Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyoshi, Bella wamtaja Mama Mobetto, Chaz Baba ampandisha jukwaani

NYOSHI Pict

Muktasari:

  • Usiku huo uliwakutanisha mashabiki wa Twanga Pepeta pamoja na wapenzi wa muziki wa dansi kutoka maeneo mbalimbali, huku burudani ikianza kwa wasanii waliokuwa wamepewa jukumu la kusindikiza uzinduzi huo.

KAMA kuna usiku ambao mashabiki wa muziki wa dansi jijini Mwanza walipata burudani ya kutosha, basi ni Septemba 26, 2026 ambapo ukumbi wa The Climax uliwaka kwa uzinduzi wa albamu mpya ya Twanga Pepeta.

Usiku huo uliwakutanisha mashabiki wa Twanga Pepeta pamoja na wapenzi wa muziki wa dansi kutoka maeneo mbalimbali, huku burudani ikianza kwa wasanii waliokuwa wamepewa jukumu la kusindikiza uzinduzi huo.

Kwanza alikuwa Nyoshi El Saadat, aliyepanda jukwaani na kuanza kuwasha moto kwa mashabiki, kabla ya nafasi hiyo kuchukuliwa na Christian Bella, ambaye naye aliendelea kuupa usiku huo ladha yake.

Lakini wakati burudani ikiendelea, jina la mama Mobetto, mama mzazi wa mwanamitindo na msanii Hamisa Mobetto, likaanza kutajwa na wasanii waliokuwa wakipanda jukwaani, jambo lililowafanya mashabiki kuanza kuonyesha shauku ya kutaka kumuona.

Nyoshi alianza kumtaja mama Mobetto, huku Christian Bella akifanya hivyo pia, kabla ya baadaye zamu ikawa ya wenyeji wa usiku huo, Twanga Pepeta, kupanda jukwaani.

Hapo ndipo Chaz Baba, kiongozi wa Twanga Pepeta, alipochukua hatua nyingine kwa kumuita mama Mobetto mbele ya jukwaa na kumpa nafasi ya kuwa sehemu ya burudani ya usiku huo.

Mama Mobetto alipanda jukwaani huku akipokewa kwa shangwe na mashabiki. Chaz Baba akampa nafasi ya kucheza muziki pamoja na Twanga Pepeta, kabla ya kumpa kipaza sauti ili kuwasalimia na kuzungumza na mashabiki waliokuwa ndani ya ukumbi huo.

Akizungumza mbele ya mashabiki hao, mama Mobetto alisema: “Nimekuja hapa Mwanza kwa ajili ya uzinduzi wa Twanga Pepeta. Nimekuja kufurahia muziki wa Twanga na kuwa pamoja na nyinyi.”

Kisha akaongeza jambo lililowafanya mashabiki kulipuka kwa shangwe, akisema: “Mwanza ni nyumbani kwetu, kwa sababu Hamisa amezaliwa Bugando hapa Mwanza.”

Kauli hiyo ilipokewa kwa shangwe kubwa na mashabiki waliokuwa The Climax, huku jina la Hamisa Mobetto likianza kutajwa na baadhi yao.

Kwa namna hiyo, uwepo wa mama Mobetto ukawa miongoni mwa matukio yaliyoongeza ladha kwenye uzinduzi huo, ambao ulianza kwa Nyoshi El Saadat, ukafuatiwa na Christian Bella na baadaye wenyeji Twanga Pepeta kuchukua jukwaa.

Uzinduzi wa albamu ya 16 ya Twanga Pepeta iitwayo Ça va bien Live Experience, ulifanyika Septemba 26, 2026 kwenye ukumbi wa The Climax jijini Mwanza, huku mashabiki wakipata nafasi ya kushuhudia usiku uliochanganya muziki wa dansi, burudani na wageni mbalimbali.