Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zaha aanza kupokea simu, timu Championship zikimtaka

Muktasari:

  • Zaha mwenye umri wa miaka 33 kwa sasa hana timu baada ya kumaliza mkataba wake katika kikosi cha Charlotte FC cha Ligi Kuu Marekani alikokitumikia kwa kwa mkopo msimu mmoja uliopita akitokea Lyon aliyoichezea pia kwa mkopo akitokea Galatasaray ya Uturuki iliyomsajili kutoka Crystal Palace katika dirisha la usajili la 2023/24.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ivory Coast, Wilfried Zaha, anafukuziwa kwa kasi na timu mbalimbali za Ligi ay Champioship England ambazo zinamtaka kwenda kuzisaidia katika vita ya kupanda Ligi Kuu msimu ujao baada ya kutokuwa na timu kwa sasa.

Zaha mwenye umri wa miaka 33 kwa sasa hana timu baada ya kumaliza mkataba wake katika kikosi cha Charlotte FC cha Ligi Kuu Marekani alikokitumikia kwa kwa mkopo msimu mmoja uliopita akitokea Lyon aliyoichezea pia kwa mkopo akitokea Galatasaray ya Uturuki iliyomsajili kutoka Crystal Palace katika dirisha la usajili la 2023/24.

Mchezaji huyo aliyewahi pia kupita Manchester United kuanzia 2013–2015, amekuwa akitangatanga katika timu tofauti baada ya kuamua mwenyewe kuondoka Palace ambayo ilikuwa ikimtaka abaki, huku kila alikotua akikumbana na ushindani wa namba na kuishia kuwa mchezaji wa benchi.

Hata hivyo, timu za Southampton, Leicester City na West Bromwich Albion zinadaiwa kubisha hodi zikimtaka mchezaji huyo ambaye kwa sasa anafanya mazoezi na kikosi cha Crystal Palace kwa ajili ya kujiweka fiti. Pia menejimenti yake inadaiwa kuwa mezani na timu kadhaa za Ligi Kuu Saudi Arabia zinazoifukuzia saini yake.


Georginio Wijnaldum

CHELSEA na Manchester Unite zinadaiwa kuwasiliana na kiungo wa kimataifa wa Uholanzi, Georginio Wijnaldum, 35, kuhusu kujiunga na klabu hizo kwa uhamisho wa bure. Mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool aliondoka Al-Ettifaq ya Saudi Pro League mwanzoni mwa msimu huu.


Eli Junior Kroupi

ARSENAL inadaiwa kwamba itarudi tena katika vita ya kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth, Eli Junior Kroupi, mwenye umri wa miaka 20, katika dirisha la usajili la Januari. Inaelezwa ilishindwa kufikia uamuzi dirisha lililopita baada ya kupata kwake majeraha.


Lautaro Martinez

KOCHA msaidizi wa Arsenal, Gabriel Heinze, anadaiwa aliwasiliana na mshambuliaji wa Inter Milan, Lautaro Martinez, mwenye umri wa miaka 29, ambaye ni raia mwenzake wa Argentina, kuhusu uwezekano wa kuhamia Arsenal kabla ya dirisha la usajili kufungwa, lakini klabu hiyo ya Italia ilikataa huku taarifa zikimhusisha tena na timu hiyo.


Christian Kofane

NEWCASTLE United na Aston Villa zitaendelea na harakati kupambania usajili wa mshambuliaji wa Bayer Leverkusen, raia wa Cameroon, Christian Kofane, 20, wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa tena Januari. Hata hivyo huenda vita ikawa kubwa zaidi iwapo nyota huyo atakuwa katika ubora zaidi


Nicolas Tagliafico

MANCHESTER United iliamua kutosajili beki wa kushoto katika siku chache za mwisho za dirisha la usajili kwa sababu haikuweza kupata chaguo lenye ubora unaostahili kuimarisha kikosi, lakini kwa sasa imerejea Ufaransa ikimtaka nyota wa Lyon, Nicolás Tagliafico ifikapo Januari, mwakani.


James Garner

CHELSEA inadaiwa kwamba inataka kupunguziwa Pauni 65 milioni na Everton kwa ajili ya kiungo wa kimataifa wa England, James Garner, 25, kwa sababu ofa hiyo iliwasilishwa ikiwa imechelewa katika dirisha la usajili lililopita. Everton inamtaka mchezaji huyo katika dirisha dogo Januari, 2027.


Anthony Martial

STRAIKA wa zamani wa Manchester United na Ufaransa, Anthony Martial, 30, kwa sasa hana klabu na anatafuta njia ya kurejea katika Ligi Kuu England, ambapo Coventry City inatajwa kuanza kumfukuzia licha ya kwamba hana makali ya kipindi kile alipokuwa Old Traffoed. Nyota huyo hana timu baada ya kuondoka Mexico alikokuwa akiichezea Monterrey.


Jadon Sancho

EVERTON inadaiwa kwamba haina mpango wa kuingia katika soko la wachezaji huru licha ya kumalizika kwa dirisha la usajili ikiwa katika hali ngumu, ingawa inaelezwa kwamba Kocha David Moyes anataka kushtukiza kwa kuvuta nyota mmojawapo huku jicho lake likiwa kwa Jardon sancho


Lamine Camara

CHELSEA itakabiliana na ushindani kutoka Liverpool katika vita ya kumsajili Lamine Camara wa Monaco iwapo itaamua kurejesha nia yake kwa kiungo huyo wa Senegal mwenye umri wa miaka 22, baada ya uhamisho wake wa kwenda Stamford Bridge kuvurugika siku ya mwisho ya dirisha la usajili lililopita.