Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mfahamu Ester Exposito, mpenzi wa Kylian Mbappe

SHOWBIZ Pict

Muktasari:

  • Mbappe, mshindi wa Kombe la Dunia 2018 ambaye anaichezea klabu ya Real Madrid, sasa si tetesi tena bali ni rasmi kuwa Ester ndiye mpenzi wake, na hii ndio safari ya uhusiano wao.

MFUNGAJI bora wa Kombe la Dunia kwa muda wote, Kylian Mbappe kutokea Ufaransa, kabla ya kuanza kwa michuano hiyo mwaka huu alikuwa akihusishwa kuwa na uhusiano na mwigizaji wa Kihispania, Ester Exposito.

Mbappe, mshindi wa Kombe la Dunia 2018 ambaye anaichezea klabu ya Real Madrid, sasa si tetesi tena bali ni rasmi kuwa Ester ndiye mpenzi wake, na hii ndio safari ya uhusiano wao.

Mnamo Aprili, wawili hao walionekana pamoja jijini Paris, Ufaransa, ambapo walipigwa picha wakiwa kwenye mgahawa wakipata chakula cha usiku kabla ya kuelekea katika ukumbi wa mchezo wa bowling.

Wiki kadhaa baadaye, walionekana wakiwa pamoja kwenye mapumziko kisiwani Sardinia, wakati huo Mbappe alikuwa akiendelea kupona jeraha la misuli ya nyuma ya paja.

SHOW 01

Juni walipigwa picha wakiwa kisiwani Ibiza kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia 2026. Licha ya kuongezeka kwa tetesi za kuwa pamoja, hakuna kati yao aliyezungumzia hadharani aina ya uhusiano wao.

Mbappe mwenyewe alichochea zaidi tetesi za uhusiano wao baada ya kuposti kwenye Instagram Story picha ya Ester akiwa amevalia jezi ya timu ya taifa ya Ufaransa.

Pia, Mbappe alirekodiwa akitazama fainali ya Kombe la Dunia akiwa pamoja na Ester na watu wengine. Katika video hiyo, Mbappe alionekana akiwa amemkumbatia mwigizaji huyo. 

Haikuishia hapo, Oktoba Mosi wawili hao walionekana wakiwasili pamoja katika ukumbi wa Boum Boum jijini Paris wakati wa Wiki ya Mitindo ya Paris. Walikuwa wameshikana mikono wakiingia ndani ya ukumbi huo, na sasa si siri tena kuwa wawili hao ni wapenzi.

SHOW 05

Je, Ester Exposito ni nani? Mrembo huyo alianza kuvutiwa na uigizaji akiwa na umri mdogo ambapo alishiriki katika maonyesho ya jukwaani kabla ya kupata nafasi katika vipindi vya televisheni akiingiza tamthilia za Kihispania. Hata hivyo, mafanikio yake makubwa katika uigizaji yalikuja mwaka 2018 alipopata nafasi ya kuigiza katika tamthilia ya vijana ya Netflix, Elite ambapo alitumia jina la Carla Roson. 

Tamthilia hiyo ilikuwa miongoni mwa kazi zilizopata mafanikio makubwa kimataifa kupitia Netflix na kumtambulisha Ester kwa mashabiki. Alishiriki katika misimu mitatu ya kwanza ya tamthilia hiyo kabla ya kujitoa.

Akizungumza na Oprah Daily mwaka 2020, Ester alieleza jinsi mafanikio yake kwenye uigizaji yalivyobadilisha maisha na kazi yake kwa muda mfupi.

“Ndani ya miaka miwili, Elite imebadilisha maisha yangu kabisa. Ingawa nilikuwa tayari nimeigiza katika filamu mbili na kushiriki katika vipindi vingine. Mafanikio ya tamthilia hii yameleta mabadiliko makubwa katika kazi yangu, sasa watu wananifahamu kote duniani,” alisema.

SHOW 02

Katika mahojiano mengine na Jarida la Numero mwaka 2023, alisema anaamini kuwa namna tamthilia hiyo ilivyochunguza wahusika wenye tabia zinazokinzana ndivyo ilivyosaidia kuwavutia watazamaji.

Ester ambaye alizaliwa Januari 26, 2000, jijini Madrid, Hispania, akizungumza na Vogue Mexico mwaka 2025, alisema uigizaji umekuwa ndoto yake tangu akiwa mtoto.

“Tangu nilipokuwa mdogo, siku zote nilitaka kuwa mwigizaji. Sijui kwa nini, kwa sababu hakuna mtu katika familia yangu anayefanya kazi inayohusiana na uigizaji, lakini ni kana kwamba nilizaliwa nikiwa na kipaji hicho; siku zote nilijua kuwa ndicho nilichotaka kufanya,” alisema.

SHOW 04

Tangu ameondoka katika tamthilia ya Elite, ameendelea kupanua wigo wa kazi zake kupitia miradi mbalimbali ya televisheni na filamu. Ameigiza katika tamthilia kama Someone Has to Die, Veneno na Bandidos, pamoja na filamu zikiwemo Venus na Lost in the Night.

Katika tamasha la Monte-Carlo 2026, alitunukiwa tuzo ya International Golden Nymph katika kipengele cha Most Promising Talent, ikiwa ni kutambua mchango na uwezo wake katika tasnia ya burudani.

Mbali na uigizaji, Ester amefahamika katika ulimwengu wa urembo na mitindo, ameshafanya kazi na chapa mbalimbali maarufu zikiwemo Desigual, Yves Saint Laurent Beauty, Dolce & Gabbana, Marine Serre na Bvlgari.

SHOW 03

“Nataka kufurahia mitindo, kujaribu vitu mbalimbali na kutokuwa na msongo wa mawazo kuhusu hilo. Ningependa kiwe kitu kinachonipa furaha na kuniletea fursa mbalimbali,” alisema wakati akizungumza na Vogue Mexico.

Umaarufu wa Ester hauishii kwenye uigizaji, ana wafuasi zaidi ya milioni 25 Instagram, licha ya kuwa na idadi kubwa ya wafuasi kwenye mitandao ya kijamii, anahakikisha hatumii mitandao hiyo kama kipimo cha maisha yake.

“Ninaichukulia Instagram kama ilivyo: ni sehemu ndogo tu ya maisha yangu ambayo haipaswi kuwa zaidi ya hapo, bila kusahau kuwa hayo si maisha halisi kwa ujumla,” aliliambia Jarida la Numero mwaka 2023.

SHOW 02

Aliongeza kuwa ingawa anashukuru mitandao hiyo kwa kumwezesha kuwasiliana na mashabiki wake, pia hujitahidi kujitenga nayo mara kwa mara.

“Mimi binafsi hujaribu kupumzika kwa kuweka simu yangu pembeni mara kwa mara, ingawa ni vigumu kufanya hivyo kwa kiwango ninachotamani kutokana na kazi yangu,” alisema.

Licha ya kuwa na uhusiano na Mbappe ambaye ni staa mkubwa wa soka duniani, Ester anakiri kuwa mchezo huo bado ni jambo jipya kwake.

“Sijui chochote kuhusu soka, nimehudhuria mechi chache tu uwanjani katika maisha yangu. Nyumbani, hakuna mtu aliyekuwa akitazama mechi kwenye TV. Ingawa Hispania ni nchi kubwa katika soka, mimi sina utamaduni huo,” alisema katika mahojiano na Le Parisien.