Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

J Lo kamuwekea limbwata Ben Affleck?

KAMA una mtazamo kuwa mpenzi wa zamani (ex) harudiwi, basi jaribu kuvaa viatu vya Ben Affleck dhidi ya Jennifer Lopez (J.Lo) bila shaka utafikiri kwa upande mwingine tofauti. Dunia inazunguka na mambo yanabadilika.

Lopez, 53, na Affleck, 51, walikuwa na uhusiano mwaka 2002 hadi 2004 walipoachana ila wakarudiana na kufunga ndoa hapo Julai 2022 ikiwa ni takribani miaka 20 tangu walipotengana.

Utakumbuka walipoachana Lopez alifunga ndoa na Marc Anthony (2004 - 2014) na kujaliwa watoto wawili, huku Affleck akimuoa Jennifer Garner (2005 - 2018) na walijaliwa watoto watatu.

Kati ya wanaume wanane ambao Lopez amewahi kuwa nao, ni Affleck pekee ndiye amerudiana naye. hilo linaibua swali moja - Affleck alimpenda sana Lopez au bibie kamuwekea limbwata? Hii ni kutokana na historia ya Lopez ambaye hadi sasa ameshafunga ndoa nne.

Ikumbukwe awali Lopez alikuwa na David Cruz waliyekutana shule walidumu hadi katikati ya miaka ya 1990. Baadaye Februari 1997 aliolewa na Ojani Noa kutokea Cuba na waliachana Januari 1998, huku Mahakama ikimzuia Noa kuchapisha kitabu kuhusu ndoa yao.

Mwaka 1999 hadi 2001 Lopez akawa penzini na mtayarishaji muziki, Puff Daddy au Diddy kwa sasa. Uhusiano wao ulikuwa na misukosuko mingi. Waliwahi kushtakiwa kwa kosa la kumiliki silaha na mali za wizi. 

Lopez alifunga ndoa ya pili na dansa wake, Cris Judd hapo Septemba 2001 na kudumu hadi Januari 2003. Cha kushangaza kabla ya talaka yake na Judd kukamilishwa ndipo Lopez akaanzisha uhusiano na muigizaji Ben Affleck.

Kuachana na Affleck waliyecheza pamoja filamu ya Gigli (2003) na Jersey Girl (2004), ndipo Lopez akawa na mwanamuziki Marc Anthony na kujaliwa mapacha Emme na Maximilian (2008), huku akicheza filamu ya El Cantante (2006).

Oktoba 2011 hadi Agosti 2016 Lopez akawa na uhusiano na dansa wake wa zamani Casper Smart. Kuachana kwao kukampa nafasi ya kuanzisha uhusiano na mcheza kikapu, Alex Rodriguez  hapo Februari 2017 na walikuja kuachana Aprili 2021.

Na baada ya miaka 18 ya kuzunguka huku na kule, Lopez alirudiana na Ben Affleck hapo Julai 2021. Walichumbiana kwa mara ya pili Aprili 8, 2022 na walifunga ndoa huko Las Vegas hapo Julai 16, 2022 ikiwa ni ndoa ya nne kwa Lopez.

Katika mahojiano na Diane Sawyer mnamo Novemba 2002, Lopez alimuelezea Affleck kama mtu mwenye akili sana. Mwenye upendo na kuvutia, huku akikiri baadhi ya watu waliona uhusiano wao hautafanikiwa.

“Tumezungumza juu ya hili mara nyingi sana na tulizungumza kuhusu ya jinsi watu wanavyomuona. Ni mtu tofauti kabisa na mimi, na sisi wawili kwa pamoja tulifikiria hili tunalifanyaje?” alisema Lopez.

Mwaka 2003 uhusiano wao uliandamwa sana na magazeti ya udaku, mapaparazi walikesha nao. Mwaka 2016 Lopez alilimbia jarida la People kuwa hakutaka uhusiano wao kuanikwa kwa umma, ilitokea tu. 

“Sasa angalau naweza kukuonyesha mimi ni nani. Kipindi kile watu waliamini chochote walichosoma kwenye majarida na magazeti ya udaku. Mara nyingi haikuwa kweli au ukweli ulikuwa kama theluthi moja,” Lopez aliiambia InStyle.

Kutokana na kuandamwa na vyombo vya habari, Lopez na Affleck waliamua kuahirisha harusi yao iliyopangwa kufanyika Septemba 14, 2003 huko Santa Barbara.

“Kwa sababu ya ufuatiliaji wa vyombo vya habari kuhusu harusi yetu, tumeamua kuahirisha tarehe. Tulihisi ni siku ambayo ingepaswa kuwa ya furaha na takatifu ila inaweza kuharibiwa,” walisema katika taarifa yao.

Hadi wanaachana mwaka 2004 hawakufunga ndoa hiyo. Mwaka 2016 Lopez alisema licha ya kutengana kulikuwa na upendo wa kweli kati yake na Affleck ambaye mwaka 2020 alimuunga mkono katika tuzo za Oscar.

Julai 2021 Lopez alichapisha picha Instagram akisherehekea siku yake ya kuzaliwa. Katika mchanganyiko wa picha nyingi kuna moja ilionyesha akibusiana na Affleck.

“Ninajihisi mwenye bahati na furaha na fahari kuwa naye. ni hadithi nzuri ya mapenzi ambayo tumeipata nafasi ya pili,” alisema Lopez baada ya kurudiana na Affleck.

“Ni matokeo mazuri kwamba hii imetokea kwa njia hii wakati huu katika maisha yetu ambapo tunaweza kuthamini na kusherehekea kwa kila mmoja na kuheshimiana. Tuna watoto, tunaishi maisha yetu kwa njia ambayo tunaweza kujivunia na watoto wetu kujivunia,” alisema Lopez baada ya kufunga ndoa na Affleck.

Katika mahojiano na jarida la Vogue mnamo Novemba 2022, Lopez alisema alibadilisha jina lake la mwisho baada ya kuolewa na Affleck akieleza kuwa watu bado watamuita ‘Jennifer Lopez’ ila jina lake halali kwa sasa ni ‘Mrs Affleck’.

“Sisi ni mume na mke. Najivunia hilo na sidhani kuwa hilo ni tatizo. Nina udhibiti mkubwa wa maisha na hatima yangu na ninahisi kuinuliwa kama mwanamke,” alisema Lopez aliyejitosa kwenye muziki na albamu yake ya kwanza, On the 6 (1999).