Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Esma awajia juu wanaomshambulia Diamond, familia yao

ESME Pict

Muktasari:

  • Esma ametoa kauli hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram, akisema amekuwa akiwaangalia baadhi ya watu wanaotoa maoni makali kuhusu familia yao, huku akidai kuwa si wote wanaokosoa wana nia njema.

DADA wa msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Esma Platnumz, amewajia juu baadhi ya watu wanaomshambulia kaka yake huyo mitandaoni, akidai kuwa wengine wanafanya hivyo huku wakimtamani kimapenzi.

Esma ametoa kauli hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram, akisema amekuwa akiwaangalia baadhi ya watu wanaotoa maoni makali kuhusu familia yao, huku akidai kuwa si wote wanaokosoa wana nia njema.

“Kuna muda huwa nawaangalia hivi visemaji vya Insta, utakuta mtu hii sio familia ya kuingia, wakati anatamani hata huyo Naseeb awe bwana ake hata wa ndotoni tu,” ameandika Esma.

ESM 01

Esma amesema baadhi ya watu wamekuwa wakitumia mitandao kutoa maneno ya mafumbo dhidi ya familia yao, hali iliyomfanya aamue kuanza kuwazuia kwenye ukurasa wake ili wasipate nafasi ya kuendelea kutoa kauli hizo.

“Nae eti kionekane kinacomment, sasa naanza kublock hivi vyenye vimdomo mdomo juu juu kama chuchunge, mnikome,” amesema.

Dada huyo wa Diamond pia amedai kuwa baadhi ya wanaomshambulia kaka yake wanaweza kuwa na historia binafsi inayowafanya wawe na hasira, akiwataka kutotumia mitandao kuhamishia hasira zao kwa familia yake.

ESM 02

“Vingine utakuta vinapiga mafumbo, kumbe vilishapitiwa vikaachwa vibaya, hasira uimalizie familia yake, ilikutuma!?” Alihoji.

Esma ameenda mbali zaidi kwa kudai kuwa baadhi ya wanawake wanaomkosoa Diamond wanafanya hivyo licha ya kuwa na tamaa kwake, huku akitoa kauli iliyozua mjadala kuhusu umaarufu wa kaka yake huyo.

“Mnasaliti mpaka mabwana zenu kwa tamaa na njaa zenu, nawachora tu wengine. Naseeb ni ndoto ya kila mwanamke, ukinitoa mimi dadaake,” ameandika.

Kauli hiyo imeendelea kuongeza mjadala mitandaoni, huku Esma akisisitiza kuwa hataendelea kuvumilia watu wanaoingiza familia yao kwenye mijadala kwa kutumia maneno ya mafumbo, akisema atawafungia kwenye mitandao ya kijamii.