Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Christian Bella asusia shoo ya Werrason, ashuka jukwaani

BELLA Pict

Muktasari:

  • Tukio hilo lilitokea wakati Bella akianza kutumbuiza mbele ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia shoo hiyo iliyokuwa na mwanamuziki mkongwe wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Werrason Ngiama Makanda.

MSANII wa muziki, Christian Bella amezua gumzo katika shoo ya Bambataa Royal Night iliyofanyika usiku wa Novemba 6, 2026, katika Ukumbi wa Super Dome, Masaki, jijini Dar es Salaam, baada ya kusimamisha ghafla onyesho lake na kushuka jukwaani akilalamikia ubovu wa sauti na vyombo.

Tukio hilo lilitokea wakati Bella akianza kutumbuiza mbele ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia shoo hiyo iliyokuwa na mwanamuziki mkongwe wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Werrason Ngiama Makanda.

Hata hivyo, mambo hayakwenda kama ilivyotarajiwa baada ya Bella kuanza kulalamikia ubora wa sauti na vyombo vilivyokuwa vikitumika.

BELL 01

Akiwa jukwaani, msanii huyo alichukua kipaza sauti na kueleza kutoridhishwa kwake na hali ya vyombo, akisema hawezi kuendelea kuimba katika mazingira hayo.

“Sound mbovu, vyombo vibovu, siwezi kuimba hivi,” alisema Bella kabla ya kusimamisha muziki na kushuka jukwaani.

Kitendo hicho kilikatisha onyesho lake likiwa bado halijakamilika, huku mashabiki waliokuwa ukumbini wakishuhudia tukio hilo.

BELL 02

Kwa upande mwingine, changamoto za sauti zilionekana pia katika baadhi ya maonyesho yaliyotangulia ya usiku huo, hali iliyoibua maswali kuhusu maandalizi ya kiufundi ya shoo hiyo.

Baada ya Bella kushuka jukwaani, Werrason alipanda na kuendelea na burudani akiendeleza ratiba ya shoo hiyo.