Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Video-Mrema: Mimi na Lipumba kweli zilipendwa

Muktasari:

Mrema aliiambia MCL Digital leo Jumatatu, Machi 26 kwamba anapenda sana nyimbo za mwanamuzi huyo na kwa muda mrefu amekuwa akizifuatilia.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Agustino Mrema amesema yeye ni miongoni kwa watu wanaokubali muziki wa Naseeb Abdul ‘Diamond’.


Mrema aliiambia MCL Digital leo Jumatatu, Machi 26 kwamba anapenda sana nyimbo za mwanamuzi huyo na kwa muda mrefu amekuwa akizifuatilia.


“Nampenda sana Diamond si ndiyo yule aliyeimba ‘zilipendwa’ huku akitutaja mimi na Lipumba? Huyu mtoto anajua kuimba,” anasisitiza.


Mrema alisema  wimbo huo ametokea kuupenda kwa sababu unaonyesha hali halisi ya maisha yake sasa kwa kuwa ni ukweli usiopingika kwamba mimi na Lipumba sasa ni zilipendwa.


“Kweli tumekuwa wazee, wakati wetu umefika na sasa tunatakiwa kuwapisha vijana waendeleze gurudumu, lakini usifikirie mimi mzee ukajua sisikilizi muziki wa kizazi kipya nasikiliza zote na nimafurahi sana wanafanya kazi nzuri,” alisema Mrema.