Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yamal aweka rekodi mbaya LaLiga

YAMAL Pict

Muktasari:

  • Winga huyo wa Barcelona mwenye umri wa miaka 19, ambaye ana asili ya Guinea ya Ikweta na Morocco, aliweka rekodi hiyo isiyopendeza katika mchezo wa ligi dhidi ya Villarreal Jumapili, Novemba 22, 2026, baada ya kushindwa kutumia nafasi nyingine ya penalti.

MADRID, HISPANIA: LAMINE Yamal ameweka rekodi isiyopendeza katika historia ya Ligi Kuu Hispania (LaLiga), baada ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kukosa penalti tatu katika mashindano hayo.

Winga huyo wa Barcelona mwenye umri wa miaka 19, ambaye ana asili ya Guinea ya Ikweta na Morocco, aliweka rekodi hiyo isiyopendeza katika mchezo wa ligi dhidi ya Villarreal Jumapili, Novemba 22, 2026, baada ya kushindwa kutumia nafasi nyingine ya penalti.

Yamal sasa amekosa penalti tatu kati ya saba alizopiga katika LaLiga, jambo lililomfanya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufikisha idadi hiyo katika historia ya ligi hiyo.

YAMA 01

Akiwa na umri wa miaka 19 na siku 132, Yamal amevunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na mshambuliaji wa zamani wa Liverpool na Chelsea, Fernando Torres, ambaye alikuwa na umri wa miaka 20 na siku 64 alipokosa penalti yake ya tatu katika LaLiga mwaka 2004.

Kiungo wa zamani wa Real Sociedad, Lopez Ufarte, anashika nafasi ya tatu katika orodha hiyo baada ya kufikisha idadi hiyo akiwa na umri wa miaka 20 na siku 312 mwaka 1979. Naye Lafuente alikosa penalti yake ya tatu akiwa na umri wa miaka 21 na siku 174 mwaka 1929.

Jambo lingine la kushangaza ni kwamba penalti mbili kati ya tatu alizokosa Yamal ziligonga mwamba wa lango kabla ya kushindwa kuingia wavuni.

Rekodi hiyo imekuja katika siku ngumu kwa Barcelona dhidi ya Villarreal, ambapo mabingwa hao walijikuta katika wakati mgumu baada ya kuwa nyuma kwa mabao 2-0 kufikia dakika ya 56.

Kukosa penalti kwa Yamal kulikuwa pigo jingine kwa Barcelona katika jitihada zao za kurejea mchezoni na kujaribu kugeuza matokeo.

YAMA 02

Pamoja na maendeleo makubwa aliyoyaonyesha na mchango wake unaozidi kukua katika safu ya ushambuliaji ya Barcelona, takwimu hizo zinaonyesha kuwa upigaji penalti ni eneo ambalo bado anahitaji kulifanyia kazi ili kuboresha kiwango chake.

Kwa mchezaji ambaye tayari anatambuliwa kuwa miongoni mwa vipaji vikubwa vya soka duniani, hiyo si rekodi ambayo angependa kujivunia.

Hata hivyo, akiwa na umri wa miaka 19 pekee, Yamal bado ana muda wa kutosha kujifunza, kuboresha upigaji wake wa penalti na kuachana na rekodi hiyo isiyopendeza.

Wakati huohuo, Yamal ameanza vizuri msimu huu akiwa Barcelona, akifunga mabao 10 na kutoa asisti tisa katika mechi 13 za LaLiga.