Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Venus amng’oa kigogo Miami Open

Muktasari:

  • Venus amemtupa nje bingwa huyo wa mashindano ya Miami Open, katika mchezo mkali uliopigwa juzi usiku.

Miami, Marekani. Nyota wa tenisi duniani Venus Williams, ameshinda kwa mbinde dhidi ya mpinzani wake Jo Konta.

Venus amemtupa nje bingwa huyo wa mashindano ya Miami Open, katika mchezo mkali uliopigwa juzi usiku.

Nguli huyo mwenye miaka 37, anatarajiwa kucheza na Monica Puig wa Puerto Rico au Danielle Collins katika mchezo wa robo fainali.

Konta, mchezaji namba moja kwa ubora England, ameondolewa katika orodha ya wachezaji tenisi bora 20 wa dunia.

Hii ni mara ya kwanza kwa Konta kuondolewa katika orodha ya nyota 20 bora duniani tangu mwaka 2016.

Venus, dada wa nyota mwingine wa tenisi Serena, alitoka nyuma kabla ya kupata ushindi huo katika seti ya pili na tatu.

Hata hivyo, Konta alipoteza mwelekeo na kumpa nafasi Venus baada ya kupata maumivu kabla ya nguli huyo kushinda seti 5-7 6-1 6-2 akitumia muda wa saa mbili na dakika 19.

Venus, aliyeanza kurejea katika ubora wake, anashika nafasi ya nane kwa viwango duniani na juzi alitumia uzoefu kupata matokeo mazuri.