Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea yatua kwa Scott kumchomoa Bournemouth

Muktasari:

  • Kwa sasa kikosi hicho cha matajiri wa Jiji la London kipo katika mipango ya kimyakimya kuhakikisha kwamba baada ya miezi minne ijayo wanamnasa mchezaji wa kiwango kikubwa kwa sababu pengo la enzo linaweza kuonekana kadri mechi zitakavyoongezeka na ratiba kuwa ngumu.

CHELSEA inapanga kumsajili kiungo wa kimataifa wa England na Bournemouth, Alex Scott, 23, kwa Pauni 60 milioni katika dirisha lijalo la usajili wa mapema Januari 2027 ili akaongeze nguvu katika kikosi hicho baada ya kuondoka kwa Enzo Fernandez aliyetimkia Manchester City kwenye dirisha lililopita la usajili.

Kwa sasa kikosi hicho cha matajiri wa Jiji la London kipo katika mipango ya kimyakimya kuhakikisha kwamba baada ya miezi minne ijayo wanamnasa mchezaji wa kiwango kikubwa kwa sababu pengo la enzo linaweza kuonekana kadri mechi zitakavyoongezeka na ratiba kuwa ngumu.

Scott amekuwa katika kiwango bora kwenye kikosi cha Bournemouth tangu alipotua 2023, ambapo wakati wa usajili wa dirisha lililopita alikuwa akiwindwa na klabu kibao za Ulaya ikiwamo zile za Hispania alikokuwa akitakiwa na vigogo, Real Madrid, lakini hawakuendelea kumfuatilia baada ya kuulizia bei yake.

Mchezaji huyo wa kikosi cha timu ya vijana ya England anapenda kucheza kiungo wa chini, lakini mara nyingi hupandisha mashambulizi akipitia eneo la katikati, ingawa katika msimu huu makali yake yanaonekana kupungua kutokana na wachezaji aliokuwa anacheza nao wengi wao kutimka.

Chelsea pia inamfuatilia kiungo wa Monaco, Lamine Camara ambaye ilimkosa katika dakika za mwisho mwisho za dirisha lililopita la usajili, licha ya kukubaliana na ada ya kumnunua ya Pauni 47.1 milioni. Hata hivyo, Camara alikubali kurudi kikosini Monaco, huku kambi yake ikisisitiza kwamba hakutendewa haki kwa kuwa walishafikia makubaliano ya kumuuza.


Pedro Neto

ARSENAL, Manchester City na Al-Hilal zinamvizia winga wa Chelsea, Pedro Neto, na zinaweza kuwasilisha ofa ya kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 26 katika dirisha la usajili la Januari. Neto alikuwa katikati ya mjadala wa usajili wakati wa dirisha lililopita la usajili alipotakiwa kwa nguvu na Man City.


Christopher Nkunku

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ufaransa na AC Milan, Christopher Nkunku, mwenye umri wa miaka 28, alikataa ofa kutoka Manchester United na Newcastle United kabla ya kukamilisha uhamisho wa mkopo wa kurejea katika klabu yake ya zamani ya RB Leipzig wakati wa dirisha lililopita. Inaelezwa aligoma kurudi England akikumbuka alivyotendewa na Chelsea aliyoitumikia kwa misimu miwili.


Folarin Balogun

STRAIKA wa kimataifa wa Marekani, Folarin Balogun anaweza kuhamia Ligi Kuu Saudi Arabia, ambako dirisha la usajili bado liko wazi, ikielezwa timu yake ya Monaco iko chini ya shinikizo la kifedha la kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 baada ya kujiondoa katika mpango wa kuhamia Everton mwishoni mwa siku ya mwisho ya dirisha la usajili lililopita Ulaya


Jacob Murphy

KIUNGO mshambuliaji wa Newcastle United, Jacob Murphy, ana mkataba unaomalizika msimu ujao, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 31 anaweza kupewa mkataba mpya na klabu hiyo. Murphy anatafakari kuondoka kwenda zake katika timu mpya itakayompa maisha mapya ya soka


Hakim Ziyech

WINGA wa zamani wa kimataifa wa Morocco na Chelsea, Hakim Ziyech, anadaiwa kuachana na Wydad Casablanca, huku mchezaji huyo  mwenye umri wa miaka 33 akihusishwa na uhamisho kwenda klabu ya Brazil, Botafogo. Ziyech amekuwa na pandashuka katika harakati zake za kutaka kurejea kwenye ubora wake, lakini amekwama alipokuwa Wydad.


Simon Adingra

EVERTON inadaiwa kuanza kumfukuzia winga wa kimataifa wa Ivory Coast na Sunderland, Simon Adingra mwenye umri wa miaka 24 anayekipiga kwa sasa katika kikosi cha Ajax. Katika msimu uliopita mchezaji huyo aliichezea Monaco kwa mkopo, ambapo haikuridhishwa na kiwango chake ili kumbakiza. Adingra ni zao la akademi za kukuza vipaji huko Ivory Coast.


Trey Nyoni

LIVERPOOL inadaiwa kukataa ofa ya Pauni 30 milioni kutoka Nottingham Forest katika dirisha lililopita la usajilikwa ajili ya kiungo wa kimataifa wa England, Trey Nyoni, mwenye umri wa miaka 19. Hata hivyo, kwa sasa inafikiria kumuuza mchezaji huyo wakati wa dirisha dogo la usajili lijalo ifikapo Januari, 2027.


Julian Alvarez

ARSENAL bado inadaiwa kuwa na nia ya kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid na Argentina, Julian Alvarez, na kwa sasa inafanya kazi ili kufanikisha mpango huo ifikapo Januari 2027. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 pamoja na watu wake wa karibu wanaendelea kuishawishi Atletico kukubaliana na uhamisho huo baada ya kumgomea kuhamia Barcelona


Nick Woltemade

NEWCASTLE United na Juventus zinadaiwa kuanza majadiliano kuhusu uhamisho wa kudumu wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 24, Nick Woltemade, baada ya kutokuwepo kwa kipengele cha kumnunua moja kwa moja atakapomaliza muda wa mkopo mwakani. Woltemade ameshaanza kuitumikia Juventus.