpenzi wangu ni mbaya, hilo halinisumbui na ni jambo lisilo na maana kwa sababu mimi si sehemu ya uendeshaji wa klabu hiyo," alisema.

Vilevile Laura ni mmoja wa watangazaji wa Podcast ijulikanayo kama Ziemlich Beste Fremde ambayo hadi sasa imeshatoa vipindi zaidi ya 143. Vipindi vipya hutolewa kila Jumatatu kupitia Spotify na Apple Podcasts kwa wasikilizaji wanaozungumza Kijerumani.